Arusha.Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 59
kujeruhiwa akiwamo Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini
Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Montecillo Padilla jana asubuhi baada ya
mtu asiyejulikana kurusha bomu wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Jengo
la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Arusha.
Miongoni mwa majeruhi, imeelezwa kuwa wanne ni mahututi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas amelielezea kuwa tukio hilo kuwa ni la kigaidi hasa kutokana na
kumlenga Balozi wa Papa nchini na kwamba mtu mmoja anashikiliwa
akihusishwa nalo.
Wataalamu wa mabomu wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) wanachunguza aina ya bomu lililotupwa lakini uchunguzi wa awali
unaonyesha lilikuwa limetengenezwa kienyeji.Bofya hapa kwa habari zaidi kutoka gazeti la Mwananchi....
Ina lillahi wa Ina Illahi Rajiun. Kwa Mwenyezi Mungu ndio tunapotoka na ndio marejeo. Jamani hizi habari zinasikitisha sana, inakuwaje Binadamu hatuziheshimu tena sehemu za ibada, absolutely terrible. Nawaombea familia za marehemu na walioumia.
Update!
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alisema watu tisa wamekamatwa hadi sasa.
Aliwataja baadhi yao kuwa ni Victor Ambrose na wengine aliowataja kwa jina mojamoja ni Joseph na David. Alisema wengine ni raia watatu wa Saudi Arabia, ambao walikuwa na wenyeji wao wawili na Watanzania wengine watatu. Wa Saudi waziri mkuu alisema bungeni wataachiwa. Soma Habari Zaidi Mwananchi
No comments:
Post a Comment