Translate

Thursday, December 12, 2019

Ali Mufuruki(1958 – 2019)

Inna lillahi waina illahi rajiun. May Allah grant him Jannah, a true visionary who will be greatly missed.

Monday, September 23, 2019

Hadithi ya Leo - Adhabu ya Kujiua (The Punishment for Suicide)



Narrated  Abu Huraira:

The Prophet (ﷺ) said, "Whoever purposely throws himself from a mountain and kills himself, will be in the (Hell) Fire falling down into it and abiding therein perpetually forever; and whoever drinks poison and kills himself with it, he will be carrying his poison in his hand and drinking it in the (Hell) Fire wherein he will abide eternally forever; and whoever kills himself with an iron weapon, will be carrying that weapon in his hand and stabbing his `Abdomen with it in the (Hell) Fire wherein he will abide eternally forever." ( Sahih Al-Bukhari 5778)

Friday, September 20, 2019

Aya ya Leo - Malaika wa Motoni (Angels of Hell)



Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.

And We have not made the keepers of the Fire except angels. And We have not made their number except as a trial for those who disbelieve - that those who were given the Scripture will be convinced and those who have believed will increase in faith and those who were given the Scripture and the believers will not doubt and that those in whose hearts is hypocrisy and the disbelievers will say, "What does Allah intend by this as an example?" Thus does Allah leave astray whom He wills and guides whom He wills. And none knows the soldiers of your Lord except Him. And mention of the Fire is not but a reminder to humanity.(Qur'an 74:31)
Jumaa Mubarak!

Friday, September 13, 2019

Aya za Leo - Malaika wanaochukua roho( The Angels who draw the soul)

When Allah Swears on his creation. Which one are you?

Naapa kwa Malaika wanao vuta kwa nguvu roho za watu wabaya. Na kwa wanao vuta kwa utaratibu roho za walio neemeshwa.

I swear by the angels who violently pull out the souls of the wicked. And by those who gently draw out the souls of the blessed. (Qur'an 79:1-2)
Jumaa Mubarak!

Sunday, September 8, 2019

Hadithi ya Leo - Kufunga Ashuraa (Fasting on Ashuraa)


Imehadithiwa na Aisha:

Kabila la Quraish, walikuwa wakifunga siku ya Ashura kabla ya uislamu. Mtume wa Allah akawaamrisha Waislamu wafunge hiyo siku mpaka Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani ulivyo amrishwa. Ndipo Mtume wa Allah akasema, " Yule anayetaka kufunga siku ya Ashura afunge, na yule asiyetaka kufunga asifunge.


Narrated `Aisha:

(The tribe of) Quraish used to fast on the day of Ashura' in the Pre-Islamic period, and then Allah's Apostle ordered (Muslims) to fast on it till the fasting in the month of Ramadan was prescribed; whereupon the Prophet (ﷺ) said, "He who wants to fast (on 'Ashura') may fast, and he who does not want to fast may not fast." (Bukhari 1893)

Happy Fasting for those fasting on the 9th-11th of Muharam (8th-10th of September).

Friday, September 6, 2019

Aya ya Leo - Zawadi (Reward)


Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kati yake. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo.

Indeed, Allah will admit those who believe and do righteous deeds to gardens beneath which rivers flow. Indeed, Allah does what He intends.(Qur'an 22:14)
Jumaa Mubarak!

Tuesday, September 3, 2019

Hadithi ya Leo - Adhan (Call to Prayer)


Imehadithiwa na Ibn Umar:

Waislamu walivyo wasili Madina, walikuwa wakikusanyika kusali kwa kukadiria muda wake. Enzi hizo, Adhan ya kuwaita watu kuswali ilikuwa haipo. Watu waka pendekeza itumike kengele kama wakristo, na wengine wakapendekeza tarumbeta kama inayotumika na wayahudi, lakini Umar ndio alikuwa wa kwanza kupendekeza itumike sauti ya mtu kuwaita watu kwenye sala. Kwahiyo Mtume wa Allah, akamuamrisha Bilal apande juu na kutangaza Adhan kuita watu kuswali.

