Translate

Thursday, June 30, 2016

Best Dua For Laylatul QadrJust play the video below and read along with you or try to memorize the dua I have posted it here many many times and I am posting it again.

Wednesday, June 29, 2016

Shk. N. Kishki, Ramadhan Hadith, (10 Za Misho Alioyokuwa Akifanya Mutume...

Haya na sisi tuutafute huo usiku kwenye 10 za mwisho. Ikiwezekana we amka tu kila siku uswali, ni usiku moja wenye neema nyingi sana, usikubali ikupite.

Monday, June 27, 2016

Aya za Leo - The Righteous (Watu Wema)


Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.

They used to sleep but little of the night, and in the hours before dawn they would ask forgiveness.And from their properties was [given] the right of the [needy] petitioner and the deprived. (Qur'an 51:17-19)

 

 

Sunday, June 26, 2016

Hadithi ya Leo - Itikaf (Kukesha Msikitini na kumkumbuka Allah)

Imehadithiwa na Abu Said Al-Khudri:
Mtume wa Allah (ﷺ) alikuwa akikesha msikitini kwenye siku kumi za kati za Ramadhani, na siku moja alikesha mpaka usiku wa ishirini na moja, na ilikuwa usiku ambayo  asubuhi yake, alikuwaga akitokaga itikaf. Mtume akasema, "Yeyote aliyekuwa kwenye Itikaf na mimi abaki kwenye itikaf kwa siku kumi za mwisho, kwani niliambiwa tarehe ya usiku wa nguvu, lakini nime sahaulishwa. Kwenye Ndoto, nilijiona nikisujudu kwenye tope na maji asubuhi ya usiku huo.  Kwahiyo, utafuteni siku kumi za mwisho na iwe usiku wa witiri(i.e.21,23,25,27,29)". Ilinyesha ule usiku na paa la msikiti lili achiya, kwani lilikuwa limetengezwa na majani ya minazi. Niliona na macho yangu alama ya tope na maji kwenye paji la uso la Mtume (i.e. asubuhi ya usiku wa 21).


Narrated Abu Sa`id Al-Khudri:
Allah's Messenger (ﷺ) used to practice I`tikaf in the middle ten days of Ramadan and once he stayed in I`tikaf till the night of the twenty-first and it was the night in the morning of which he used to come out of his I`tikaf. The Prophet (ﷺ) said, "Whoever was in I`tikaf with me should stay in I`tikaf for the last ten days, for I was informed (of the date) of the Night (of Qadr) but I have been caused to forget it. (In the dream) I saw myself prostrating in mud and water in the morning of that night. So, look for it in the last ten nights and in the odd ones of them." It rained that night and the roof of the mosque dribbled as it was made of leaf stalks of date-palms. I saw with my own eyes the mark of mud and water on the forehead of the Prophet (i.e. in the morning of the twenty-first). 
( Bukhari 2027)
 

Aya ya Leo - Usiku wa Nguvu(The Night of Power)


Hakika! Tumeishusha (hii Qur'an) kwenye usiku  wa Nguvu.

We have indeed revealed this (Message) in the Night of Power.

Friday, June 24, 2016

Dua to Break your Fast - Dua ya Kufungulia

Dua - Prayer to break fast]
Ewe Allah. Nimefunga kwa ajili yako na nakuamini na nafaungua na riski yako.

Jinsi ya kuisema. 
How to say it Properly.

 
Or you can also recite.  
Pia unaweza kusoma
Dua - Prayer to break fast

Kiu kimepotea, mishipa ime lainika na Allah Akipenda, dhawabu(ya kufunga) imesha tengenezwa.
Jinsi ya kuisema.
 How to say it properly.
 
 

Aya ya Leo - Be in Good Company (Kuwa na Watu Wema)

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usimt'ii tuliye mghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake yakawa yamepita mpaka.

