Translate

Friday, December 29, 2017

Aya za Leo - Ufunuo (Revelation)



Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima!
Hakika wewe ni miongoni mwa walio tumwa,
Kwenye Njia Iliyo Nyooka.
[Huu ni] Uteremsho wa Mwenye Nguvu, Mwenye Kurehemu.
Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika.

By the wise Qur'an.
Indeed you, [O Muhammad], are from among the messengers,
On a straight path.
[This is] a revelation of the Exalted in Might, the Merciful,
That you may warn a people whose forefathers were not warned, so they are unaware.
(Qur'an 36:2-6)

Happy Last Friday of the year everyone. May Allah bless us all and make 2018 a year filled with plenty of his blessings.

Friday, December 8, 2017

Aya ya Leo - Talaka (Divorce)




Na mtakapo wapa wanawake t'alaka, nao wakafikia kumaliza eda yao, basi warejeeni kwa wema au waachilieni kwa wema. Wala msiwarejee kwa kuwadhuru mkafanya uadui. Na atakaye fanya hivyo, amejidhulumu nafsi yake. Wala msizichukulie Aya za Mwenyezi Mungu kwa maskhara. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, na aliyo kuteremshieni katika Kitabu na hikima anacho kuonyeni kwacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.


And when you divorce women and they have [nearly] fulfilled their term, either retain them according to acceptable terms or release them according to acceptable terms, and do not keep them, intending harm, to transgress [against them]. And whoever does that has certainly wronged himself. And do not take the verses of Allah in jest. And remember the favor of Allah upon you and what has been revealed to you of the Book and wisdom by which He instructs you. And fear Allah and know that Allah is Knowing of all things. (Qur'an 2:231)
Ijumaa Njema Wandugu.

Friday, December 1, 2017

Send Salutations upon Him the Intercessor of the Muslim Nation - Sami Yusuf

Mwenyezi Mungu atujaalie wote In'Shaa'llah tuwe kwenye lile kundi atakaye tuombea siku ya kiyama.

These videos have subtitles, make sure yours is turned on if you want to see the translation.
Happy Mawlid Al-Nabi!

Aya ya Leo - Muhammad (S.A.W)


Ewe Mtume, kwa hakika tumekutuma kama shahidi na mleta habari njema pamoja na Onyo.

O Prophet, indeed We have sent you as a witness and a bringer of good tidings and a Warner. 
(Qur'an 33:45)

Jumaa Mubarak na Maulid Njema Wadau!

Friday, November 24, 2017

Aya ya Leo - Mtihani (Test)

It is coming, and guess what its part of life. Allah anakuelekeza chakufanya.

Hakika mtapewa mitihani katika mali zenu na nafsi zenu, na bila ya shaka mtasikia udhia mwingi kutoka kwa walio pewa Kitabu kabla yenu na wale wanao mshirikisha Allah. Na ikiwa mtasubiri na mkamcha Mungu basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimia.

You will surely be tested in your possessions and in yourselves. And you will surely hear from those who were given the Scripture before you and from those who associate others with Allah much abuse. But if you are patient and fear Allah - indeed, that is of the matters [worthy] of determination.(Qur'an 3:186)
IJumaa Njema Wadau!

Monday, November 20, 2017

Hadithi ya Leo - Vitu Saba Kila Muislamu humpasa kufanya (Seven things every Muslim must do)

Je unaya tenda?

Imehadithiwa na Al-Bara' bin 'Azib:

Mtume wa Allah (ﷺ) alituamrisha kufanya vitu saba na alitukataza kufanya vitu saba vingine. Vitu alivyo amrisha ni:
1. Kufuata maandamano ya mazishi
2. Kumtembelea Mgonjwa
3. Kukubali mualiko
4. Kusaidia wanaoonewa
5. Kutimiza Ahadi
6. Kurudisha Salamu
7. Kumjibu anayo piga chafya ( kwakusema, " Mwenyezi Mungu awe na huruma na wewe, kama mpiga chafya atasema, "Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu").

Na katukataza: Kutumia vijiko vya fedha,  na vyombo vya fedha, kuvaa pete za dhahabu, kuvaa nguo za hariri, Dibaj( hariri tupu), Qissi na Istabrag (Aina zingine mbili za hariri).


Narrated Al-Bara' bin `Azib:
 

Allah's Messenger (ﷺ) ordered us to do seven things and forbade us to do other seven. 
He ordered us:
1. To follow the funeral procession.

