Translate

Friday, August 24, 2012

Waislamu Tanzania Wagoma Kushiriki Sensa 2012


Kikundi cha waislamu Tanzania wagoma kushiriki sensa itakayofanyika Mwezi wa nane tarehe 26 mwaka 2012. 

Hizi ndio sababu zao:

Nchi imeshafanyiwa sensa mara sita 1948, 1957, 1967, 1978, 1988 na 2002. Majibu yalikuwa kama hivi. 

Mwaka                                     Waislamu      Wakristo     Wapagani
1957(Muda wa Ukoloni)           58%                 32%               10%
1967 (Muda wa Uhuru)            31.4%              33.5%            34.3%
1988 (Muda wa Uhuru)            Kipengele cha Dini kilitolewa
2002 (Muda wa Uhuru)            Kipengele cha Dini kilitolewa
2012 (Miaka 50 ya Uhuru)                                  ?

Kesi inakuja mwaka 1967 miaka kumi baada ya sensa ya wakoloni, wapagani walizidi idadi yao kwa asilimia 24.3 na waislamu walipungua kwa asilimia 26.6, na wakristo waliongezeka kwa asimilia 1.5. Yaani, asimilia 25 ya waislamu waliacha dini zao kuwa Wapagani au ilikuwaje? Madai ni kwamba, haya majibu yalicheleweshwa kutolewa na yalirushwa mitamboni bila wananchi kuelezwa habari hizi.  Waislamu, kisa cha mgomo ni kwamba hawaamini hivi vyombo vinavyo fanya hii sensa na wanataka kipengele cha dini kiwekwe au sivyo HAISABIWI MTU!!!. Wanataka kiwekwe kurekebisha makosa yaliyo pita. Habari ndio hiyo.

Hii picha hapo juu ya mashekhe Zanzibar 1962, nimeitoa Zanzinet.org

\


2 comments:

  1. Mbona tunarudi nyuma tena? Nyerere si alisema nchi yetu haina dini, ila watanzania wana dini. Nini Tena wanarudisha huu udini. Watoe hicho kipengele cha dini.

    ReplyDelete
  2. I agree with anon hapo juu, tunarudi nyuma sana

    ReplyDelete