Translate

Saturday, January 31, 2015

Choo na Sinki Pamoja

Katika kupita pita zangu google, nikakutana na hii system ya kuweka sinki na Choo kwenye system mmoja.

Yaani namaanisha hivi
Na hivi..
Yaani hii system inafanya kazi hivi. Uki Flush choo baada ya kulitumia, maji masafi yanatoka kwenye hicho kibomba. Wewe una nawa zako na sabuni, unasepa. 
Maji yataendelea kutoka mpaka tank la maji ya ku flush yakijaa ndo maji yataacha yenyewe.  
Yale maji uliyo nawai mikono pamoja na maji mengine masafi ndo yataenda kwenye tank, kutumika ku flush choo. Yaani hamna cha kushika bomba la maji wala nini, ni FULL BACTERIA FREE.
Sasa kama unaona itakuwa tabu watu kusimama chooni na kunawa hapo hapo, unaweza pia kuchagua design hiyo hapo chini.
Au hii hapa

Unanunua dude zima kama lilivyo hapo juu, na kwenda kupachika tu kwako, of cause fundi bomba anahitajika. 
Yaani the choices are endless. Mie ndo naona, wenzetu wa Japan walikuwa wakiitumia hii system long time toka mwaka 1956.
Jamani kila nyumba iwe na hii system.
Mtume alituambia, msipoteze maji, hata kama unatia udhu kando ya mto wenye maji mengi.
The Prophet said, Do not waste water, even if you perform your ablution on the banks of an abundantly-flowing river.
Weekend Njema Wadau!
Monday, January 26, 2015

Mfalme Abdullah bin AbdulAziz Al Saud Afariki Dunia(1924-2015)


Mfalme wa Saudi na Mlinzi wa Msikiti Miwili Mitakatifu, Abdullah bin AbdulAziz Al Saud Alifariki Dunia tarehe 23, Januari 2015. Alichukua Ufalme mwaka 2005 baada ya kaka yake kufariki. Marehemu ni mtoto wa Ibn Saud ambayo ndo aliyo anzisha Nchi ya Saudi Arabia. Ni wakati wa ufalme wake, wanawake wali ruhusiwa kupiga kura na kushindana kwenye michezo ya Olympics.Mfalme Abdullah alifariki na Pneumonia akiwa na miaka 90.

Mfalme Akiswaliwa
 Na Kaburi Lake alipozikwa.

Innalillahi Waina Illahi Rajiun. Kwa Mwenyezi ndio tulipotoka na ndo tunapo rejea. Mwenyezi Mungu aridhike nae na ampokee kwenye Pepo yake.

Saturday, January 24, 2015

Quote of the day - Patience( Uvumilivu)Uvumilivu haimaanishi kukubali tu yaliyokutokea bila matokeo. Ina maanisha kuona mbali, na kuweka imani kwenye matokea yake. Uvumilivu una maanisha nini? Una maanisha kuangalia mwiba na kuona uwa, kuongalia usiku na kuona alfajiri. Kutokuwa na Uvumilivu, ni kuto kuona mbali na kutoweza kuona matokeo. Wampendao Mungu hawaishiwi uvumilivu, kwani wanajua muda unahitajika kwa mwezi kutoka chembe kuwa mduara.  ~Rumi

Friday, January 23, 2015

Aya za Leo - Uvumilivu (Patience)
Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri,Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.

Be sure we shall test you with something of fear and hunger, some loss in goods or lives or the fruits (of your toil), but give glad tidings to those who patiently persevere. Who say, when afflicted with calamity: "To Allah We belong, and to Him is our return". They are those on whom (Descend) blessings from Allah, and Mercy, and they are the ones that receive guidance.

(Quran 2:155-157)

Ijumaa Njema Wadau!

Wednesday, January 21, 2015

Reza Aslan: Bill Maher 'not very sophisticated'

Reza Aslan offers his reaction to Bill Maher's recent remarks regarding the link between violence and Islam.

Saturday, January 17, 2015

Quote of the day - The Human Body


This being human is a guest house. Every morning a new arrival. A joy, a depression, a meanness, some momentary awareness comes as an unexpected visitor. Welcome and attend them all! Even if they’re a crowd of sorrows, who violently sweep your house empty of its furniture, still treat each guest honorably. He may be clearing you out for some new delight. The dark thought, the shame, the malice, meet them at the door laughing, and invite them in.

Kuwa binadamu ni kama nyumba ya wageni. Kila Kukicha mgeni mpya anawasili. Furaha, Huzuni, Ubaya, kufunguka akili kwa ghafla zinakuja kama mgeni asiyetarajiwa. Wakaribishe na uwahudumie wote. Hata kama ni umati wa Huzuni, wanao kusafishia thamani zako nyumbani, lakini mhudumie kila mgeni kwa heshima zote. Anaweza kua ana kusafisha kwa furaha inayokuja. Mawazo ya giza, aibu, ouvu, kutana nao mlangoni huku unacheka, na uwakaribishe ndani.
-RUMI

Friday, January 16, 2015

Wapiga ramli kupigwa marufuku TZ

Mwaka Mpya Mambo Mapya.

Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.
Waziri wa mambo ya ndani, nchini humo, Mathias Chikawe amesema kwamba msako wa kitaifa utaanza hivi karibuni kuwakamata waganga hao na kuwafikisha mahakamani ikiwa wataendelea na kazi zao.
Watu wenye ulemavu wa ngozi, wanakabiliwa tisho kubwa juu ya maisha yao, kwani wamekuwa wakilengwa kwa sehemeu zao za mwili na waganga pamoja na wapiga ramli wanaoamini kwamba viungo hivyo huleta bahati ya kupata mali.
Chama cha maalbino nchini humo kimesifu uamuzi wa serikali kuwapiga marufuku waganga hao.
"ikiwa kutakuwepo ushirikiano kati yetu na serikali, itakuwa ndio mwanzo wa nguvu mpya ya kupambana na ukatili unaotendewa walemavu wa ngozi,'' alisema mwenyekiti mmoja wa chama hicho Ernest Njamakimaya.
"ninaamini hii ndio njia ya pekee ambayo tunaweza kutumia kupambana na ukatili huo na kuukomesha kabisa.''
'ushahidi unavyovurugwa''
Soma Habari zaidi hapa ....

Ijumaa Njema Wadau!

Tuesday, January 13, 2015

Hadithi ya Leo - Mwanaume Mwenye Kupenda Kuongea aka MmbeaAbu Said Al-Khudri( Mwenyezi Mungu Aridhike Nae) alisema:
 Mtume wa Allah(S.A.W) alisema, "Mtu Mbaya kuliko watu wote kwa Allah siku ya Kiyama, ni yule ambaye anatoa siri za Mkewe za ndani na kwenda kuzisambaza kwa watu."

Abu Sa'id Al-Khudri (May Allah be pleased with him) reported:
Messenger of Allah (ﷺ) said, "The most evil of the people to Allah on the Day of Resurrection will be the man who consorts with his wife and then publicizes her secret."


[Muslim] Book 2, Hadith 685

Thursday, January 1, 2015

Aya ya Leo - Utiifu(Obidience)


Mwenye Kumtii Mtume amemtiee Mwenyezi Mungu (Kwani anayoyaamrisha Mtume yametoka kwa Mungu). Na anayekuengeuka(anajidhuru mwenyewe). Hatukukupeleka wewe kuwa mlinzi juu yao( wakipotea ulamiwe wewe. La. Hatukufanay hivyo).

He who obeys the Messenger has obeyed Allah ; but those who turn away - We have not sent you over them as a guardian.

(Qur'an 4:80)