Narrated Ibn `Umar:

When the Muslims arrived at Medina, they used to assemble for the prayer, and used to guess the time for it. During those days, the practice of Adhan for the prayers had not been introduced yet. Once they discussed this problem regarding the call for prayer. Some people suggested the use of a bell like the Christians, others proposed a trumpet like the horn used by the Jews, but `Umar was the first to suggest that a man should call (the people) for the prayer; so Allah's Messenger (ﷺ) ordered Bilal to get up and pronounce the Adhan for prayers. (Bukhari 604)

Saturday, August 31, 2019

Happy New Islamic Year!


Heri ya Mwaka Mpya!
Mwenyezi Mungu atujaalie uwe mwaka wa Heri na Baraka zake! 

Friday, August 16, 2019

Aya ya Leo - Allah


Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

Whatever is in the heavens and whatever is on the earth is exalting Allah, the Sovereign, the Pure, the Exalted in Might, the Wise. (Qur'an 62:1)

Sunday, August 11, 2019

Wednesday, August 7, 2019

The luck of the draw - The Road to Hajj - India | Featured Documentary

If your lucky to be going this year, please look out for the old folks and lend a helping hand when you can.

Alhamdullilah! Tanzania tuna bahati sana na msaada tunaopata wa kwenda kuhiji.

Saturday, August 3, 2019

UMRAH MECCA | MEDINA

Okay if this doesn't make you smile, make some dua, because it is just the sweetest video.
The little girl stole my heart, you can tell she is Daddy's little girl.

Beautiful Family! Mashaallah!
May Allah Bless us all to be able to visit Makkah and Madinna Insh'aa'llah.

Friday, August 2, 2019

Aya ya Leo - Mbinguni (The Heavens)



Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.
So He ordained them seven heavens in two periods, and revealed in every heaven its affair; and We adorned the lower heaven with brilliant stars and (made it) to guard; that is the decree of the Mighty, the Knowing. (Qur'an 41:12)
Jumaa Mubarak!

Friday, July 26, 2019

Aya ya Leo - Nafsi yako (Your Soul)

Take care of your soul.

 Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.

Whoever does good, its for his own soul, and whoever does evil, it is against it; and your Lord is not in the least unjust to the servants. (Qur'an 41:46)
Jumaa Mubarak!

Friday, July 19, 2019

Aya ya Leo - Kusamehe (To Forgive)



Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha, basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.
And the recompense of evil is punishement like it, but whoever forgives and amends, he shall have his reward from Allah, surely He does not love the unjust. (Qur'an 42:40)

Friday, July 12, 2019

Aya ya Leo - Malaika (Angels)


Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!

And they make the angels-- them who are the servants of the Beneficent Allah, female(divinities). What! did they witness their creation? Their evidence shall be written down and they shall be questioned. (Qur'an 43:19)
Jumaa Mubarak!

Friday, July 5, 2019

Aya ya Leo - Matamanio (Desire)

Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.

Whoever desires the harvest of the Hereafter - We increase for him in his harvest. And whoever desires the harvest of this world - We give him thereof, but there is not for him in the Hereafter any share.
(Qur'an 42:20)

Friday, June 28, 2019

Aya ya Leo - Habari (The Message)


Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo tunamuongoza tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoza kwenye Njia Iliyo Nyooka.

And thus We have revealed to you an inspiration of Our command. You did not know what is the Book or [what is] faith, but We have made it a light by which We guide whom We will of Our servants. And indeed, [O Muhammad], you guide to a straight path (Qur'an 42:52)
Jumaa Mubarak Wandugu!


Aya za Leo - Nijengee Mnara - Firauni (Build for me a tower..-Pharaoh )

.. build for me a tower that I may attain the means of access to the heavens, then reach the God of Moses..-Pharaoh
Na Firauni akasema:" Ewe Haman! nijengee mnara ili niweze kupata njia." "Njia za mbinguni ili nikamuone Mungu wa Musa; na kwa yakini ninamjua kuwa ni muongo tu (huyo Musa, lakini nataka kukuonyesheni na nyinyi)." Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake na akazuiliwa njia(ya haki); lakini vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu.

