Translate

Monday, May 11, 2020

Hadithi ya Leo - Geti la Ar-Raiyan (Gate of Ar-Raiyan)



Imehadithiwa na Sahl:

Mtume (ﷺ) alisema, "Kuna geti Akhera linaloitwa Ar-Raiyan, na wote wanaofunga wataingia kupitia geti hilo Siku Ya Kiyama, hamna wengine bali yao wataingia kupitia hapo. Itaulizwa,  'Wako wapi wale waliokuwa wakifunga?'
Watanyanyuka, na hakuna zaidi yao wataingia kupitia hapo.
Baada yao, geti litafungwa na hakuna mwingine atakayeweza kuingia kupitia geti hilo."

Narrated Sahl:

The Prophet (ﷺ) said, "There is a gate in Paradise called Ar-Raiyan, and those who observe fasts will enter through it on the
Day of Resurrection and none except them will enter through it. It will be said, 'Where are those who used to observe fasts?'
They will get up, and none except them will enter through it.
After their entry the gate will be closed and nobody will enter through it."
(Bukhari 1896)

Friday, May 8, 2020

Aya ya Leo - Hekima (Wisdom)


Yeye humpa hekima amtakaye; na aliye pewa hekima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hakuna atakayekumbuka isipokuwa wale wenye uelewa.

He gives wisdom to whom He wills, and whoever has been given wisdom has certainly been given much good. And none will remember except those of understanding.
(Qur'an 2:269)
Jumaa Kareem! 
Allah atukubalie funga na dua zetu. 

Wednesday, May 6, 2020

SHEIKH SULEIMAN KILEMILE AFARIKI DUNIA

Inna lillahi Waina Illahi Rajiun!
Mwenyezi Mungu ampe kauli dhabit, amsamehe madhambi yake na Amlaze mahali pema peponi.

Habari nilizopata ni sheikh amefariki kutokana na matatizo ya kisukari. 
Sasa kuna video ya mazishi yake iliyokua ikizunguka ikionyesha umati wa watu uliokusanyika kumzika sheikh wetu. 
Alhamdullilah amepumzishwa salama.

 Lakini jamani ndugu zangu ngoja tuongee leo kuhusu mazishi ya sheikh wetu mpendwa. Tumeambiwa kuna ugonjwa wa Corona na Serikali imekataza mikunsanyiko ya watu, sawa wengine walikuwa wamejikinga na barakoa na gloves, lakini lile jeneza watu wangapi wamelishika? Kuna mtu pale hakushika barakoa lake kulirekebisha kabla ya kuosha mikono yake au kutumia kitakasa mkono? Maana sio kama watu walikuwa kwenye kiyoyozi, lazima mtu alifuta jasho, au alitengeneza barakoa lake likae vizuri, yote hii ni kushika uso. Pia ule ukaribu wa watu haukuwa mita 2 au 3, na pale kulikuwa na wazee wetu na ma sheikh wetu ambao ni watu wazima, wengine wana matatizo ya pressure, kisukari, moyo nakadhalika.
Mwenyezi Mungu atustiri na siombei mabaya lakini naona kama majibu tutayapata baada ya siku 14.
Ndugu zangu najua ni vigumu lakini tujitahidini kufuata maagizo tunayo pewa na serikali. Sasa kwa vile yameshatokea, kama ulikuwepo, kajitenge kwa siku 14 ukitunza afya yako ili usiambukize familia yako.
Allah Atustiri!

Monday, May 4, 2020

Hadithi ya Leo - Jira Nyeusi/Habar Soda (Black Seed)


Imehadithiwa na Abu Huraira"
Nilisikia Mtume wa Allah (ﷺ) akisema, "Kuna tiba kwenye jira nyeuse(Habar Soda) kwa magonjwa yote isipokuwa kifo."

 Narrated Abu Huraira:
I heard Allah's Messenger (ﷺ) saying, "There is healing in black cumin for all diseases except death." (al-Bukhari 5688)

Friday, May 1, 2020

Aya ya Leo -Rekodi (The Register)

 Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha.

Indeed, it is We who bring the dead to life and record what they have put forth and what they left behind, and all things We have enumerated in a clear register. (Qur'an 36:12)
Jumaa Mubarak!

 

Rostam Aziz Donates COVID-19 Diagnostic Test to Zanzibar

 He also donated 9,000 hand sanitizers and 90,000 masks to the health care workers and the front-liners.
Mashaallah!
Mzee Aziz Katishaaaaa!
Kanunua kifaa cha kuweza kupima coronavirus Zanzibar na kupata majbu ndani ya masaa matatu na nusu. Sasa hivi Zanzibar hamna tena mambo ya kutuma tests Dar alafu usubirie majibu baada ya siku kadhaa.
Jamani haya ni zaidi ya mahaba.
Atasaidia watanzania wengi sana na kuokoa wengi, na kila mtu kwakweli ajitolea jinsi awezavyo kuwasaidia wananchi.
Mwenyezi Mungu amkubalie dua zake zote, amfungulie milango yake yote ya Kheri hapa duniani na Akhera. 
BE INSPIRED!