2. To visit the sick.
3. To accept invitations.
4. To help the oppressed.
5. To fulfill the oaths.
6. To return the greeting.
7. To reply to the sneezer: (saying, "May Allah be merciful on you,"
provided the sneezer says, "All the praises are for Allah,"). 


He forbade us to use silver utensils and dishes and to wear golden rings, silk (clothes),
Dibaj (pure silk cloth), Qissi and Istabraq (two kinds of silk cloths).

(Sahih al-Bukhari  Book 23, Hadith 3)

Friday, November 17, 2017

Aya ya Leo - Death (Kifo)

Tick Tock!⏰

Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu.

Every soul will taste death, and you will only be given your [full] compensation on the Day of Resurrection. So he who is drawn away from the Fire and admitted to Paradise has attained [his desire].
And what is the life of this world except the enjoyment of delusion.
(Qur'an 3:185)
Jumaa Mubarak!

Monday, November 6, 2017

Hadithi ya Leo - Nini Uislamu (What is Islam)


Ime hadithiwa na Abu Huraira kwamba Mtume wa Allah alisema:
Niulizeni vitu vinavyo husu dini, lakini wale(masahaba wa mtume) kwa kumhesimu Mtume walishindwa kuuliza maswali. 

Akaja mtu wasiomjua na kukaa karibu na mtume akauliza, Mtume wa Allah, nini Uislamu?
Mtume Akamjibu, Hutakiwi kumshirikisha Allah na chochote, unatakiwa uswali, ulipe Zakat kwa maskini, na ufunge mwezi wa ramadhani. Yule Mtu akasema, umeongea ukweli. 

Akauliza tena, Mtume wa Allah, nini Imani?  
Mtume Akamjibu, Kumuani Allah, Malaika wake, vitabu vyake, kukutana naye, mitume wake, na kuamini siku ya kufufuka na Qadr(Amri zake). Yule Mtu akasema, umeongea ukweli.

Akauliza tena, Mtume wa Allah, nini ihsan? 
Mtume Akajibu, Ihsan inamaanisha kwamba 
unamuogopa Allah kama vile unamuona, japokuwa humuoni, lakini yeye anakuona. Yule Mtu akamjibu, umongea ukweli.

Akauliza tena, lini siku ya kiyama? 
Mtume Akamajibu, Yule anayoulizwa hana huo ujuzi kuliko muulizaji. Lakini mimi nitahadithia baadhi ya ishara zake, nazo ni: ukimuona mtumwa akizaa mkuu wake, hiyo ni moja ya ishara zake, ukimwona mtu peku, bila nguo, kiziwi na bubu( yaani mtu Mjinga na mpumbavu) ndio anayoiongoza dunia, hiyo ni moja ya ishara zake. Ukiona wachungaji wa ngamia weusi wakifurahia majengo, hiyo ni moja ya ishara zake.
Kiyama ni moja ya vitu vitano vilivyo kwenye vitu visivyojulikana. Hamna anayeyajua isipokuwa Allah. Alafu mtume akasoma aya hii kutoka kwenye Qur'an.
Hakika Allah, ni yeye pekee anayejua kuhusu siku ya kiyama, na ni yeye mwenye kutuma mvua, na anajua yaliyoko kwenye matumbo. Na hakuna anayejua yatakayo mkuta kesho, na atakapofia. Ni Allah ndio anayejua na anayefahamu.

Abu Huraira akasema, Yule mtu akaamka na kuondoka zake. Mtume wa Allah, akasema mtafuteni, masahaba wakamtafuta lakini hawakumpata.
Hapo ndio mtume wa Allah akasema, yule alikuwa ni Jibril, alitaka kuwafundisha nyinyi vitu vya dini, mlivyoshindwa kuuliza wenyewe.


It is narrated on the authority of Abu Huraira that the Messenger of Allah (ﷺ) said:
Ask me (about matters pertaining to religion), but they (the Companions of the Holy Prophet) were too much overawed out of profound respect for him to ask him (anything). 

In the meanwhile a man came there, and sat near his knees and said: Messenger of Allah,
 What al-lslam is? 
-to which he (the Holy Prophet) replied: You must not associate anything with Allah, and establish prayer, pay the poor-rate (Zakat) and observe (the fasts) of Ramadan. He said: You (have) told the truth. 