And Pharaoh said: O Haman! build for me a tower that I may attain the means of access. The means of access to the heavens, then reach the god of Musa, and I surely think him to be a liar. And thus the evil of his deed was made fairseeming to Pharaoh, and he was turned away from the way; and the struggle of Pharaoh was not (to end) in aught but destruction. (Qur'an 40: 36-37)
Ijumaa Njema!

Friday, June 21, 2019

Aya ya Leo - Dua (Prayer)


Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.

My Lord! Forgive me and my parents and him who enters my house believing, and the believing men and the believing women; and do not increase the unjust in aught but destruction! (Qur'an 71:28)
Jumaa Mubarak!

Tuesday, June 18, 2019

Monday, June 10, 2019

Hadithi ya Leo - Mapovu ya Bahari (Sea foam)


Imehadithiwa na Abu Huraira:

Mtume wa Allah alisema, Yoyote anayesema,
'Subhan Allah wa bihamdihi,' 
Mara mia moja kwa siku, atasamehewa dhambi zake zote atakama zilikuwa nyingi kama mapovu ya bahari. 

Narrated Abu Huraira:

Allah's Messenger (ﷺ) said, "Whoever says,
'Subhan Allah wa bihamdihi,' 
one hundred times a day, will be forgiven all his sins even if they were as much as the foam of the sea. (Bukhari 6405)

Friday, June 7, 2019

Aya ya Leo - Uumbaji (Creation)


Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake.

Allah begins creation; then He will repeat it; then to Him you will be returned.
(Qur'an 30:11) 
(Ijumaa Njema Wadau)

Monday, June 3, 2019

How to Perform Eid Prayer ( in English )


WHAT IS THE AUTHENTIC METHOD FOR PERFORMING THE EID PRAYER? - DR ZAKIR NAIK


Hadithi ya Leo - Dhawabu Mia (One Hundred Good Deeds)


Imehadithiwa na Abu Huraira:

Mtume wa Allah alisema, "Yoyote anayesema: 
" La ilaha illal-lah wahdahu la sharika lahu, lahu-l-mulk wa lahul- hamd wa huwa 'ala kulli shai'in qadir 
(Hakuna Mungu ila Allah pekee, bila Mwenzie. Yeye ndio Mmiliki, na Mwenye sifa zote, na Mwenye Nguvu juu ya kila kitu)," 
mara mia moja, atapata dhawabu sawa na mtu anayeachia watumwa kumi, na dhawabu mia moja itaandikwa kwenye hesabu zake, na dhambi mia zitafutwa kwenye hesabu zake, na itakuwa ngao yake kutoka kwa shetani siku hiyo mpaka usiku wake, na hamna atakayeweza kumzidi zaidi ya yule anayetenda mema zaidi yake.


 Narrated Abu Huraira:
Allah's Messenger (ﷺ) said," Whoever says: 
"La ilaha illal-lah wahdahu la sharika lahu, lahu-l-mulk wa lahul- hamd wa huwa 'ala kulli shai'in qadir 
(There is no god but Allah, alone, without partner. His is the sovereignty, and His the praise, and He has power over everything)," 
one hundred times will get the same reward as given for manumitting ten slaves; and one hundred good deeds will be written in his accounts, and one hundred sins will be deducted from his accounts, and it (his saying) will be a shield for him from Satan on that day till night, and nobody will be able to do a better deed except the one who does more than he." (Bukhari 6403)

Tukumbuke kufanya sunna ya kwenda kuutafuta Mwezi wa Iddi.

THE MESSAGE - THE STORY OF ISLAM | ENGLISH - FULL HD

This movie never gets old.

Friday, May 31, 2019

Aya ya Leo - Midnight Sun (Jua la Usiku)

Hata alipo fika matokeo ya jua aliliona linawachomozea watu tusio wawekea pazia la kuwakinga nalo.


Until, when he came to the rising of the sun, he found it rising on a people for whom We had not made against it any shield. (Qur'an 18:90)

Alhamdullillah! Ndo tunamalizia Ramadhani na Ijumaa Yetu ya mwisho.
Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi, apokee dua zetu na atufungulie Milangu yetu ya Kheri hapa Duniani na Akhera.
Ijumaa Njema!

