Translate

Sunday, June 5, 2016

Muhammad Ali 1942-2016


Cassius Marcellus Clay, Jr.  Almaaruf Muhammad Ali  alizaliwa January 17, 1942 Lousiville, Kentucky Marekani. Alikuwa ni bondia, mpiganaji wa haki za mwananchi na za kibanadamu na Mtu wa dini.


Ali katoka kwenye familia ya watoto watano, dada moja na kaka zake wanne. Alikuwa ni bondia maarufu wa kimarekani, na alishinda Olympic Gold Medal akiwa na miaka 18. Akiwa na miaka 22 alishinda mashindano ya ubondia wa dunia mwaka 1964. Baada ya hapo alibadilisha dini na Jina akaitwa Muhammad Ali. Mwaka 1966, Ali aligoma kwenda kupigana kwenye vita vya vietnam, kitendo ambacho kilimfanya afungwe jela, na kunyanganywa pasipoti yake, na medali zake za ushindi. Mwaka 1971, alirudisha kesi yake kotini na akashinda.

Ali aliendelea kushindana kwenye ubondia, na akatoka mshindi mwaka 1974 na 1978 akapewa jina la the greatest kwasababu ya kushinda ubondia wa dunia mara tatu. Ali, alistaafu ubondia mwaka 1981. Mwaka 1984 Ali tambuliwa na ugonjwa wa Parkinsons, ni ugonjwa ambao wakati mwingine unakuja kwa ajili ya kichwa kupigizwa na kuna uwezekano aliupata kutokana na kazi yake.

Mwaka 1991 kwenye Golf War, Ali alienda Iraq kukutana na Sadam Hussein kuongea nae ili awaachie mateka wa kimarekani. Mwaka 2002, Alienda Kabul, Afghanistan kama Mjumbe wa Amani wa Umoja wa Mataifa. Mwaka 2001 alipewa medali ya Presidential Citizens Medal na Raisi Clinton, na mwaka 2005 alipewa Presidential Medal of Freedom na Raisi Bush. Mwaka 2007 center ya Muhammad Ali ilifunguliwa kwenye mji wa Lousville, Kentucky.

Muhammad Ali alifariki na Septic Shock, baada ya kulazwa hospitalini siku tano kwa matatizo ya pumzi, kaacha Mke na watoto nane.

Mwenyezi Mungu amuwekee Nuru kwenye Kaburi lake, na ampokee kwenye pepo yake.

He was God Fearing and Made sure we knew about it, every chance he got.

No comments:

Post a Comment