Translate

Wednesday, November 21, 2012

Saidia Jamii - Mdhamini Mtoto


BISMILLAHI RAHMANI RAHIM
TAASISI YA MIKAKATI YA MAENDELEO YA JAMII
“MIKAKATI”
S.L.P 2013 ARUSHA. TEL:+255 784 848 483/ + 255 715 015 000 Email: secgeneral@mikakatitanzania.org Website: www.mikakatitanzania.org


ASSALAAM ALEYKUM,
YAH: MAFUNZO YA VETA


Taasisi ya “Mikakati” imeonelea ni vema ikatumia nafasi yake kusaidia kusomeshwa kwa vijana wa Kiislamu waliomaliza Elimu ya msingi, mafunzo ya VETA.

Mnamo mwezi OKTOBA 2012, “MIKAKATI” ilichukua fomu na kupeleka vijana WATANO (5) VETA -Arusha kwenye usaili na ifikapo tarehe 15/12/2012 tutapokea majibu.

Napenda kuchukua fursa hii kukuomba wewe binafsi na waislamu wote walio na uwezo, kuchukua jukumu la kuwalipia ada vijana watakaobahatika kuchaguliwa. Pesa zinazohitajika kwa mwaka ni Tshs. 260,000 KWA KILA KIJANA MMOJA. Hii inajumuisha Ada, Malazi na Chakula.

HIVYO, TUNAKUOMBA WEWE BINAFSI UJITOLEE KUMLIPIA ANGALAU KIJANA MMOJA KATIKA WATAKAOCHAGULIWA ; NA KWAKWELI UTUHAKIKISHIE KUJITOLEA KWAKO KABLA YA TAREHE 30.11.2012. NI TSHS. 260,000 TU KWA MWAKA MZIMA!!!

Kumbuka kuwa katika vitu vitakavyomsaidia Muislamu akifa ni pamoja na Elimu yenye manufaa aloitoa kwa jamii. Basi kunjua mkono wako kuwezesha elimu hii yenye manufaa kuwafikia hawa vijana.

QUR’AN: “Na mnapoazimia jambo,basi mtegemeeni ALLAH-SW”

UFAFANUZI: Azimieni mambo ya kheri,tekelezeni wajibu wenu kwa juhudi na uaminifu wa hali ya juu, kisha mwachieni ALLAH-SW kuleta mafanikio.

IMETAYARISHWA NA:
RAMADHANI I. MAABADI,

…………………………………
KATIBU,
KAMATI YA ELIMU NA DA’AWA.
“MIKAKATI “,
ARUSHA.
03/11/2012

0653-724017
0754-724017

No comments:

Post a Comment