Wednesday, May 29, 2019

Msomi wa Leo - Rajai Ayoub

Msikilize Mwenyewe akielezea Historia yake.
Mashaallah! Mwenyezi Mungu Amzidishie Kipaji chake, na amfungulie milango yake ya Kheri.

Monday, May 27, 2019

Hadithi ya Leo - Ubinadamu (Humanity)


Imehadithiwa na Abu Musa Al-Ash'ari

Mtume alisema, "Toa chakula kwa wenye njaa, watembelee wagonjwa na muachie
aliyefungwa" (kwa kulipia fidia yake)
Narrated Abu Musa Al-Ash'ari:

The Prophet (ﷺ) said, "Give food to the hungry, pay a visit to the sick and release
(set free) the one in captivity" (by paying his ransom). (
Bukhari 5373)
Happy Monday!

Sunday, May 26, 2019

Farawan family | One year later


LIVE: FAINALI Za Kuhifadhi QURAAN - Diamond Jubilee

Tis the season of Qur'an competitions.
International Qur'an Competition in Tanzania.
I love this, Qur'an competitions everywhere.
Mashaallah! Good luck to all the participants, you are all winners.

Update:
Top 3 winners for the International Qur'an competition, even though it was a tight race are:
1. Zakaria Sheha Ally (16) from Tanzania won $5,000
2. Gaffari Mohammed (14) from England won $4,000
3. Shamsi Mwalimu Said (19) from Tanzania won $3,000

Friday, May 24, 2019

Aya ya Leo - Tafakari (Reflections)

Petra, mji wa zamani Jordan, ambaye nyumba zake zilijengwa ndani ya majabali.

Je! Hawatembei katika ardhi wakaona ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua
ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyo istawisha wao.
Na Mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.

Have they not traveled through the earth and observed how was the end of those before them? They were greater than them in power, and
they plowed the earth and built it up more than they have built it up,
and their messengers came to them with clear evidences. And Allah would not ever have wronged them, but they were wronging themselves. (Qur'an 30:9)
(Jumaa Mubarak!)

Tuesday, May 21, 2019

Hadithi ya Leo - I'tikaf (Kuhamia Msikitini kwa Ajili ya Kumtukuza Allah) - Retiring to a Mosque for the remembrance of Allah



Imehadithiwa na Abu Huraira:

Mtume alikuwaga anafanya I'tikaf(Kuhamia Msikitini kwa Ajili ya Ibada) kila mwaka mwezi wa
Ramadhani kwa siku kumi, na ule mwaka wa kifo chake, alifanya I'tikaf kwa siku ishirini.

Narrated Abu Huraira:

The Prophet (ﷺ) used to perform I`tikaf every year in the month of Ramadan for ten days,
and when it was the year of his death, he stayed in I`tikaf for twenty days.
(Bukhari 2044)

Monday, May 20, 2019

Top 5 winners from the Qur'an competition in Tanzania



5. Sumayyah Juma Abdallah from Tanzania  won 4 million Tshs.
4. Idrissa Ousmane from Niger won 5 Million Tshs.
3. Shamsuddin Hussein Ali from Tanzania won 8.5 million Tshs and a plot in kigamboni.
2. Faruq Karibu Yakubu  from Nigeria won 12 million Tshs.
1. Mouhamed el Moudjtaba Diallo from Senegal won 20 million Tshs and a free ticket to go to Hajj.

All participants received 200 dollars each. 
Mashallaah! Congratulations to the winners and all the participants.
Happy Monday Folks!

Sunday, May 19, 2019

Mashindano ya Qu'ran ya Afrika (Africa Qur'an Competition in Tanzania)


Usipitwe mambo ni moto moto. Lazima Tushinde mwaka huu.
Mashaallah! May Allah bless you all, you are all winners.

Friday, May 17, 2019

Aya ya Leo - Dua ya Nabii Musa (Prophet Moses's Prayer)


(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
Na unifanyie wepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
Ili wapate kuelewa maneno yangu.
Na nipe waziri kutoka kwenye familia yangu,
Harun, ndugu yangu.
Kwake yeye niongeze nguvu zangu.
Na umshirikishe katika kazi yangu.
Ili tukutakase sana.
Na tukukumbuke sana.
Hakika Wewe unatuona.

