Translate

Thursday, April 30, 2015

Msomi wa Leo - Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (1919 - 2006)

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani, ni mshairi, msomi wa dini na mwanasiasi. Sheikh alizaliwa Stone town,Zanzibar tarehe 13 January 1919. Alifundishwa dini na baba yake Sheikh Muhsin bin Ali (1878-1953) na wanazuoni wengine wa Afrika ya Mashariki.

Sheikh alivyo maliza sekondari akiwa na miaka 18, aliendelea na elimu ya dunia kwenye Chuo Kikuu cha Makerere Uganda na kusomea ukulima.

Mwaka 1942 Sheikh aliajiriwa na serikali kama afisa msaidizi wa kilimo mwangapani.  Mwaka 1947 Sheikh aliacha kazi ya serikali na akawa Mhariri Mkuu wa gazeti la Mwongozi kwa muda wa miaka kumi na tano.  Mwongozi lilikuwa ni gazeti la siasa, la ijtimaa na la dini. Na lilikuwa maarufu kwa kazi yake kubwa ya kudai haki za wananchi na kutapakaza misingi ya Kiislamu huko Zanzibar na sehemu mbali mbali za Afrika ya Mashariki.

Sheikh Al-Barwani alijiunga na chama cha Zanzibar Nationalist Party na alifanya juhudi nyingi ili  Zanzibar ipate Uhuru kutoka kwa Muingereza. Hapo alikuwa maarufu kwa jina la "Zaim" yaani Mwongozi. Mwaka 1961 Sheikh alichaguliwa kuwa Waziri wa Elimu na Waziri wa Mambo ya Ndani, kisha akawa Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje katika serekali ya kidemokrasia ya Zanzibar. Wakati wa Uongozi wake, alikuwa katika harakati za kuondoa ubaguzi zenj, na aka hamasisha uchaguzi wa kura na aka hakikisha walimu wanapewa likizo ya uzazi na kulipwa.

Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Sheikh aliwekwa jela kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bila ya mashtaka, kwa sababu ya fikra zake za kisiasa.Alivyo achiwa, alihamia Kenya, alafu akaenda Misri, baada ya muda akarudi Kenya na mwisho yeye na familia yake wakahamia Dubai.  Mwaka 1989 mke wake wa zaidi ya miaka 25 alifariki dunia.
 

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ameandika vitabu vingi vya dini, lakini anajulikana kwa kazi yake kubwa ya kutafsiri Qur'an kwa kiswahili cha ki unguja, pamoja na kitabu chake cha utenzi cha mashairi ya Kiswahili wa beti 1300 juu ya maisha ya Mtume (s.a.w.).

Sheikh Alifariki dunia tarehe 20 March mwaka 2006 akiwa na miaka 86, Mji wa Muscat, Oman. 
Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake, amwekee Nuru kwenye Kaburi lake na ampokee Kwenye Pepo yake. 

Read his story in English here>>> 

Friday, April 24, 2015

Maongezi yako na Allah yakoje? How do you converse with Allah?

Sami Yusuf - Ala Bi Dhikrika (Your Remembrance) - Kumbukumbu yako
Basi leo tuanze maongezi yetu hivi!
Jumaa Mubarak!

Thursday, April 23, 2015

Mawaidha ya Leo kutoka kwa Mufti MenkSheikh kasema yote. Huwa nampenda huyu sheikh cause anaishi kwenye dunia ya leo, yaani he's a realist.
Mambo ya majini na mapepo sikuhizi imekuwa too much sasa, mpaka watu wanasahau kuishi maisha yao ya kila siku. 
Happy Thursday Folks!

Friday, April 17, 2015

Aya ya Leo - Asili ya binadamu (Origins of the Sons of Adam)


Aliumbwa na maji yaliyotoka kati ya uti wa mgongo na mbavu.

He was created from a fluid, ejected. Emerging from between the backbone and the ribs.(Qur'an 86:6-7)
Jumaa Mubarak!

Africa 360 - Xenophobia in South Africa: myth or reality?

Xenophobia - Intense or irrational dislike or fear of people from other countries.
Kwa kiswahili, ni chuki  au uoga wa watu kutoka nchi zingine.Is South Africa really Xenophobic or is it as the guy on the video says, local businesses afraid of a little competition, and so they fill the locals with fear and incite violence.

Wednesday, April 15, 2015

Aya ya Leo - Asili ya binadamu (Origins of the Sons of Adam)

 Kwahiyvo mwache binadamu aangalie aliumbwa na kitu gani.
So let man observe from what he was created. 
 (Qur'an 86:5)

Friday, April 10, 2015

Aya ya Leo - Mwangalizi(Protector)


Hamna Nafsi ambayo haina mwangalizi juu yake.
There is no soul but that it has over it a protector. (Qur'an 86:4)

Saturday, April 4, 2015

Moja ya Mapango makubwa duniani Vietnam

Yaani hili pango ni kubwa mno, wamelirekodi kutumia drones(zile ndege
ndogo kama toy) wakaiwekea video camera, basi ikazunguka karibia pango
zima. Yaani pango lina  msitu na mto wake wenyewe.
Just Watch and Enjoy God's creation.

Ni Mji chini ya Mji. 
Hivi yale mapango yetu ya Amboni Tanga, tunashindwa kweli kutuma kijidenge cha toy na HD cam corder ichukua video ya pango nzima? Maana hii ni marketing tosha kwa Vietnam, ma tourist wata miminika  kuiona this major wonder of the world that we do not know of.

Poleni Kenya

Jamani Majirani zetu Poleni kwa huu msiba mkubwa mliouapata. Mwenyezi Mungu awapeni hekima na Amani kuweza kuli kabili hili Janga, na awapokee vyema marehemu waliotangulia kwake In'Shaa'llah.

Friday, April 3, 2015

Aya ya Leo - Uzinzi (Adultery)


Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.

And come not near unto adultery. Lo! it is an abomination and an evil way.  
(Qur'an 17:32)
Have a Peaceful Friday!