He (again) said: Messenger of Allah, What al-Iman (the faith) is?  
He (the Holy Prophet) said: That you affirm your faith in Allah, His angels, His Books, His meeting, His Apostles, and that you believe in Resurrection and that you believe in Qadr (Divine Decree) in all its entirety, He (the inquirer) said: You (have) told the truth. 

He (again) said: Messenger of Allah, What al-Ihsan is? 
Upon this he (the Holy Prophet) said: (Al-Ihsan implies) that you fear Allah as if you are seeing Him, and though you see Him not, verily He is seeing you. He (the inquirer) said: You (have) told the truth. 

He (the inquirer) said: When there would be the hour (of Doom)? 
(Upon this) he (the Holy Prophet said: The one who is being asked about it is no better informed than the inquirer himself. I, however, narrate some of its signs (and these are): when you see a slave (woman) giving birth to her master - that is one of the signs of (Doom) ; when you see barefooted, naked, deaf and dumb (ignorant and foolish persons) as the rulers of the earth - that is one of the signs of the Doom. And when you see the shepherds of black camels exult in buildings - that is one of the signs of Doom. The (Doom) is one of the five things (wrapped) in the unseen. No one knows them except Allah. Then (the Holy Prophet) recited (the following verse):

" Verily Allah! with Him alone is the knowledge of the hour and He it is Who sends down the rain and knows that which is in the wombs and no person knows whatsoever he shall earn on morrow and a person knows not in whatsoever land he shall die. Verily Allah is Knowing, Aware". 

He (the narrator, Abu Huraira) said: Then the person stood up an (made his way). The Messenger of Allah (ﷺ) said: Bring him back to me. He was searched for, but they (the Companions of the Holy Prophet) could not find him. The Messenger of Allah (ﷺ) thereupon said: He was Gabriel and he wanted to teach you (things pertaining to religion) when you did not ask (them yourselves).
(Sahih Muslim Book 1 Hadith 7)



Monday, October 30, 2017

Why was there never a black Prophet !!! - Sh Omar Suleiman

Kwanini Hakujawai kuwa na Mtume Mweusi?

I nearly chocked on my water. I bet you didn't see that one coming.
Looks like I need to bring back the Monday Hadith series, we seem to be missing out.
Happy Monday everyone, have a wonderful and eventful week.

Friday, October 27, 2017

Aya ya Leo - Usimzulie Allah Msiyojajua (Don't Say about Allah what you don't know)



Na wanapo fanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu. Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua?

And when they commit an immorality, they say, "We found our fathers doing it, and Allah has ordered us to do it." Say, "Indeed, Allah does not order immorality. Do you say about Allah that which you do not know?" (Qur'an 7:28)
 Jumaa Mubarak!

Monday, October 23, 2017

Mawaidha ya Leo (Muda) (Time) - Mufti Menk


Kweli Siku hizi kuna distractions nyingi. Siku inaisha unajikuta mtu umepoteza muda wako kwenye vitu visivyo na maana na wala havija kuongeza kifikra, kidini wala kimaendeleo.

Vitu vya Kutafakari!
Mwenyezi Mungu Tuepushe na Tuongoze.
Jumatatu Njema wadau, Mwenyezi Mungu akujaalie wiki yako iwe na maendeleo mema.

Friday, October 20, 2017

Aya ya Leo - Chunga Nafsi Yako (Guard Your Soul)

Enyi mlio amini! Kilicho lazima juu yenu ni nafsi zenu. Hawakudhuruni walio potoka ikiwa nyinyi mmeongoka. Ni kwa Mwenyezi Mungu ndio marudio yenu nyote; basi atakwambieni yale mliyo kuwa mkiyatenda.

O you who have believed, upon you is [responsibility for] yourselves. Those who have gone astray will not harm you when you have been guided.  To Allah is your return all together; then He will inform you of what you used to do. (Qur'an 5:105)

Jumaa Mubarak!

Monday, October 16, 2017

Qur'an Recitation by Yaseen Rajab from Syria!

 Lets start our week right.
God Gifted Talent of Syrian Kid ~ Amazing Quran Recitation, imitates Abd...


Mashaallah! May Allah bless him and his family with all of his heart's desire in this world and the next.
Have a blessed week.

Friday, October 13, 2017

Aya za Leo - Adabu (Manners)


Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri,Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili, na wanaficha fadhila alizo wapa Mwenyezi Mungu. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya fedheha, Na ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu, wala hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho; na yule ambaye Shet'ani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya mno.

