Translate

Monday, December 24, 2012

Msomi wa Leo - Sheikh Hamza Yusuf (1958 - Sasa)

Sheikh Hamza Yusuf ni Mzaliwa wa Jimbo la Washington, Marekani. Alisoma dini kwa muda wa miaka Kumi, UAE, Saudi Arabia, Afrika Kaskazini na Afrika Magharibi. Alisomea chini ya wasomi wakuu wa hizo nchi. Ana Shahada ya Nursing kutoka Chuo cha Imperial Valley na Shahada ya Masomo ya Dini kutoka chuo kikuu cha San Jose. Sheikh ni moja wa waanzilishi wa chuo cha Dini cha Zaytuna kilichopo mji wa Berkeley Jimbo la California. Ni mshauri wa chuo kikuu cha Stanford kwenye idara ya masomo ya kiislamu, na pia chuo cha Berkeley's Graduate Theological Union.

Sheikh ameandika vitabu vingi vya dini, na pia ametoa ushauri kwa wakuu wengi wa nchi. Anaishi jimbo la California na mke wake na watoto wao watano wa kiume. Msikilize mwenyewe Sheikh anavyo kuelezea umuhimu wa kuondosha umaskini na kuinua jamii.

Mwenyezi Mungu amzidishie Kheri ya Dunia na Akhera.

No comments:

Post a Comment