[Moses] said, "My Lord, expand for me my breast [with assurance]
And ease for me my task
And untie the knot from my tongue
That they may understand my speech.
And appoint for me a minister from my family -
Aaron, my brother.
Increase through him my strength
And let him share my task
That we may exalt You much
And remember You much.
Indeed, You are of us ever Seeing."
(Qur'an 20:25-35)

Jumaa Mubarak!

Tuesday, May 14, 2019

Monday, May 13, 2019

Hadithi ya Leo - Kumlipizia Marehemu Fungo la Ramadhani (Repaying Missed Ramadhan Fasting Days for the deceased)


Imehadithiwa na Aisha:

Mtume wa Allah alisema, "Yeyote aliyefariki na alitakiwa kulipa (Siku ambazo hakufunga mwezi wa Ramadhani) basi ndugu zake wanatakiwa kufunga kwa ajili yake."


Narrated `Aisha:

Allah's Messenger (ﷺ) said, "Whoever died and he ought to have fasted (the missed days of Ramadan) then his guardians must fast on his behalf."
(Bukhari 1952)

Happy Monday and Second Week of Ramadhan!

Sunday, May 12, 2019

Iftar from the Prophet's Mosque (Al Masjid An Anabawi)

Futarii kutoka Msikiti wa Mtume. 
Mashaallah, hakuna mtu kukosa futari hapa.
Don't you just wish you were there right now.
Sema muda ukikaribia tunakuwaga tuna hesabu dakika.

Mwenyezi Mungu Awaongezee wanaojitolea kufuturisha pale walipopungukiwa na azidi kuwashushia baraka zake.
Mnaamka kula daku lakini, maana imejaa baraka tele, usikubali kupitwa nazo.

Saturday, May 11, 2019

Je Unapelelezwa na Simu Yako?

Lets get Educated! 
Jinsi ilivyo rahisi kuhack simu zenu za mkono.
Je! unatabia za ku download apps kwenye simu yako ya mkono mara kwa mara? Basi hii video inakulenga wewe. Facebook wanapelekeshwa kila siku na serizali za wenzetu, kwasababu wanachukua habari nyingi sana kutoka kwenye simu yako zaidi ya wewe unavyodhani.

Hizi app zinaweza ku access camera yako , mic yako ya simu na accounts zako za hela kama Tigo pesa na kadhalika. Hatari kweli, inabidi uwe muangalifu sana ni link gani una fungua kutoka kwenye simu yako, na ni apps gani una download.

Jamani Weekend ya kwanza ya Ramadhani Alhamdullillah tunaimalizia! 
Mwenyezu Mungu atuwezeshe tuweze kumaliza Ramadhani yetu salama. Msisahau kuwechekeni majirani zenu jamani ambao majiko yao hayawakagi mara nyingi.

Friday, May 10, 2019

Aya ya Leo - Mazuri yanatoka kwa Allah (Goodness is From Allah)



Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu [Ewe Binadamau] linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma [Ewe Muhamad] kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha.
 
What comes to you of good is from Allah, but what comes to you of evil, [O man], is from yourself. And We have sent you, [O Muhammad], to the people as a messenger, and sufficient is Allah
as Witness. (Qur'an 4:79)
 
Happy First Friday of Ramadhan!

Thursday, May 9, 2019

Futariii Bureee China na Silent Ocean

Jamani makampuni yakifanya vitu vizuri namna hii, kwakweli tutawapa free promo.

Mashaallah! Mashaallah! Ni Mfano wa kuigwa. Inasaidia sana ukiwa mgeni kwenye nchi za watu.
Mwenyezi Mungu awaongezee pale walipo pungukiwa na azidi kuwafungulia milango yao ya kheri.

Mawaidha ya Leo kutoka kwa Nouman Ali Khan

Your Fasting Will Be Wrong If You Do This

Wednesday, May 8, 2019

Msomi wa Leo - Al Būsīrī (1212-1295)

Abu Abdullah Muhammad ibn Sa'īd ul-Būsīrī Ash Shadhili  Almaarufu Al-Busiri, alizaliwa Misri mwaka 1212. Al-Busiri alipata elimu yake ya dini chini ya Sheikh Al-Mursi Abu'l-'Abbas, Alikuwa anajulikana kama Mshairi Maarufu sana Misri.