Worship Allah and associate nothing with Him, and to parents do good, and to relatives, orphans, the needy, the near neighbor, the neighbor farther away, the companion at your side, the traveler, and those whom your right hands possess.
Indeed, Allah does not like those who are self-deluding and boastful.Who are stingy and enjoin upon [other] people stinginess and conceal what Allah has given them of His bounty - and We have prepared for the disbelievers a humiliating punishment,And [also] those who spend of their wealth to be seen by the people and believe not in Allah nor in the Last Day. And he to whom Satan is a companion - then evil is he as a companion.
(Qur'an 4:36-38)
Ijumaa Njema Wandugu!

Friday, October 6, 2017

Aya za Leo - Jibril na Mikail (Gabriel and Michael)

Sema: Aliye kuwa ni adui wa Jibril, basi huyo ndiye aliye iteremsha Qur'ani moyoni mwako kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inayo thibitisha yaliyo kuwa kabla yake, na ni uwongofu na bishara njema kwa Waumini.

Say, "Whoever is an enemy to Gabriel - it is [none but] he who has brought the Qur'an down upon your heart, [O Muhammad], by permission of Allah, confirming that which was before it and as guidance and good tidings for the believers." (Qur'an 2:97)

Aliye kuwa adui wa Mwenyezi Mungu na Malaika wake na Mitume wake na Jibril na Mikail, basi hakika Mwenyezi Mungu ni adui wa makafiri.

Whoever is an enemy to Allah and His angels and His messengers and Gabriel and Michael - then indeed, Allah is an enemy to the disbelievers. (Qur'an 2:98)

Jumaa Mubarak!

Friday, September 29, 2017

Aya ya Leo - Onyo (Warning)


Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat'ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie khabari ya adhabu iliyo chungu.

O you who have believed, indeed many of the scholars and the monks devour the wealth of people unjustly and avert [them] from the way of Allah . And those who hoard gold and silver and spend it not in the way of Allah - give them tidings of a painful punishment.(9:34)
Ijumaa Njema!

Thursday, September 28, 2017

REPOST:::: Ashura (The Day of Atonement)

Ashura is a day that usually falls on the 10th day of the Month of Muharram( The January of the Islamic Calendar). Its history goes back to Moses's time and it commemorates the day that the jews were freed from Egypt, Moses (A.S) fasted on this day and told the people to fast. Muslims remember this day by fasting on the 9th and 10th day of the month of Muharam. It is also a day observed in mourning, as it is the day the grandson of prophet Mohammed(S.A.W), imam Hussein ibn Ali (R.A) was killed in the Battle of Karbala. So let's try to fast on the 9th and 10th of Muharam, in order to fully participate on this day of Atonement.

Ashura this year(2017) will fall on Friday and Saturday. 
Happy Fasting everyone!

Friday, September 22, 2017

Aya ya Leo - Allah


Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.  

It is He who has sent His Messenger with guidance and the religion of truth to manifest it over all religion, although they who associate others with Allah dislike it.(9:33)
Jumaa Mubarak!
 

Thursday, September 21, 2017

Happy New Islamic Year 1439!

Happy New Islamic Year!
Alhamdulillah!
Yeeeh! We made it, we are still here by the grace of Allah! 
If you lost a loved one in the past year, May Allah grant them Janna.
If 1438 was a trial for you, May Allah make this year easier for you.
Lets not forget to pray for all our brothers and sisters facing trials and tribulations right now, May Allah Protect them.
Don't get tired of praying, Keep your faith Strong and May Allah guide and protect us this year and the many more years to come. 
Aaamin!

Friday, September 15, 2017

Aya ya Leo - Nuru (The light)


Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.
 
They want to extinguish the light of Allah with their mouths, but Allah refuses except to perfect His light, although the disbelievers dislike it.(9:32)
Jumaa Mubarak!

Friday, September 8, 2017

Aya ya Leo - Misikiti (Masjid)



Hakika wanao amirisha misikiti ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, na wala hawamchi ila Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.
The mosques of Allah are only to be maintained by those who believe in Allah and
the Last Day and establish prayer and give zakah and do not fear except Allah,
for it is expected that those will be of the [rightly] guided.
(9:18)
Ijumaa Njema!

