Translate

Sunday, September 16, 2012

Msomi wa Leo - Sheikh Hassan Cisse (1945–2008)

Mzaliwa wa Senegal, na ni Imaam wa International Muslim Community ya Medina Baye, Senegal. Sheikh ni Hafiz wa Qurani, alifundhishwa dini na babu na baba yake, na ana Shahada cha chuo kikuu cha Ain Shams Egypt, kwenye fasihi ya Kiarabu na dini. Ana Masters ya Kiingereza kutoka University of London, na alianza PHD yake marekani, lakini ilibidi aikatishe baba yake alivyofariki, arudi ku ongoza Medina Baye. Alikuwa anaongea, kiarabu, kifaransa, Kizungu, Kihausa na KiWolof. Sheikh, aliandika vitabu vingi vya dini, na alikuwa anafanya kazi nyingi za kuinua jamii ya waislamu Africa Magharibi. Alifariki Dunia mwaka 2008,  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Msikilize mwenyewe Sheikh anakwambia umuhimu wa Maulid na kumpenda Mtume Mohammed(S.A.W). The video is in English.




No comments:

Post a Comment