Al-Busiri japukuwa alikuwa ni Mshairi wa Misri, familia yake ilitokea Moroko. Alianza kuandika Mashairi yake chini ya Ibn Hinna vizier wa Misri. Aliandika mashairi mengi lakini Mashairi yake maarufu ni Qasida al-Burda. Qaswida hizo tunazisikia mpaka leo kwenye maulidi na maharusi, na washairi waliokuja baada yake, bado wanazitumia mashairi yake kama misingi ya mashairi yao. Qaswida zake ziliweza kutafsiriwa kwenye lugha tofauti na zikakuza ukubwa wake. Busiri alifariki mwaka 1295 mjini Alexandria, Misri. 

Sikiliza moja ya Qaswida kwenye kitabu chake cha Qasida Al-Burda.


Mwenyezi Mungu Amuwekee Nuru Kwenye Kaburi lake na Amuinue daraja kwenye Pepo yake. 


Tuesday, May 7, 2019

Qaswida ya Leo kutoka Uingereza- Sami Yusuf

Swali Je Umejitayarishaje ukiitwa na Mola Wako?
Question, How well have you prepared yourself when your called back by your Lord?




Hebu tutafakari kidogo kwenye Mwezi huu Mtukufu.

Monday, May 6, 2019

Hadithi ya Leo - Muda wa Kufunga (When to fast)



Imehadithiwa na Abdullah bin Umar:

Mtume was Allah alisema, " Mwezi unaweza kuwa usiku 29, na msifunge mpaka muuone mwezi, na kama kuna mawingu, basi malizieni siku thalathini ya Sha'ban."

Narrated `Abdullah bin `Umar:

Allah's Messenger (ﷺ) said, "The month (can be) 29 nights (i.e. days), and do not fast
till you see the moon, and if the sky is overcast, then complete Sha'ban as thirty days."
(Bukhari 1907)

Sunday, May 5, 2019

Ramadhan 2019 Kareem!

Ramadhan is here and oh how exciting . 


For those Starting on Monday, may it be a blessing for you and your family and for the rest of us starting on Tuesday, Happy last day of Shabaan and may we all celebrate Eid together. 

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kuanza Jumanne Mei 7, 2019

Friday, March 15, 2019

Aya ya Leo - Muhammad



Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili  kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda  mema katika wao msamaha na ujira mkubwa.

Muhammad is the Messenger of Allah ; and those with him are forceful against the disbelievers,  merciful among themselves. You see them bowing and prostrating [in prayer], seeking bounty from  Allah and [His] pleasure. Their mark is on their faces from the trace of prostration. That is their  description in the Torah. And their description in the Gospel is as a plant which produces its offshoots and strengthens them so they grow firm and stand upon their stalks, delighting the sowers - so that Allah may enrage by them the disbelievers. Allah has promised those who believe and do righteous deeds among them forgiveness and a great reward. 
 (Qur'an 48:29)
Ijumaa Kareem!

Monday, March 11, 2019

✈️ China orders airlines to ground Boeing 737 MAX 8 after crash | Al Jaz...

Aircraft manufacturer Boeing says it has 'no new guidance' to offer. Seriously! Boeing? I think its time to switch to Airbus.


To God we belong and to him is our return.
What a tragedy!May Allah give comfort to the families left behind and may He accept their souls in his heaven.

Hadithi ya Leo - Ukarimu(Mercy)


Ime hadithiwa na Jarir bin Abdullahi:
Mtume wa Allah alisema, "Allah hata onyesha ukarimu kwa wale wasiokuwa na ukarimu kwa wanaadamu."

Narrated Jarir bin Abdullah:
Allah's Messenger (ﷺ)said, "Allah will not be merciful to those who are not merciful to mankind."
 (Sahih Al-Bukhari 7376)
Happy Monday!

Friday, March 8, 2019

Friday, March 1, 2019

Aya za Leo - Ujumbe wa Muhammad(S.A.W)(Muhammad's Message)

Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; imefunguliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanao mshirikisha, Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera.
Hakika wanao amini na wakatenda mema watakuwa na ujira usio na ukomo.  

