Nime fowardiwa hii video ya huyu binti, simjui wala hanijui, lakini nimesikitishwa mno. Jamani, mjini hakuendiki, na hata ukikaa nyumbani hali ni hivi. Inatia Huruma mno, yaani kwanza kujenga nyumba bongo it takes years, kwasababu wengi wetu hatuna mambo ya kuchukua mikopo.Sasa mtu umechakarika mpaka umejenga nyumba yako, na kuitengeneza vizuri ndani na finishing na furniture nzuri. Alafu hiyo sehemu mliouziwa kiwanja mjenge amabayo imekuwa cleared na serikali kwa ujenzi, hauna miundombinu ya kuku support wewe mwenye nyumba.
Yaani jamani hivi serikali mnawezaje kuwacha viwanja viuzwe sehemu ambayo bado hamjaiweka sawa ili watu waweze kujenga na wasipata hizi hasara. Angalia huyo mdada, tiles zake, furniture zake, sijui washing machine na vitu vingine vingi familia yake imejipiga ili wawe na maisha bora, leo poof imetoweka. Nani atamsadia kununua vitu upya? Na inavyo onekana wala hakai bondeni.
Mi naona tatizo ni hivi, Idara ya Ardhi ya dar hawana proper procedure ya ku approve ujenzi. Kama sehemu haina miundo mbinu ya kutosha, msiwe mna approve ujenzi wakati mabomba ya maji machafu na masafi hamna, wala njia za maji za mvua za size ya kutosha hamna. Kama bado mnataka ku approve na serikali haina hiyo hela ya kutengeneza hiyo sehemu(Which they never do), mtu akitaka kujenga magorofa ya nyumba nyingi, alizamishwe kuchangia kwenye miundo mbinu ya ku support huo ujenzi. Kwa mfano, ajenge njia nzuri iliyo nyanyuka kwa watu kutembea, aweke mifereji ya ku channel maji ya mvua tena zifunikwe sio mambo ya watu na magari kudumbukia humo, kama pipe ya city ni ndogo, achangie kulipia kubadilisha pipe za maji machafu na masafi za mji ziwe kubwa kumsupport yeye na wakazi wake. Yaani kuwe na regulations na standards za size ya mabomba, mifereji na mifereji yote ifunikwe, tumechoka kusikia watu wamekufa kwa kuanguka kwenye mifereji.
Pole kwa hii familia, Kwakweli huu ni mtihani mzito, Mwenyezi Mungu yupo na atawa fungulia riziki Inshallah. Qur'an inatuambia, kwenye uzito wepesi unakuja.