Translate

Sunday, December 28, 2014

Ustadhi Ali Comorian Afariki Dunia


Sheikh Ali Mzee Bin Comorian ametutoka duniani. Sheikh alikuwa na madrasa yake ya kufundisha dini kwa watu wazima mtaa wa kariakoo, na ni mbunifu wa kaswida nyingi za dini hapa nyumbani. 
Mazishi yake yata fanyika kesho saa Nne(4) asubuhi, Mtaa wa Kariakoo na Likoma kwa Maalim Bahiya, na sala itafanyika msikiti wa makonde. 
Marehemu aacha mke.
Inna lillahi waina illahi rajiun. Mwenyezi Mungu amfungulie milango ya pepo, amrehemu na kumpa maghfira.

Thursday, December 25, 2014

Hadithi ya Yesu kwenye Qur'an

Hadithi ya Yesu ni moja ya hadithi ndefu sana kwenye Qur'an, ilibidi aongelewe zaidi ya ukurasa moja. Qur'an ilianza na mababu zake, familia ya Imran, mpaka kwa mama yake Mariam ikaishia kwake. Unapata na stori kidogo ya John the Baptist mwanzo wake. Hapa nimeku wekea mkusanyiko wa hadithi yake kutoka Suratul Al-Imran(Familia ya Imran), ukurasa wa 3 kwenye Qur'an aya 33-60, iliyo tafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani, mwenyezi Mungu amrehemu.


Kuzaliwa kwa Mariam

Hakika Mwenyezi Mungu alimteuwa Adam na Nuhu na ukoo wa Ibrahim na ukoo wa Imran juu ya walimwengu wote.Ni wazao wao kwa wao; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua. Alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. 

Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet'ani aliye laaniwa.Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake.Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.

Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi.  Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya(John the Baptist), ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema.Akasema Zakariya: Mola wangu Mlezi! Vipi nitapata mwana na hali ukongwe umenifikia, na mke wangu ni tasa? Akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo. Akasema: Mola wangu Mlezi! Niwekee alama. Akasema: Alama yako ni kuwa hutasema na watu kwa siku tatu, isipo kuwa kwa kuashiria tu. 

Na mdhukuru Mola Mlezi wako kwa wingi na mtakase jioni na asubuhi.Na angalia pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteuwa, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wote.Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao. Hizi ni khabari za ghaibu tunazo kufunulia; nawe hukuwa nao walipo kuwa wakitupa kalamu zao nani wao atamlea Maryamu, na hukuwa nao walipo kuwa wakishindana.


Kuzaliwa kwa Yesu

Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu).Naye atazungumza na watu katika utoto wake na katika utuuzima wake, na atakuwa katika watu wema.Maryamu akasema: Mola wangu Mlezi! Vipi nitampata mwana na hali hajanigusa mwanaadamu? Mwenyezi Mungu akasema: Ndivyo vivyo hivyo, Mwenyezi Mungu huumba apendacho.Anapo hukumu jambo, huliambia: Kuwa! Likawa.



Na atamfunza kuandika na Hikima na Taurati na Injili.Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia: Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu, ya kwamba nakuundieni kwa udongo kama sura ya ndege. Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu. Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwi nyinyi ni wenye kuamini. Na ninasadikisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale mlio harimishiwa, na nimekujieni na Ishara kutokana na Mola Mlezi wenu. Kwa hivyo mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabudni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.

Isa alipo hisi kuwa kati yao pana ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu.Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia.Na Makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga.Pale Mwenyezi Mungu alipo sema: Ewe Isa! Mimi nitakutimizia muda wako wa kuishi(Hawatakuuwa hao maadui), na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale walio kufuru, na nitawaweka wale walio kufuata juu ya wale walio kufuru, mpaka Siku ya Kiyama. Kisha marejeo yenu yatakuwa kwangu, nikuhukumuni katika yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.

Ama wale walio kufuru, nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Akhera, wala hawatapata wa kuwanusuru. Na ama wale walio amini na wakatenda mema basi Mwenyezi Mungu atawalipa ujira wao kaamili. Na Mwenyezi Mungu hawapendi madhaalimu.Haya tunayo kusomea ni katika Aya na Ukumbusho wenye hikima.Hakika mfano wa Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam; alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa! Basi akawa.Hii ni kweli itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wanao fanya shaka.

To get the english version of the same story, read my previous post here>>> 

Tuesday, December 23, 2014

Miji mikubwa iliyo anguka - Pompeii

Leo tuna tembelea Ulaya, specifically an ancient Roman town near Naples in the Italian Region of Campania called Pompei. Huu Mji pamoja na miji ya karibu Herculaneum na vimji vingine, vilifunikwa na meter 4-6 za majivu na mawe madogo, muda Mlima Vesuvius ulivyo ripuka na volcano. 

Kabla huja anza kuwaza kama ndo Sodoma na Gomora, ntakujibu, sio Sodoma na Gomora kwa sababu mbili za msingi. Hii Volcano ili errupt miaka 79 baada ya kuzaliwa kwa nabii issa(Yesu), na pia sehemu yake sio maeneo ya uarabuni. Huu Mji ulikuwa na watu 11,000, system ya maji ya kisasa, system ya kutoa maji machafu ambayo hata uingereza walikuja kuwa nayo miaka 1000 baadae, na sehemu zao za kutembea zilikuwa zimejengwa na aina ya jiwe, ambayo usiku mwezi ukitoka yale mawe yana waka mwanga kwa ku reflect mwanga wa mwezi. Yaani walikuwa na taa za barabarani zenye kuwashwa na mwezi, Upo hapo?