And keep yourself patient [by being] with those who call upon their Lord in the morning and the evening, seeking His countenance. And let not your eyes pass beyond them, desiring adornments of the worldly life, and do not obey one whose heart We have made heedless of Our remembrance and who follows his desire and whose affair is ever [in] neglect.  (Qur'an 18:28)

 Jumaa Mubarak Everyone!

Ismail Kambi Mshindi wa Mashindano ya Quran

Hongera Ismail Kambi kwa kushinda mashindano ya Afrika Mashariki! 
Mwenyezi Mungu akuzidishie Elimu ya Dini na ya Dunia.
Na washiriki wote pia ni washindi mbele ya Allah. Mwenyezi Mungu awazidishie Elimu ya Dini na ya Dunia.

I just luv this month. Yaani, ni full mahaba kwa Allah! Mashindano mengine ya kimataifa ya Qur'an. yameanza leo usiku msikiti wa mtoro baada ya Taraweh, na yatamalizika Jumapili ukumbi wa diamond Jubilee. Mashindano haya yatavuka mipaka ya Africa.
Good luck to all the participants of the Qur'an Competition that started tonight! Your all winners in front of Allah.

Diversity in Islam | Nouman Ali Khan | illustrated | Subtitled

Monday, June 20, 2016

World Refugee Day (Siku ya Wakimbizi)

 
Today is World Refugee day. Lets Pray for the Families that were forced to leave their homes in one way or another. May Allah Guide them, grant them peace and justice. For those that have died during their Journey, May Allah bless them, forgive their sins and accept them to his heaven. Don't forget to donate generously to an organization of your choice that deals with refugees.

Leo ni siku ya wakimbizi duniani. Basi tuwaombea familia zote zilizolazimika kuondoka majumbani kwao kwa njia moja au nyingine. Mwenyezi Mungu awaongoze, awape amani na awatendee haki. Na wale waliofariki wakiwa safarini, Mwenyezi Mungu awa rehemu, awa samehe madhambi yao na awapokee kwenye pepo yake. Usisahau kutoa mchango wako kwenye jumuiya unayoipenda wewe yenye kuhusika na wakimbizi.
Scholarships for the Analysis and Management of Cultural Heritage (AMCH) - Deadline July 13th 2016

Talk about a Happy Mondaaayyyy! Free College Education!!! Chuo Kikuu Bureee!!! that is my kinda talk. Folks, Go and get your PhD for free in Italy. Yup, freebies, make sure you apply before July 13th, details below. Good luck every one!

Applications are now being accepted for scholarships for the Analysis and Management of Cultural Heritage (AMCH) curriculum within the 2016/17 PhD program at the IMT School for Advanced Studies Lucca (www.imtlucca.it), one of the five Schools of Excellence in Italy.  Applications are welcome from strong candidates in any field

Instructions to navigate your way on the application page are on the link below.
https://applications.imtlucca.it/call_for_applications_xxxii/docs/guidelines.pdf

Actual page for the application to start your process can be found here...
https://applications.imtlucca.it/call_for_applications_xxxii/index.php

Friday, June 17, 2016

Aya za Leo - Hadithi ya Vijana kwenye pango (The Story of the Youth from the cave)

Bali unadhani ya kwamba wale Watu wa Pangoni na Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu.Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa wa kadhaa.Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa. 

 

Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uwongofu.Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.

 

Hawa watu wetu wameshika miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhaahiri? Na nani aliye dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu?Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.

 

Na (ungelikuwepo) ungeliona jua linapo chomoza linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni; na linapo kuchwa linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa basi huyo ni mwenye kuongoka. Na anaye muacha kupotea basi hutampatia mlinzi wala mwongozi.Nawe utawadhania wamacho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama unge watokea hapana shaka ungeli geuka kuwakimbia, kwa khofu.

 

Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidi muda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala asikutajeni kabisa kwa yeyote.Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao; na hapo hamtafanikiwa kabisa! 

 

Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti juu yao. 

