Translate

Friday, August 29, 2014

Aya ya Leo - Iblees

Na [waelezee] tulivyo waambia malaika, "Msujudieni Adam", waka sujudi ila Iblis. Yeye alikuwa moja wa majini, na akavunja amri ya mola wake. Je, mtamchukua yeye na vizazi vyake kama walinzi wenu badala ya mimi? wakati wao ni adui zenu! Mabaya ndio yatakuwa mabadilishano yenu kwa watendao mabaya.

And [mention] when We said to the angels, "Prostrate to Adam," and they prostrated, except for Iblees. He was of the jinn and departed from the command of his Lord. Then will you take him and his descendants as allies other than Me while they are enemies to you? Wretched it is for the wrongdoers as an exchange. (Qur'an 18:50)

Monday, August 25, 2014

Hadithi ya Leo - Unyenyekevu

Iyad bin Himar alisema:
Mtume wa Allah(S.A.W) alisema:
"Allah alini fungulia kwamba mnyenyekeane. Mtu asijiinue yeye kuwa juu ya mwingine wala msitendeane maovu."


'Iyad bin Himar (May Allah be pleased with him) reported:
Messenger of Allah (ﷺ) said, "Allah has revealed to me that you should humble yourselves to one another. One should neither hold himself above another nor transgress against another."
Muslim Book 1, Hadith 602

Friday, August 22, 2014

Aya ya Leo - Allah

Sifa njema zote ni za Allah, Mola na Mlezi wa madunia.

Praise be to Allah, the Cherisher and Sustainer of the worlds.(Qur'an 1:2)

Wednesday, August 20, 2014

Monday, August 18, 2014

Hadithi ya Leo - Salamu(Greetings)

Ime hadithiwa na Abu Hurairah:
Kwamba mtume wa Allah(S.A.W) alisema: " Kwa yule ambaye kwenye mkono wake ni Roho yangu! Huta ingia Peponi mpaka uamini, na huta amini mpaka mpendane. Niwaambieni jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Salimianeni."


Narrated Abu Hurairah:
that the Messenger of Allah (ﷺ) said: "By the One in Whose Hand is my soul! You will not enter Paradise until you believe, and you will not believe until you love one another. Shall I inform you about a matter which if you do it, then you will love one another? Spread the Salam among each other."
Tirmidhi 2688

Friday, August 15, 2014

Aya ya Leo - Mitume(Prophets)


Na hatukuwatuma mitume bali wawaletee habari njema na kuwaonya. Na wale wasio amini na kubisha kwa kutumia uwongo [wanajaribu] kubatilisha ukweli, na wamechukua aya zangu zinazo waonyana na kuzi kejeli .

And We send not the messengers except as bringers of good tidings and warners. And those who disbelieve dispute by [using] falsehood to [attempt to] invalidate thereby the truth and have taken my verses, and that of which they are warned, in ridicule.(Qur'an 18:56)

Mawaidha ya Leo kutoka kwa Mufti Menk

Before You Share Photos Online, Watch This - Mufti Menk
Sheikh anakwambia mna post vipicha vyenu mitandaoni mnakula maraha, mnakaribisha wivu, chuki na vijicho.
Habari ndiyo hiyo!

Monday, August 11, 2014

Hadithi ya Leo- Kutia Wuḍūʾna Soksi


Imehadithiwa na Urwa bin Al-Mughira:
Baba yangu alisema, "Kuna siku nilikuwa na mtume(ﷺ) safarini na nikawahi kumtoa Khuffs(Soksi zilizo tengenezwa na kitambaa kizito au ngozi). Akani amrisha nizi wache, kwani alizivaa baada ya kutia wudhu. Basi akapaka maji juu yake".


Narrated `Urwa bin Al-Mughira:
My father said, "Once I was in the company of the Prophet (ﷺ) on a journey and I dashed to take off his Khuffs (socks made from thick fabric or leather). He ordered me to leave them as he had put them after performing ablution. So he passed wet hands over them".( Bukhari 206)

Friday, August 8, 2014

Aya ya Leo - Wuḍūʾ


Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru

O you who have believed, when you rise to [perform] prayer, wash your faces and your forearms to the elbows and wipe over your heads and wash your feet to the ankles. And if you are in a state of janabah, then purify yourselves. But if you are ill or on a journey or one of you comes from the place of relieving himself or you have contacted women and do not find water, then seek clean earth and wipe over your faces and hands with it. Allah does not intend to make difficulty for you, but He intends to purify you and complete His favor upon you that you may be grateful.(Qur'an 5:6)
Ijumaa Njema Wadau!

Monday, August 4, 2014

Hadithi ya Leo - Kutia Wuḍūʾna Soksi


Imehadithiwa na Al-Mughira bin Shu'ba:
Nilikuwa na Mtume wa Allah(S.A.W) kwenye moja ya safari zake, na akaenda kujisaidia. Aliporudi, nikawa nammiminia maji ya kutia Wuḍūʾ; akaosha uso, mikono na akapaka maji kichwani na juu ya Khuff(soksi zilizo tengenezwa na kitambaa kizito au ngozi) zake.

Narrated Al-Mughira bin Shu`ba:
I was in the company of Allah's Messenger (ﷺ) on one of the journeys and he went out to answer the call of nature (and after he finished) I poured water and he performed ablution; he washed his face, forearms and passed his wet hand over his head and over the two Khuff (socks made from thick fabric or leather).
(Bukhari 182)

Saturday, August 2, 2014

Friday, August 1, 2014

Aya za leo - Mungu Akipenda(If Allah Wills)


Na usiliongelee jambo, "hakika, kesho ntalifanya", bila[kuongezea], "Mwenyezi Mungu akipenda". Na mkumbuke mola wako unaposahau na useme, " Pengine mola wangu ataniongoza kwa kile kilicho kuwa karibu zaidi kwa wema kuliko hiki .

And never say of anything, "Indeed, I will do that tomorrow", Except [when adding], "If Allah wills." And remember your Lord when you forget [it] and say, "Perhaps my Lord will guide me to what is nearer than this to right conduct." (Qur'an 18:23-24)