Translate

Friday, January 18, 2019

Aya za Leo - Watu Wema (The Righteous)

  Hakika tumemuumba Mwanaadamu katika taabu.
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
Kwani hatukumpa macho mawili?
Na ulimi, na midomo miwili?
Na tukambainishia zote njia mbili (iliyo Njema na Mbaya)?
Lakini hakujituma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
Na nini kitakachokujulisha ni nini njia ya vikwazo vya milimani?  
Kumkomboa mtumwa;
Au kumlisha siku ya njaa
Yatima aliye jamaa (Na asiyekua jamaa),
Au masikini aliye vumbini.
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

We have certainly created man into hardship.
Does he think that never will anyone overcome him?
He says, "I have spent wealth in abundance."
Does he think that no one has seen him?
Have We not made for him two eyes?
And a tongue and two lips?
And have shown him the two ways?
But he has not broken through the difficult pass.
And what can make you know what is [breaking through] the difficult pass?
It is the freeing of a slave
Or feeding on a day of severe hunger
An orphan of near relationship
Or a needy person in misery
And then being among those who believed and advised one another to patience and advised one another to compassion.
Those are the companions of the right.
(Qur'an 90:4-18)

Ijumaa Njema!

No comments:

Post a Comment