Translate

Friday, January 11, 2019

Surah ya Leo - Al Waaqi'ah - Isiyozuilika (The Inevitable)

Je wewe ni watu wa mkono wa kulia? Umejitayarishaje uwe angalau ata wale wa mwisho mwisho kwenye kundi la watu wenye kheri?

Qu'ran Chapter 56.
Msomi Sheikh Yusuf Simbano.
Ijumaa Njema Wadau!

Friday, January 4, 2019

Aya ya Leo - Maisha ya Dunia(Worldy Life)



Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri. 

The example of [this] worldly life is but like rain which We have sent down from the sky that the plants of the earth absorb - [those] from which men and livestock eat - until, when the earth has taken on its adornment and is beautified and its people suppose that they have capability over it, there comes to it Our command by night or by day, and We make it as a harvest, as if it had not flourished yesterday. Thus do We explain in detail the signs for a people who give thought.
 (Qur'an 10:24)
Ijumaa Njema!

Aya ya Leo - Alama (Signs)

  Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.

Indeed, in the creation of the heavens and earth, and the alternation of the night and the day, and the [great] ships which sail through the sea with that which benefits people, and what Allah has sent down from the heavens of rain, giving life thereby to the earth after its lifelessness and dispersing therein every [kind of] moving creature, and [His] directing of the winds and the clouds controlled between the heaven and the earth are signs for a people who use reason.
(Qur'an 2:164) 
Jumaa Mubarak!

Friday, December 28, 2018

Aya ya Leo - Mungu Mmoja(One God)



Na Mungu wenu ni Mungu mmoja tu, hapana mungu ila Yeye. Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

And your god is one God. There is no deity [worthy of worship] except Him, the Entirely Merciful, the Especially Merciful. (Qur'an 2:163)

Jumaa Mubarak!

Friday, December 21, 2018

Aya ya Leo - Imani ya Mungu Mmoja (Monotheism)


Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Ingekuwa hivyo basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.

Allah has not taken any son, nor has there ever been with Him any deity. [If there had been], then each deity would have taken what it created, and some of them would have sought to overcome others. Exalted is Allah above what they describe [concerning Him]. (Qur'an 23:91)
Jumaa Mubarak!

Friday, October 19, 2018

Aya za Leo - Adabu (Manners)


Mtume alikunja kipaji na akageuka
Kwa sababu alimjia kipofu [akamkatiza]
Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
Au ata kumbushwa, na ukumbusho utamfaa?
Na yule ajionaye hana haja,
Wewe ndio unamshughulikia?
Na si juu yako kama hata takasika.
Lakini yule aliye kujia kwa juhudi
Akiwa na uoga,
 Ndio wewe unampuuza?
Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
Basi anaye penda akumbuke.
Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa.


The Prophet frowned and turned away
Because there came to him the blind man, [interrupting].
But what would make you perceive, [O Muhammad], that perhaps he might be purified
Or be reminded and the remembrance would benefit him?
As for he who thinks himself without need,
To him you give attention.
And not upon you [is any blame] if he will not be purified.
But as for he who came to you striving [for knowledge]
While he fears [ Allah ],
From him you are distracted.
No! Indeed, these verses are a reminder;
So whoever wills may remember it.
[It is recorded] in honored sheets. (Qur'an 80:1-13)

Jumaa Mubarak!