Sasa mji kama huu, na teknolojia yao yote, walikuwa hawajui kitu kinaitwa Volcano? Mwenyezi Mungu ni Mkubwa, mripuko ulipo anza, watu badala ya kukimbia mji, walikimbilia makwao. Kweli sisi binadamu hatujui mpaka tufundishwe na baba yetu Adam ndo aliyetutangulia na somo directly kutoka kwa Mola wa viumbe vyote, imechukua watu kufa, ndo tumejua volcano ni nini. Inakufanya mtu ufikiri, siri gani zingine za dunia hatuzijui?
Anywho, let me stop talking and let you watch how it went down on the Last Day of Pompeii. 
Enjoy!

Monday, December 22, 2014

Hadithi ya Leo - Ulimi (Tongue)


Imehadithiwa na Abdullah Bin Umar:
Sa'd bin Ubada aliuguwa na Mtume(S.A.W) pamoja na Abdur Rahman Bin Auf, Sa'd bin Abi Waqqas na Abdullah bin Mas'ud walimtembelea kumjulia hali. Alipofika, akamkuta kazungukwa na watu wake wa nyumbani, akauliza, amesha fariki? Wakajibu, hapana Mtume wa Allah. Mtume akaanza kulia, watu walivyo ona analia, na wao wakaanza kulia. Akasema,

"mnaweza kunisikiliza? Allah hamuadhibu mtu kwa machozi ya watu, wala kwa huzuni kwenye mioyo ya watu, lakini ana adhibu au ana samehe kwasababu ya hii," Akanyooshea ulimi na kuongeza, "Marehemu ana adhibiwa kwa vilio vya makelele yenye maneno kutoka kwa ndugu zake kwa ajili yake."

Umar alikuwa ana chapa watu na fimbo, na kurushia mawe and kumwagia mchanga kwenye nyuso za watu wanaolilia marehemu zao kwa makelele, maneno na vishindo.

Narrated `Abdullah bin `Umar:
Sa`d bin 'Ubada became sick and the Prophet (ﷺ) along with `Abdur Rahman bin `Auf,

Sa`d bin Abi Waqqas and `Abdullah bin Mas`ud visited him to inquire about his health.
When he came to him, he found him surrounded by his household and he asked, "Has he died?"
They said, "No, O Allah's Apostle." The Prophet (ﷺ) wept and when the people saw the
weeping of Allah's Messenger (ﷺ) they all wept. He said, 


"Will you listen? Allah does not punish for shedding tears, nor for the grief of the heart but he punishes or bestows His Mercy because of this." He pointed to his tongue and added, 
"The deceased is punished for the wailing of his relatives over him."

 `Umar used to beat with a stick and throw stones and put dust over the faces (of those who used to wail over the dead).



Thursday, December 18, 2014

Msomi wa Leo - Sh. Nurdin Muhammad ahmad aka Sh.Nurdin Kishki

Sheikh Kishki ni mzaliwa wa Dar-Es-Salaam, Tanzania. Ni sheikh kwenye Msikiti wa Vetinari uliokuwa Dar-Es-Salaam. Alisoma dini chini ya sheikh Ibrahim, Sheikh Mohamad, Sheikh Harun, Sheikh Abdul kadr na baadae akamalizia kusomea dini Al-Azhar sharif Misri.

Mwaka 1999 Sheikh alihitimu kuhifadhi Qur'ani, na akashinda mshindi wa Kwanza kwenye  mashindano ya Qur'ani ya kimataifa nchini, na wa pili mwaka wa pili. Sheikh pia alishwahi kushiriki kwenye mashindano ya Qur'ani Misri na Iran.

Alifungua madrasa yake ya kwanza, Madrasatul Iqra(mtaa wa mkamba, Changombe), na pia alifundisha madrasa ya abubakar sadiq(mtaa wa temeke, karibu na eneo la sokota). Baada ya zile madrasa kufungwa,  alianzisha Madrasa ya Istiqama maeneo ya temeke.

Sheikh ametoa Mawaidha ya Dini mikoa 16 ya Tanzania(mbeya, Iringa, Singida, Rukwa(Sumbawanga na vijiji vyake),Kigoma, Tabora, Mwanza, Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha, Zanzibar, Tanga, Morogoro, Mikoa ya Pwani). Nje ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Mozambique, Imarat (Dubai), Oman na Saudi Arabia.

Sheikh katengeneza video nyingi za dini, na pia ni Mkurugenzi wa taasisi ya kiislamu Al-Hikmah Education Center.

Msikilize mwenyewe akikuelezea historia yake na changamoto mbali mbali alizopata kwenye safari zake za dini.

Mwenyezi Mungu Amlinde na Amzidishie Elimu ya Dini na ya Dunia.

Friday, December 5, 2014

Aya za Leo - Sadaka


Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishie muda kidogo
nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema?
Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.


And spend [in the way of Allah ] from what We have provided you before death approaches one of you and he says,
"My Lord, if only You would delay me for a brief term so I would give charity and be among the righteous."
But never will Allah delay a soul when its time has come. And Allah is Acquainted with what you do.
(Qur'an 63:10-11)

Ijumaa Njema Wadau!

Tuesday, December 2, 2014

Monday, December 1, 2014

Why is India so filthy? | The Ugly Indian | TEDxBangalore

Kuna Mengi ya Kujifunza hapa, sio kila siku tusubiri serikali itufanyie, na sisi wenyewe tujitume.

Plenty of great ideas.