Translate

Monday, June 30, 2014

Saturday, June 28, 2014

When is Ramadhan in 2014 Again?

According to the Fiqh Council of N.America and Islamic Society of N.America who follow the rules that a new moon is born before the sunset in Makka, Ramadhan 1 starts on Saturday June 28th. There was also a sighting report on moonsighting.com, of a sighting on Friday, June 27th from Tucson, AZ, USA by a very experienced observer using a C-8 telescope. So Its Confirmed Ramadhan starts on June 28th there.

Mwezi Umeonekana Marekani State ya Arizona kwa kutumia darubini aina ya C-8.


Luxemburg announced Ramadhan to start on June 28th as well following the fatwa of  the European Council of Fatwa and Research, as well as many European countries that follow them.  

UAE and Saudi Authorities have stated there was no moon sighted on the Friday of June 27th, so Ramadhan starts on Sunday for them.

Bakwata didn't announce of any Sighting Reports in Tanzania, So Ramadhan Starts on Sunday  June 29th as well. 


Ramadhan Mubarak! Everyone, Stay Safe and Blessed!

Update!
Mwezi haukuonekana Marekani, kutokana na maelezo ya moonsighting.com.
 
Moonsighting.com discredited the Arizona moonsighting claim after careful review of the report,in which the observer who is one of their member agreed to it as well. Read the full report here...


Aya ya Leo - Ramadhani
Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuongoza watu na hoja zilizo wazi za uongozi na upambanuzi. Basi atakaye uona [Mwezi] katika mwezi huu afunge. Na aliye mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa ame kuongozeni ili mpate kushukuru.

The month of Ramadhan [is that] in which was revealed the Qur'an, a guidance for the people and clear proofs of guidance and criterion. So whoever sights [the new moon of] the month, let him fast it; and whoever is ill or on a journey - then an equal number of other days. Allah intends for you ease and does not intend for you hardship and [wants] for you to complete the period and to glorify Allah for that [to] which He has guided you; and perhaps you will be grateful.
"

 -- Surat Al-Baqarah 2:185

Wednesday, June 25, 2014

Perween Saeed

Perween ni mwenyeji wa mji wa Surjani Karachi, Pakistan. Ni mama wa nyumbani mwenye miaka 53, na mwanzilishi wa Kampuni ya Mama Ntilie Khana Ghar. Ana cheti cha Shahada ya kwanza kutoka chuo cha PECHS, na Shahada ya pili cha Uandishi wa Habari, kutoka Chuo kikuu cha Karachi, Pakistan. Ana mume na watoto wawili wa kike.

Mwaka 2002, ilitokea habari ya mama aliyeua watoto wake wawili sababu alikuwa hana uwezo wa kuwalisha, hii ilimshtua Perween, na kumfanya kujituma kusaidia maskini aliokuwa akiwaona kila siku, ndo hapo akapata wazo la kuanzisha shirika lake lakusadia kuwalisha maskini.

Kampuni yake ya Khana Ghar, alianzisha nyumbani kwake, akipika Roti na Mchuzi na kuwauzia watu kwa bei ya chini. Kwa Rupee 3 (Tshs.51.27), unapata Roti moja kubwa haswa ya kujitosheleza na bakuli la mchuzi.

Kwanini asifanye bure? mwenyewe anasema hakutaka watu wasio na uwezo wategemee vyakula vya bure, mtu inabidi aifanyie kazi kula yake ndo atakuwa na uchungu nayo.

Sasa hivi analisha karibia watu 2000 kwa siku mchana na jioni, na menu yake ni roti kila siku, na kila siku hubadilisha mboga, mchuzi wa choroko, mchuzi wa mboga, mchuzi wa mbaazi, ila jumapili wanapika mchuzi wa nyama. Alianza kwa kupika mwenyewe, sasa ameajiri mama wa kupika mchuzi, na roti zinapikwa na vijana watatu. Robo ya mapato yake inatoka kwa wateja, nyingine inatoka kwake, ndugu majamaa na marafiki, na wasamaria wema. Alianza na moja sasa ana tatu.
 

Mwezi wa Ramadhani anapata misaada mingi kutoka kwa watu, inawasadia kutoa mgao wa vifurushi wa vyakula bure kwa wanaohitaji. Kila kifurushi kina vyakula vifuatavyo:
Kilo 2 za Dengu
Kilo 2 za Mafuta na samli
Kilo 10 za Unga wa Ngano
Kilo 3 za Sukari
Paketi 1 ya majani ya chai
Robo Kilo ya Pilipili hoho, Giligilani, Binzari na Ukwaju
Kilo 5 za Mchele
Kilo 1 za Choroko nyeusi, choroko za manjano, tende, chumvi, maziwa ya unga na chupa ya sharbaat
Na Eid Zake Je?

Ooh She throws the grandest parties in the poorest of neighborhoods!
  
Pia kampuni yake husaidia wanafunzi wasio na uwezo kununua vitabu vya shule, nguo za shule, sanda, na pia husaidia kuchangia mabibi harusi na harusi zao kwa wale wasio na uwezo. Perween anasema, kila siku hua anatafuta jinsi ya kusaidia jamii. 

Watch her story below.
The video is in English

Inspired Yet?

source: khanaghar.org

Friday, June 20, 2014

Qaswida ya leo kutoka Tanzania - Arafa Abdillah

AKIRIMIWE MGENI NA ARAFA ABDILLAH (SANJARI)

Tusijitie aibu mgeni huyu ni mwema.
Tumuonyeshe adabu, mapenzi na kujituma.
Akirudi kwa Wahabu, Ripoti iwe ni njema.

Let's not embarrass ourselves, this guest is good.
Lets show him Good Manners, Love and Commitment
So that when he returns to God, the report should be good.


Ramadhani huyo anakuja, je umejitayarishaje kumpokea huyu mgeni?