Translate

Friday, August 3, 2012

Msomi wa Leo - Ahmed Deedat (1918-2005)

Nitakuwa sijaitendea hii blog haki, kama sijamsema muanzilishi wa mijadala kulinganisha dini kati ya uislamu, ukristo na uyahudi Ahmed Hussein Deedat.  Muafrika kusini ambaye ni moja wa waanzilishi wa Islamic Propagation Centre International (IPCI) iliokuwa Afrika Kusini. Nia yao ilikuwa kuchapisha vitabu tofauti kuhusu dini ya kiislamu, na kutoa madarasa kwa waislamu wapya waliosilimu. Pia alianzisha As-Salaam Educational Institute kwenye mji wa Braemar. Anajulikana kwa vitabu vyake alivyo andika kuhusu tofauti ya uislamu na ukristo, na mijadala yake mingi aliyo fanya na wakristo wakubwa wa dini. Alikuwa pia anatoa hotuba nyingi kwenye maswala ya kulinganisha dini tofauti, na alikuwa ni msomi wa Quran na Biblia. Alizaliwa mwaka 1918 akafariki 2005, na alikuwa na mke moja na watoto watatu (wavulana wawili na msichana moja) .

Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi

Msikilize mwenyewe akiwa kwenye moja ya hotuba zake.
Alikuwa mkali huyo.No comments:

Post a Comment