Translate

Friday, July 26, 2019

Aya ya Leo - Nafsi yako (Your Soul)

Take care of your soul.

 Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.

Whoever does good, its for his own soul, and whoever does evil, it is against it; and your Lord is not in the least unjust to the servants. (Qur'an 41:46)
Jumaa Mubarak!

Friday, July 19, 2019

Aya ya Leo - Kusamehe (To Forgive)Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.
And the recompense of evil is punishement like it, but whoever forgives and amends, he shall have his reward from Allah, surely He does not love the unjust. (Qur'an 42:40)

Friday, July 12, 2019

Aya ya Leo - Malaika (Angels)


Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!

And they make the angels-- them who are the servants of the Beneficent Allah, female(divinities). What! did they witness their creation? Their evidence shall be written down and they shall be questioned. (Qur'an 43:19)
Jumaa Mubarak!

Friday, July 5, 2019

Aya ya Leo - Matamanio (Desire)

Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.

Whoever desires the harvest of the Hereafter - We increase for him in his harvest. And whoever desires the harvest of this world - We give him thereof, but there is not for him in the Hereafter any share.
(Qur'an 42:20)