 

Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao. Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ila wachache tu. Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwa yeyote yule.

 

Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na wakazidisha tisa.Sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi muda walio kaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona kulioje na kusikia kwake! Hawana mlinzi isipo kuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake. 

>>>Cont... in English 

Thursday, June 16, 2016

Aya ya Leo - Rehema (Mercy)

Nawe Sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na Urehemu nawe ni Mbora wa wanao rehemu.

So Say:"O my Lord! grant Thou forgiveness and mercy for Thou art the best of those who show mercy!" (Qur'an 23:118)


Tumemaliza siku kumi za mwanzo za mwezi wa Ramadhani, basi tumuombe Allah atusamehe madhambi yetu na atu rehemu. 

Wednesday, June 15, 2016

Hadithi ya Leo - Ukijishahau ukala ukiwa umefunga

Haya Sheikh keshaongea hapo, kwa hiyo isiwe kisingizio tena, ni mfungo kwa kwenda mbele.

Aya ya Leo - Kejeli(Ridicule)

 

Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.

O you who have believed, let not a people ridicule [another] people; perhaps they may be better than them; nor let women ridicule [other] women; perhaps they may be better than them. And do not insult one another and do not call each other by [offensive] nicknames. Wretched is the name of disobedience after [one's] faith. And whoever does not repent - then it is those who are the wrongdoers. (Qur'an 49:11)

Thursday, June 9, 2016

PRAY!


WORD!

Hamza Yusuf on the Passing of Muhammad AliAmiin!

Who's Your Bodyguard(Nani Bodyguard wako)? - Muhammad Ali

Mohammed Ali aliulizwa je una bodyguard?
Akajibu ndio anayo moja. Akamfafanua ifuatavyo...
Hana Macho, bali anaona. 
Hana Masikio, bali anasikia.
Anakumbuka kila kitu, 
Akitaka kuumba kitu, yeye huki amrisha na kina kuwa.
Husikia siri zilizo kuwa kwenye akili zilizotulia....
 Nani Huyo? Allah ndio bodyguard wake.
Powerful words indeed. Sheikh Ali just Schooled us on Allah.
Mwenyezi Mungu Amrehemu!

Tuesday, June 7, 2016

Funny Quran teacher beats up student

Hahaha! Raise your hand if this was you.
Muwe mnatuhurumia jamani mtu unaogopa kabisa kwenda chuoni.

Monday, June 6, 2016

Intent to Fast - Kutia Niya ya Kufunga

What to say when you intend to make fast.
Chakusema wakati unataka kutia niya ya kufunga.

Dua - Intent to keep fast
Natia Nia ya kufunga kesho kwa Mwezi wa Ramadhani.
Jinsi ya kuisema. 
How to say it properly.

Makkah Live HD

Yaani hizi technology, kweli Mwenyezi Mungu ni Mkubwa. Haya Ukishindwa kwenda msikitini kuswali taraweh, live from Makka. Yaani unaswali na masheikh wakumbwa kabisa ukiwa nyumbani.

99 Beautiful Names - Spoken Word by Boonaa Mohammed

Let's Kick off this Ramadhan right! Happy fasting folks 2016, you can absolutely do it. If you couldn't fast in the past, now is your chance to start. Let's get those blessings going, outweigh your sins with good, oh and don't forget to give back to your communities.
Bismillah!

Sunday, June 5, 2016

Muhammad Ali 1942-2016


Cassius Marcellus Clay, Jr.  Almaaruf Muhammad Ali  alizaliwa January 17, 1942 Lousiville, Kentucky Marekani. Alikuwa ni bondia, mpiganaji wa haki za mwananchi na za kibanadamu na Mtu wa dini.