Say, O [Muhammad], "I am only a man like you to whom it has been revealed that your god is but one God; so take a straight course to Him and seek His forgiveness." And woe to those who associate others with Allah -Those who do not give zakah, and in the Hereafter they are disbelievers.
Indeed, those who believe and do righteous deeds - for them is a reward uninterrupted.

(Qur'an 41:6-8)
                                                                   Jumaa Mubarak!

Monday, February 25, 2019

Hadithi ya Leo - Tiba (Cure)


Abdul-Aziz bin Suhaib alisema:"Thabit Al-Bunani na mimi tulienda kwa Anas bin Malik na 
Thabit akasema: ' Ewe Abu Hamzah! Nina sumbuliwa na maradhi.'
Basi Anas akasema: ' Je nikusomee Ruqya ya Mtume wa Allah juu yako?'
Akasema: 'Ndiyo'.
Akasema:' Ewe Allah! Mola wa Nafsi zote, ondoa maradhi yake na umpe tiba. Kwani wewe ndiye unaye toa tiba, na hakuna anaye toa tiba bali wewe, tiba ambaye haiachi maradhi yoyote.

Abdul-Aziz bin Suhaib said:"Thabit Al-Bunani and I entered upon Anas bin Malik, and
Thabit said: 'O Abu Hamzah! I am suffering from an illness.
So Anas said: 'Shall I not recite the Ruqyah of the Messenger of Allah over you?'
He said: 'Why, yes.'
He said: 'O Allah! Lord of mankind, remove the harm, and cure (him).Indeed You are the One Who cures, there is none who cures except you, a cure that leaves no disease.'"

"‏ اللَّهُمَّ رَبَّ النَّاسِ مُذْهِبَ الْبَاسِ اشْفِ أَنْتَ الشَّافِي لاَ شَافِيَ إِلاَّ أَنْتَ شِفَاءً لاَ يُغَادِرُ سَقَمًا ‏"
(Tirmidhi 973)

Happy Monday!

Friday, February 15, 2019

Aya ya Leo - Waumini (Believers)

NA WAUMINI WANAUME NA WAUMINI WANAWAKE WAO KWA WAO NI MARAFIKI WALINZI. HUAMRISHA MEMA NA HUKATAZA MAOVU, NA HUSHIKA SALA, NA HUTOA ZAKA, NA HUMT'II MWENYEZI MUNGU NA MTUME WAKE. HAO MWENYEZI MUNGU ATAWAREHEMU. HAKIKA MWENYEZI MUNGU NI MTUKUFU MWENYE NGUVU, MWENYE HIKIMA.

The believing men and believing women are allies of one another. They enjoin what is right and forbid what is wrong and establish prayer and give zakah and obey Allah and His Messenger. Those - Allah will have mercy upon them. Indeed, Allah is Exalted in Might and Wise.

(Qur'an 9:71)

Monday, February 11, 2019

Hadithi ya Leo - Theluthi ya Quran ( A third of the Quran)


Imehadhithiwa na Abu Hurairah:
Kwamba Mtume wa Allah alisema: " Jikusanyeni na nitawasomea theluthi ya Qurani. "
Akasema: " Yoyote aliyeweza akajikusanya, basi Mtume wa Allah akatoka na kusoma Qul Huwa Allahu Ahad, kisha akarudi ndani. Baadhi ya watu wakaanza kuambizana, "Mtume wa Allah alisema: 'Nitasoma theluthi ya Qurani, nilifikiri hizi ni habari za Peponi.'" Mtume wa Allah akatoka nje na kusema: " Ni Kweli nilisema nitawasomea theluthi ya Qurani, na hii ni kama theluthi ya Qurani."
 
Narrated Abu Hurairah:
that the Messenger of Allah (ﷺ) said: "Gather and I shall recite to you one third of the Qur'an." He said: "So whoever was to gather did so, then the Messenger of Allah (ﷺ) came out and recited Qul Huwa Allahu Ahad. Then he went back in. Some of them said to each other: "The Messenger of Allah (ﷺ) said: 'I shall recite to you one third of the Qur'an I thought that this was news from the Heavens. Allah's Prophet (ﷺ) came out and said: "Indeed I said that I would recite to you one third of the Qur'an, and it is indeed equal to one third of the Qur'an."
 (Tirmidhi: Vol. 5, Book 42, Hadith 2900)




Happy Monday! Msisahau kusoma Qul Huwa Allahu jamani.











