Aya za Leo - Hadithi ya Vijana kwenye pango (The Story of the Youth from the cave)
Bali unadhani ya kwamba wale Watu wa Pangoni na
Maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?Vijana hao walipo kimbilia kwenye pango walisema: Mola wetu Mlezi! Tupe rehema
itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo
letu.Tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda
wa miaka kadhaa wa kadhaa.Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi
mawili lilio hisabu sawa muda walio kaa.
Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao
walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na
Sisi tukawazidisha uwongofu.Na tukazitia nguvu nyoyo zao walipo simama na
wakasema: Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Hatutamwita
mwenginewe kabisa badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo
itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.
Hawa watu wetu wameshika miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi
hawawatolei uthibitisho ulio dhaahiri? Na nani aliye dhaalimu zaidi kuliko
anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu?Na mkijitenga nao na vile wanavyo viabudu badala ya
Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, akufungulieni Mola wenu Mlezi rehema
yake, na akutengenezeeni ya kukufaeni katika mambo yenu.
Na (ungelikuwepo) ungeliona jua linapo chomoza linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni; na linapo kuchwa linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika
uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi
Mungu. Ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa basi huyo ni
mwenye kuongoka. Na anaye muacha kupotea basi hutampatia mlinzi wala mwongozi.Nawe utawadhania wamacho, na hali wamelala. Nasi
tunawageuza kulia na kushoto. Na mbwa wao amenyoosha
miguu yake ya mbele kizingitini. Kama unge watokea hapana shaka ungeli geuka
kuwakimbia, kwa khofu.
Na kwa namna hii tuliwainua usingizini wapate
kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema:
Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi anajua zaidi
muda mlio kaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha
zenu ende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa akuleteeni
cha kukila. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala
asikutajeni kabisa kwa yeyote.Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao; na hapo hamtafanikiwa kabisa!
Na namna hivi tuliwa juulisha kwa watu wapate kujua ya
kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipo
kuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao walisema:
Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema walio shinda
katika shauri yao: Bila ya shaka tutawajengea msikiti
juu yao.
Watasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na
wanasema: Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.
Wanavurumisha ovyo. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa
nane wao ni mbwa wao. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye jua sawa sawa hisabu yao. Hawawajui ila wachache tu.
Basi usibishane juu yao ila kwa mabishano ya juu juu
tu hivi. Wala usiulize khabari zao kwa yeyote yule.
Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na
wakazidisha tisa.Sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi muda walio kaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona kulioje na kusikia
kwake! Hawana mlinzi isipo kuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu
yake.
>>>Cont... in English
Or have you thought that the companions of the cave and the inscription were, among Our signs, a wonder?[Mention]
when the youths retreated to the cave and said, "Our Lord, grant us
from Yourself mercy and prepare for us from our affair right guidance." So We cast [a cover of sleep] over their ears within the cave for a number of years. Then
We awakened them that We might show which of the two factions was most
precise in calculating what [extent] they had remained in time.
It
is We who relate to you, [O Muhammad], their story in truth. Indeed,
they were youths who believed in their Lord, and We increased them in
guidance. And
We made firm their hearts when they stood up and said, "Our Lord is the
Lord of the heavens and the earth. Never will we invoke besides Him any
deity. We would have certainly spoken, then, an excessive
transgression.
These,
our people, have taken besides Him deities. Why do they not bring for
[worship of] them a clear authority? And who is more unjust than one who
invents about Allah a lie?" [The
youths said to one another], "And when you have withdrawn from them and
that which they worship other than Allah , retreat to the cave. Your
Lord will spread out for you of His mercy and will prepare for you from
your affair facility."
And
[had you been present], you would see the sun when it rose, inclining
away from their cave on the right, and when it set, passing away from
them on the left, while they were [laying] within an open space thereof.
That was from the signs of Allah . He whom Allah guides is the
[rightly] guided, but he whom He leaves astray - never will you find for
him a protecting guide. And
you would think them awake, while they were asleep. And We turned them
to the right and to the left, while their dog stretched his forelegs at
the entrance. If you had looked at them, you would have turned from them
in flight and been filled by them with terror.
And
similarly, We awakened them that they might question one another. Said a
speaker from among them, "How long have you remained [here]?" They
said, "We have remained a day or part of a day." They said, "Your Lord
is most knowing of how long you remained. So send one of you with this
silver coin of yours to the city and let him look to which is the best
of food and bring you provision from it and let him be cautious. And let
no one be aware of you. Indeed,
if they come to know of you, they will stone you or return you to their
religion. And never would you succeed, then - ever."
And
similarly, We caused them to be found that they [who found them] would
know that the promise of Allah is truth and that of the Hour there is no
doubt. [That was] when they disputed among themselves about their
affair and [then] said, "Construct over them a structure. Their Lord is
most knowing about them." Said those who prevailed in the matter, "We
will surely take [for ourselves] over them a masjid."
They
will say there were three, the fourth of them being their dog; and they
will say there were five, the sixth of them being their dog - guessing
at the unseen; and they will say there were seven, and the eighth of
them was their dog. Say, [O Muhammad], "My Lord is most knowing of their
number. None knows them except a few. So do not argue about them except
with an obvious argument and do not inquire about them among [the
speculators] from anyone."
And they remained in their cave for three hundred years and exceeded by nine.
Say,
" Allah is most knowing of how long they remained. He has [knowledge
of] the unseen [aspects] of the heavens and the earth. How Seeing is He
and how Hearing! They have not besides Him any protector, and He shares
not His legislation with anyone." (Qur'an 18:9-22,25-26)
Jumaa Mubarak Everyone. Don't forget to squeeze in some ayas from Suratul Al-Kahf.
No comments:
Post a Comment