Translate

Monday, October 30, 2017

Why was there never a black Prophet !!! - Sh Omar Suleiman

Kwanini Hakujawai kuwa na Mtume Mweusi?

I nearly chocked on my water. I bet you didn't see that one coming.
Looks like I need to bring back the Monday Hadith series, we seem to be missing out.
Happy Monday everyone, have a wonderful and eventful week.

Friday, October 27, 2017

Aya ya Leo - Usimzulie Allah Msiyojajua (Don't Say about Allah what you don't know)Na wanapo fanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu. Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua?

And when they commit an immorality, they say, "We found our fathers doing it, and Allah has ordered us to do it." Say, "Indeed, Allah does not order immorality. Do you say about Allah that which you do not know?" (Qur'an 7:28)
 Jumaa Mubarak!

Monday, October 23, 2017

Mawaidha ya Leo (Muda) (Time) - Mufti Menk


Kweli Siku hizi kuna distractions nyingi. Siku inaisha unajikuta mtu umepoteza muda wako kwenye vitu visivyo na maana na wala havija kuongeza kifikra, kidini wala kimaendeleo.

Vitu vya Kutafakari!
Mwenyezi Mungu Tuepushe na Tuongoze.
Jumatatu Njema wadau, Mwenyezi Mungu akujaalie wiki yako iwe na maendeleo mema.

Friday, October 20, 2017

Aya ya Leo - Chunga Nafsi Yako (Guard Your Soul)

Enyi mlio amini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni walio potoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Ni kwa Mwenyezi Mungu ndio marudio yenu nyote; basi atakwambieni yale mliyo kuwa mkiyatenda.

O you who have believed, upon you is [responsibility for] yourselves. Those who have gone astray will not harm you when you have been guided.  To Allah is your return all together; then He will inform you of what you used to do. (Qur'an 5:105)

Jumaa Mubarak!

Monday, October 16, 2017

Qur'an Recitation by Yaseen Rajab from Syria!

 Lets start our week right.
God Gifted Talent of Syrian Kid ~ Amazing Quran Recitation, imitates Abd...


Mashaallah! May Allah bless him and his family with all of his heart's desire in this world and the next.
Have a blessed week.

Friday, October 13, 2017

Aya za Leo - Adabu (Manners)


Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri,Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili, na wanaficha fadhila alizo wapa Mwenyezi Mungu. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya fedheha, Na ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu, wala hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho; na yule ambaye Shet'ani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya mno.

Worship Allah and associate nothing with Him, and to parents do good, and to relatives, orphans, the needy, the near neighbor, the neighbor farther away, the companion at your side, the traveler, and those whom your right hands possess.
Indeed, Allah does not like those who are self-deluding and boastful.Who are stingy and enjoin upon [other] people stinginess and conceal what Allah has given them of His bounty - and We have prepared for the disbelievers a humiliating punishment,And [also] those who spend of their wealth to be seen by the people and believe not in Allah nor in the Last Day. And he to whom Satan is a companion - then evil is he as a companion.
(Qur'an 4:36-38)
Ijumaa Njema Wandugu!

Friday, October 6, 2017

Aya za Leo - Jibril na Mikail (Gabriel and Michael)

Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Say, "Whoever is an enemy to Gabriel - it is [none but] he who has brought the Qur'an down upon your heart, [O Muhammad], by permission of Allah, confirming that which was before it and as guidance and good tidings for the believers." (Qur'an 2:97)

Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.

Whoever is an enemy to Allah and His angels and His messengers and Gabriel and Michael - then indeed, Allah is an enemy to the disbelievers. (Qur'an 2:98)

Jumaa Mubarak!