Friday, February 8, 2019

Sura ya Leo - Allah

Sema: Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee.
Mwenyezi Mungu Mkusudiwa.
Hakuzaa wala hakuzaliwa.
Wala hana anaye fanana naye hata mmoja.

(Qur'an 112:1-4)
Jumaa Mubarak Wadau.



Friday, February 1, 2019

Aya ya Leo - Onyo (Warning)

Basi ole wao wanao andika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie nacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyo andika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayo yachuma. 

 

So woe to those who write the "scripture" with their own hands, then say, "This is from Allah," in order to exchange it for a small price. Woe to them for what their hands have written and woe to them for what they earn.
(Qur'an 2:79)

Jumaa Mubarak Wadau.



Friday, January 25, 2019

Aya ya Leo - Niiteni (Call upon Me)

Have you made your call yet?
 

Na  Mola wenu Mlezi anasema: "Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu bila shaka wataingia Jahanamu wadhalilike."

And your Lord says: "Call on Me; I will answer your (Prayer): but those who are too arrogant to serve Me will surely find themselves in Hell - in humiliation!" (Qur'an 40:60)
Jumaa Kareem! 




Friday, January 18, 2019

Aya za Leo - Watu Wema (The Righteous)

  Hakika tumemuumba Mwanaadamu katika taabu.
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
Kwani hatukumpa macho mawili?
Na ulimi, na midomo miwili?
Na tukambainishia zote njia mbili (iliyo Njema na Mbaya)?
Lakini hakujituma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
Na nini kitakachokujulisha ni nini njia ya vikwazo vya milimani?  
Kumkomboa mtumwa;
Au kumlisha siku ya njaa
Yatima aliye jamaa (Na asiyekua jamaa),
Au masikini aliye vumbini.
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

We have certainly created man into hardship.
Does he think that never will anyone overcome him?
He says, "I have spent wealth in abundance."
Does he think that no one has seen him?
Have We not made for him two eyes?
And a tongue and two lips?
And have shown him the two ways?
But he has not broken through the difficult pass.
And what can make you know what is [breaking through] the difficult pass?
It is the freeing of a slave
Or feeding on a day of severe hunger
An orphan of near relationship
Or a needy person in misery
And then being among those who believed and advised one another to patience and advised one another to compassion.
Those are the companions of the right.
(Qur'an 90:4-18)

Ijumaa Njema!

Friday, January 11, 2019

Surah ya Leo - Al Waaqi'ah - Isiyozuilika (The Inevitable)

Je wewe ni watu wa mkono wa kulia? Umejitayarishaje uwe angalau ata wale wa mwisho mwisho kwenye kundi la watu wenye kheri?

Qu'ran Chapter 56.
Msomi Sheikh Yusuf Simbano.
Ijumaa Njema Wadau!

Friday, January 4, 2019

Aya ya Leo - Maisha ya Dunia(Worldy Life)



Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri. 

The example of [this] worldly life is but like rain which We have sent down from the sky that the plants of the earth absorb - [those] from which men and livestock eat - until, when the earth has taken on its adornment and is beautified and its people suppose that they have capability over it, there comes to it Our command by night or by day, and We make it as a harvest, as if it had not flourished yesterday. Thus do We explain in detail the signs for a people who give thought.
 (Qur'an 10:24)
Ijumaa Njema!

Aya ya Leo - Alama (Signs)

  Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.

Indeed, in the creation of the heavens and earth, and the alternation of the night and the day, and the [great] ships which sail through the sea with that which benefits people, and what Allah has sent down from the heavens of rain, giving life thereby to the earth after its lifelessness and dispersing therein every [kind of] moving creature, and [His] directing of the winds and the clouds controlled between the heaven and the earth are signs for a people who use reason.
(Qur'an 2:164) 
Jumaa Mubarak!