Translate

Friday, May 29, 2015

Aya ya Leo - Mlalamikaji(Whiner)


Na katika watu wapo wanao sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu. Lakini wanapo pewa maudhi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wanayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapo kuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi husema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi. Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliomo vifuani mwa walimwengu?

And of the people are some who say, "We believe in Allah ," but when one [of them] is harmed for [the cause of] Allah , they consider the trial of the people as [if it were] the punishment of Allah . But if victory comes from your Lord, they say, "Indeed, We were with you." Is not Allah most knowing of what is within the breasts of all creatures?  (Qur'an
29:10)

Friday, May 22, 2015

Aya ya Leo - Utiifu kwa Wazazi(Obeying your Parents)


Na tumemuusia mwanaadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watakushikilia unishirikishe Mimi na usiyo kuwa na ujuzi nayo, basi usiwat'ii. Kwangu Mimi ndio marejeo yenu, na nitakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda. 

And We have enjoined upon man goodness to parents. But if they endeavor to make you associate with Me that of which you have no knowledge, do not obey them. To Me is your return, and I will inform you about what you used to do.(Qur'an 29:8)

Tuesday, May 19, 2015

Ramadhan Countdown - Happy Shaaban 2015

Alhamdullilah Tumemaliza Mwezi wa Raajab, tuna anza mwezi wa Shaaban ile tuweze kuu karibisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Bi Aisha Mwenyezi Mungu Aridhike Nae, ali hadithia kwamba Mtume wa Allah (S.A.W) alikuwa anafunga siku nyingi sana kwenye huu mwezi. Basi In'Shaa'llah na sisi tujihatihidi kufunga angalau siku chache za huu mwezi na sisi tukombe madhawabu ya bure bure.

Friday, May 15, 2015

Aya ya Leo - Wema (Righteous)


Na walio amini na wakatenda mema, kwa yakini tutawafutia makosa yao, na tutawalipa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda. 

Those who believe and work righteous deeds,- from them shall We blot out all evil (that may be) in them, and We shall reward them according to the best of their deeds. (Qur'an 29:7)
Jumaa Mubarak!

Monday, May 11, 2015

Hadithi ya Leo - Huruma


Imehadithiwa na Jarir bin Abdullah"
Mtume alisema, " Yule asiye onyesha huruma kwa wengine, na yeye hata onyeshwa huruma."

Narrated Jarir bin `Abdullah:
The Prophet (ﷺ) said, "He who is not merciful to others, will not be treated mercifully.
(Bukhari 6013)
Jumatatu Njema Wadau!

Saturday, May 9, 2015

Mafuriko ya Dar

Nime fowardiwa hii video ya huyu binti, simjui wala hanijui, lakini nimesikitishwa mno. Jamani, mjini hakuendiki, na hata ukikaa nyumbani hali ni hivi. Inatia Huruma mno, yaani kwanza kujenga nyumba bongo it takes years, kwasababu wengi wetu hatuna mambo ya kuchukua mikopo.Sasa mtu umechakarika mpaka umejenga nyumba yako, na kuitengeneza vizuri ndani na finishing na furniture nzuri. Alafu hiyo sehemu mliouziwa kiwanja mjenge amabayo imekuwa cleared na serikali kwa ujenzi, hauna miundombinu ya kuku support wewe mwenye nyumba.

Yaani jamani hivi serikali mnawezaje kuwacha viwanja viuzwe sehemu ambayo bado hamjaiweka sawa ili watu waweze kujenga na wasipata hizi hasara. Angalia huyo mdada, tiles zake, furniture zake, sijui washing machine na vitu vingine vingi familia yake imejipiga ili wawe na maisha bora, leo poof imetoweka. Nani atamsadia kununua vitu upya? Na inavyo onekana wala hakai bondeni.

Mi naona tatizo ni hivi, Idara ya Ardhi ya dar hawana proper procedure ya ku approve ujenzi. Kama sehemu haina miundo mbinu ya kutosha, msiwe mna approve ujenzi wakati mabomba ya maji machafu na masafi hamna, wala njia za maji za mvua za size ya kutosha hamna. Kama bado mnataka ku approve na serikali haina hiyo hela ya kutengeneza hiyo sehemu(Which they never do), mtu akitaka kujenga magorofa ya nyumba nyingi, alizamishwe kuchangia kwenye miundo mbinu ya ku support huo ujenzi. Kwa mfano, ajenge njia nzuri iliyo nyanyuka kwa watu kutembea, aweke mifereji ya ku channel maji ya mvua tena zifunikwe sio mambo ya watu na magari kudumbukia humo, kama pipe ya city ni ndogo, achangie kulipia kubadilisha pipe za maji machafu na masafi za mji ziwe kubwa kumsupport yeye na wakazi wake. Yaani kuwe na regulations na standards za size ya mabomba, mifereji na mifereji yote ifunikwe, tumechoka kusikia watu wamekufa kwa kuanguka kwenye mifereji.

Pole kwa hii familia, Kwakweli huu ni mtihani mzito, Mwenyezi Mungu yupo na atawa fungulia riziki Inshallah. Qur'an inatuambia, kwenye uzito wepesi unakuja.

Friday, May 8, 2015

Aya ya Leo - Juhudi (Effort)Na anaye fanya juhudi basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.

And whoever strives only strives for [the benefit of] himself. Indeed, Allah is free from need of the worlds.  (Qur'an 29:6)

Tuesday, May 5, 2015

Qaswida ya Leo kutoka U.A.E - Ahmed Bukhatir

♦O Most Magnificent! ♦ يا عظيم ♦ Ahmed Bukhatir ♦ Ya Illahi♦


Ahmed Bukhatir kazaliwa Sharjah, United Arab Emirates tarehe 16 October 1975. Ni Mtoto wa tano kati ya watoto Kumi. 

Bukhatir alianza kuimba Qaswida toka akiwa na miaka 20, na akatoa album yake ya kwanza mwaka 2000. Alivyo kuwa na miaka 29, alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya Mahusiano ya Umma ya Promax ME.Sasa ni Mwenyekit wa kampuni ya McFadden Group of Companies, yenye kushughulika na mambo ya ujenzi. 

Read his Biography in English Here>>>

Monday, May 4, 2015

Hadithi ya Leo - Mmea


Imehadithiwa na Anas bin Malik:
Mtume alisema, "Kama Muislamu akipanda mmea wowote na binadamu au mnyama akaula, atapewa malipo yake kama vile alitoa sadaka ".

Narrated Anas bin Malik:
The Prophet (ﷺ) said, "If any Muslim plants any plant and a human being or an animal eats of it, he will be rewarded as if he had given that much in charity." (Bukhari 6012 )
Happy Monday!

Friday, May 1, 2015

Aya ya Leo - Ibada(Worship)

Haiwezi kuwa mtu aliye pewa na Mwenyezi Mungu Kitabu na hikima na Unabii kisha awaambie watu: Kuweni wa kuniabudu mimi badala ya Mwenyezi Mungu. Bali atawaambia: Kuweni wenye kumuabudu Mola Mlezi wa viumbe vyote, kwa kuwa nyinyi mnafundisha Kitabu na kwa kuwa mnakisoma.

It is not (possible) that a man, to whom is given the Book, and Wisdom, and the prophetic office, should say to people: "Be ye my worshippers rather than Allah's": on the contrary (He would say) "Be ye worshippers of Him Who is truly the Cherisher of all: For ye have taught the Book and ye have studied it earnestly." (Qur'an 3:79)