Ali katoka kwenye familia ya watoto watano, dada moja na kaka zake wanne. Alikuwa ni bondia maarufu wa kimarekani, na alishinda Olympic Gold Medal akiwa na miaka 18. Akiwa na miaka 22 alishinda mashindano ya ubondia wa dunia mwaka 1964. Baada ya hapo alibadilisha dini na Jina akaitwa Muhammad Ali. Mwaka 1966, Ali aligoma kwenda kupigana kwenye vita vya vietnam, kitendo ambacho kilimfanya afungwe jela, na kunyanganywa pasipoti yake, na medali zake za ushindi. Mwaka 1971, alirudisha kesi yake kotini na akashinda.

Ali aliendelea kushindana kwenye ubondia, na akatoka mshindi mwaka 1974 na 1978 akapewa jina la the greatest kwasababu ya kushinda ubondia wa dunia mara tatu. Ali, alistaafu ubondia mwaka 1981. Mwaka 1984 Ali tambuliwa na ugonjwa wa Parkinsons, ni ugonjwa ambao wakati mwingine unakuja kwa ajili ya kichwa kupigizwa na kuna uwezekano aliupata kutokana na kazi yake.

Mwaka 1991 kwenye Golf War, Ali alienda Iraq kukutana na Sadam Hussein kuongea nae ili awaachie mateka wa kimarekani. Mwaka 2002, Alienda Kabul, Afghanistan kama Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa. Mwaka 2001 alipewa medali ya Presidential Citizens Medal na Raisi Clinton, na mwaka 2005 alipewa Presidential Medal of Freedom na Raisi Bush. Mwaka 2007 center ya Muhammad Ali ilifunguliwa kwenye mji wa Lousville, Kentucky.

Muhammad Ali alifariki na Septic Shock, baada ya kulazwa hospitalini siku tano kwa matatizo ya pumzi, kaacha Mke na watoto nane.

Mwenyezi Mungu amuwekee Nuru kwenye Kaburi lake, na ampokee kwenye pepo yake.

He was God Fearing and Made sure we knew about it, every chance he got.

Ramadhan 2016 Starts on Monday June 6th

Hurray! We start fasting tomorrow on Monday the 6th, so tighten those belts and let's do it right this time.  The moon sighting committee of UAE and Saudi have announced the moon was sighted in the region on Sunday June 5th. The Fiqh council of North America have also announced Ramadhan to start tomorrow. Let's wipe out our sins on the first 10 days of mercy in'shaa'llah.

Mwezi umeonekana uarabuni na wametangaza Ramadhani unaanza kesho Jumatatu Juni 6. Fiqh council ya Marekani pia wametangaza mwezi wa ramadhani kuanza kesho. Na nimesikiliza Radio Ihsan, Mwenyekiti wa  Baraza la wana Sunna Tanzania akitangaza Ramadhani kuanza Kesho, Kutokana na taarifa za Mwezi kuonekana sehemu mbali mbali ikiwemo handeni Tanga. Kwa hiyo wandugu tunaanza kufunga kesho, tujitahidi tufanye mema ili madhambi yetu yafutwe kati ya siku kumi hizi za mwanzo za msamaha.

Mwenyezi Mungu akubali funga zetu, akubali sala zetu, atusamehe madhambi yetu na atulinde na mabaya ya hii dunio, adhabu ya kaburi na moto wa Jahaman.

May Allah forgive Accept our fast, accept our prayers, forgive our sins and protect us from the bad of this world and the fire of hell .


Update!
Nimepata Habari Sheikh Jongo Kadhi wa Dar Es Salaam katangaza kwenye Radio Kheri kwamba Ramadhani inaanza Jumanne. Haya Ramadhani Njema kwa ndugu zangu watakao anza Jumatatu na wale pia watakao anza Jumanne. In'Shaa'llah Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi.

Happy Ramadhan to everyone starting on Monday and also those folks starting on Tuesday.

Thursday, June 2, 2016

Amulets - Hirizi

Haya mkayatupe kabisa yale ma kinga, toa yale mavisu na ndimu kwenye vitanda vya watoto, na yale ma hirizi na vitanzi. Usiweweseke, Allah Peke yake ndio kinga yako.