Translate

Friday, July 26, 2013

FUTARIIII!!!!!!!!!

Jamani ndo tuna karibia kumaliza fungo kumi la pili. Vipi mmnaendelaje? Naona kwenye mitandao tu watu wanarusha mafutari ya kufa mtu. Tukumbukeni tu kutokufanya kufuru, maana unajikuta wakati umefunga unatamani kila kitu, futari tunabugia, matokea yake? choo kinakuwa cha tabu. Tukazane kufuata suna ya Mtume Muhamad (Rehema na baraka ziwe juu yake), yeye alikuwa anaanza na Maji na tende.

Maji yanaanza kuendesha digestive system yako.
Na tende zimejaa virutubisho kibao, za kukupa nguvu na fiber ya kukusaidia kupata choo vizuri.

Basi tujitahidini kuswali Magharibi kabla ya kuanza hizo main course za futari, maana ile inama inuka pia zoezi, lakini ni zoezi zuri kwa vile unamshukuru Mtawala wa ulimwengu kwa kukuwezesha kupata hiyo futari.

Nawaacha na picha za futari la nguvu kutoka kwa mdau wangu wa UK. Enjoy!

Mmh! Jamani Tambi ni tamu asikudanganye mtu.
Mambo ya Biriani la kondoo.Toba!
Samaki wa kukaanga.
na kumalizia na Chai ya maziwa, sponge cake na bajia.
Jamani Jamani! Natamani Chai na Keki sasa.

Ijuma Njema wadau!

No comments:

Post a Comment