Translate

Sunday, July 22, 2012

FUTARIIII!!!!!

Uji wa pili pili manga, kunde za nazi, maharage ya sukari, tambi, chapati, kalmati, mihogo, viazi vitamu, mzuzu wa nazi. Uwii jamani kuna muislamu asiyeiwaza futari toka akiamka japo muda wake haujafika? Jamani na mimi nipo kwenye huo mkumbo. Nikiangalia ramadhani hii watu wa Europe wanaanza kufungua kuanzia saa tatu usiku mpaka nne kasoro,  mmh! poleni maanake huo ni mtihani.

Leo nataka kuongelea maswala ya futari.Tuna tatizo sisi waislamu ya kubugia time ya futari mpaka unashindwa kufanya lingine lolote. Matokeo yake unabaki hupati choo vizuri, unanenepa mwezi wa ramadhani, which defeats the purpose of fasting. Tukumbukeni kula balanced diet na kula in moderation.

Basi ngoja niwaacheni na vi tips vya kuwapikia familia zenu time hizi za ramadhan.
Anza na matunda, hii itawa keep familia busy kidogo wakati wewe unamalizia futari.
Pia utawapa familia yako nutrition na fiber wanazohitaji.
Tafuta matunda yaliyo kwenye msimu, ndio matamu zaidi. 


Matunda kama Tende yanapatikana mwaka mzima, na hata mtume Mohammed(S.A.W) alikuwa anapenda kuanzia nayo. 
Wakimaliza kula matunda, suna tu sio kushiba sasa, waka swali magharibi :) 


Mzuzu wa kukaanga is usually a hit in my household, ukichanganya na mbuzi kidogo.

Baada ya matunda(Dessert kwanza) dish kama hili baada ya salaa magharibi. Ni vizuri zaidi upate mboga ya majani kidogo au lettuce, lakini sisi kwetu mchicha utaula mwenyewe, watu wanataka vya sukari tu na starch nyingi.

Nawaacha na futari spread kutoka msikitini USA, wenzetu watu wa nchi zingine kama USA, UK na Uarabuni, huwa wanafuturisha kwenye misikiti yao. Na sisi pia tujitahidi kupeleka hata maji na tende msikitini jamani watu waweze kufungua vinywa.

No comments:

Post a Comment