Translate

Friday, January 25, 2019

Aya ya Leo - Niiteni (Call upon Me)

Have you made your call yet?
 

Na  Mola wenu Mlezi anasema: "Niombeni nitakujibuni. Kwa hakika wale wajivunao kufanya ibada yangu bila shaka wataingia Jahanamu wadhalilike."

And your Lord says: "Call on Me; I will answer your (Prayer): but those who are too arrogant to serve Me will surely find themselves in Hell - in humiliation!" (Qur'an 40:60)
Jumaa Kareem! 




Friday, January 18, 2019

Aya za Leo - Watu Wema (The Righteous)

  Hakika tumemuumba Mwanaadamu katika taabu.
Ati anadhani hapana yeyote ataye muweza?
Anasema: Nimeteketeza chungu ya mali.
Ati anadhani ya kuwa hapana yeyote anaye mwona?
Kwani hatukumpa macho mawili?
Na ulimi, na midomo miwili?
Na tukambainishia zote njia mbili (iliyo Njema na Mbaya)?
Lakini hakujituma kwenye njia ya vikwazo vya milimani.
Na nini kitakachokujulisha ni nini njia ya vikwazo vya milimani?  
Kumkomboa mtumwa;
Au kumlisha siku ya njaa
Yatima aliye jamaa (Na asiyekua jamaa),
Au masikini aliye vumbini.
Tena awe miongoni mwa walio amini na wakausiana kusubiri na wakausiana kuhurumiana.
Hao ndio watu wa kheri wa kuliani.

We have certainly created man into hardship.
Does he think that never will anyone overcome him?
He says, "I have spent wealth in abundance."
Does he think that no one has seen him?
Have We not made for him two eyes?
And a tongue and two lips?
And have shown him the two ways?
But he has not broken through the difficult pass.
And what can make you know what is [breaking through] the difficult pass?
It is the freeing of a slave
Or feeding on a day of severe hunger
An orphan of near relationship
Or a needy person in misery
And then being among those who believed and advised one another to patience and advised one another to compassion.
Those are the companions of the right.
(Qur'an 90:4-18)

Ijumaa Njema!

Friday, January 11, 2019

Surah ya Leo - Al Waaqi'ah - Isiyozuilika (The Inevitable)

Je wewe ni watu wa mkono wa kulia? Umejitayarishaje uwe angalau ata wale wa mwisho mwisho kwenye kundi la watu wenye kheri?

Qu'ran Chapter 56.
Msomi Sheikh Yusuf Simbano.
Ijumaa Njema Wadau!

Friday, January 4, 2019

Aya ya Leo - Maisha ya Dunia(Worldy Life)



Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni, kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza, iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri. 

The example of [this] worldly life is but like rain which We have sent down from the sky that the plants of the earth absorb - [those] from which men and livestock eat - until, when the earth has taken on its adornment and is beautified and its people suppose that they have capability over it, there comes to it Our command by night or by day, and We make it as a harvest, as if it had not flourished yesterday. Thus do We explain in detail the signs for a people who give thought.
 (Qur'an 10:24)
Ijumaa Njema!

Aya ya Leo - Alama (Signs)

  Hakika katika kuumbwa kwa mbingu na ardhi, na kukhitalifiana usiku na mchana, na marikebu ambazo hupita baharini kwa viwafaavyo watu, na maji anayo yateremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na akaeneza humo kila aina ya wanyama; na katika mabadiliko ya pepo, na mawingu yanayo amrishwa kupita baina ya mbingu na ardhi, bila shaka zimo Ishara kwa watu wanao zingatia.

Indeed, in the creation of the heavens and earth, and the alternation of the night and the day, and the [great] ships which sail through the sea with that which benefits people, and what Allah has sent down from the heavens of rain, giving life thereby to the earth after its lifelessness and dispersing therein every [kind of] moving creature, and [His] directing of the winds and the clouds controlled between the heaven and the earth are signs for a people who use reason.
(Qur'an 2:164) 
Jumaa Mubarak!