Translate

Wednesday, May 6, 2020

SHEIKH SULEIMAN KILEMILE AFARIKI DUNIA

Inna lillahi Waina Illahi Rajiun!
Mwenyezi Mungu ampe kauli dhabit, amsamehe madhambi yake na Amlaze mahali pema peponi.

Habari nilizopata ni sheikh amefariki kutokana na matatizo ya kisukari. 
Sasa kuna video ya mazishi yake iliyokua ikizunguka ikionyesha umati wa watu uliokusanyika kumzika sheikh wetu. 
Alhamdullilah amepumzishwa salama.

 Lakini jamani ndugu zangu ngoja tuongee leo kuhusu mazishi ya sheikh wetu mpendwa. Tumeambiwa kuna ugonjwa wa Corona na Serikali imekataza mikunsanyiko ya watu, sawa wengine walikuwa wamejikinga na barakoa na gloves, lakini lile jeneza watu wangapi wamelishika? Kuna mtu pale hakushika barakoa lake kulirekebisha kabla ya kuosha mikono yake au kutumia kitakasa mkono? Maana sio kama watu walikuwa kwenye kiyoyozi, lazima mtu alifuta jasho, au alitengeneza barakoa lake likae vizuri, yote hii ni kushika uso. Pia ule ukaribu wa watu haukuwa mita 2 au 3, na pale kulikuwa na wazee wetu na ma sheikh wetu ambao ni watu wazima, wengine wana matatizo ya pressure, kisukari, moyo nakadhalika.
Mwenyezi Mungu atustiri na siombei mabaya lakini naona kama majibu tutayapata baada ya siku 14.
Ndugu zangu najua ni vigumu lakini tujitahidini kufuata maagizo tunayo pewa na serikali. Sasa kwa vile yameshatokea, kama ulikuwepo, kajitenge kwa siku 14 ukitunza afya yako ili usiambukize familia yako.
Allah Atustiri!

No comments:

Post a Comment