Friday, August 25, 2017

Aya ya Leo - Nyumba ya Kwanza ya Ibada (The First House of Worship)


Kwakweli, nyumba ya kwanza (ya Ibada) iliyotengezwa kwajili ya walimwengu ni ule wa Makkah - wenye baraka na muongozo wa ulimwengu.

Indeed, the first House [of worship] established for mankind was that at Makkah - blessed and a guidance for the worlds. (Qur'an 3:96)

Wednesday, August 23, 2017

The Facilities Management Team of Masjid Al-Haram

Appreciating their hard work. May Allah Reward them and bless their families.

No Laziness here, even the supervisors are out in the field.
May Allah guide and protect our brothers and sisters going for Hajj this year.
Mwenyezi Mungu awaongoze na awalinde ndugu zetu wanaokwenda Haji mwaka huu.

Friday, August 4, 2017

Aya ya Leo - Muda wa Umma (Term of Nations)


Na kila umma una muda wake. Utakapo fika muda wao basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia. 

And for every nation is a [specified] term. So when their time has come, they will not remain behind an hour, nor will they precede [it].(Qur'an 7:33)

Friday, July 7, 2017

Aya ya Leo - Mapenzi ya Mali (The love of wealth)

Watu wamepambiwa kupenda matamanio ya wanawake, na wana, na mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi asili, na mifugo, na mashamba. Hayo ni starehe ya maisha ya duniani; na kwa Mwenyezi Mungu ndio kwenye marejeo mema.

It has been made attractive for people to love the desired things; that is, women, children, hoarded heaps of gold and silver, branded horses, cattle and tillage.That is an enjoyment of the worldly life; but with Allah lies the beauty of the final resort. (Qur'an 3:14)

Jumaa Mubarak!

Friday, June 30, 2017

Aya ya Leo - Qur'an


Yeye ndiye aliye kuteremshia Kitabu hichi. Ndani yake zimo Aya muhkam, zenye maana wazi. Hizo ndizo msingi wa Kitabu hichi. Na ziko nyengine za mifano. Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitna, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili.

He is the One who has revealed to you the Book(the Qur'an). Out of it there are verses that are Muhkamat(of established meaning), which are the principal verses of the Book, and some others are Mutashabihat (whose definite meanings are unknown). Now those who have perversity in their hearts go after such part of it as is mutashabih, seeking (to create) discord, and searching for its interpretation (that meets their desires), while no one knows its interpretation except Allah; and those well-grounded in knowledge say:"We believe therein; all is from our Lord." Only the men of understanding observe the advice. (Qur'an 3:7)

Ijumaa Njema


Tuesday, June 27, 2017

Mariam Nabatanzi from Uganda Gave birth to 44 Children

When you wonder how our great great great grandmother Hawa( May peace be with her),was able to populate the world, Allah sometimes decides to show us that it can still happen even today.

This is woman is amazing, and may Allah guide her, give her patience and open more doors for her.

How to be a better person - Hamza Yusuf

Lets not forget to fast the first 6 days of Shawwal immediately after Ramadhan.

Friday, June 23, 2017

Aya ya Leo - Eda (Mourning Period)


Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi. Na wanapo timiza eda yao basi hapana ubaya
kwao kwa wanao jifanyia kwa mujibu wa ada. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.

And those who are taken in death among you and leave wives behind - they, [the wives, shall] wait four months and ten [days]. And when they have fulfilled their term, then there is no blame upon you for what they do with themselves in an acceptable manner.And Allah is [fully] Acquainted with what you do.(Qur'an 2:234)

Wednesday, June 21, 2017

Hadithi ya Leo - Taraweeh




Imehadhithiwa na Abu Huraira:

Nilimsikia Mtume wa Allah akisema kuhusu Ramadhani,"Yeyote aliyesali usiku Kwenye huo mwezi kwa Imani yote na matumaini ya kulipwa na Allah, basi dhambi zake zote zilizopita zita samehewa".

Narrated Abu Huraira:

I heard Allah's Messenger saying regarding Ramadhan, "Whoever prayed at night in it (the month of Ramadan) out of sincere Faith and hoping for a reward from Allah, then all his previous sins will be forgiven."
(Bukhari 2008)

Friday, June 16, 2017

Aya ya Leo - Kumnyonyesha Mtoto (Breastfeeding a baby)

Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kaamili kwa anaye taka kutimiza kunyonyesha. Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe. Na juu ya mrithi mfano wa hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa kwa kuridhiana na kushauriana, basi si vibaya kwao. Na mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha basi hapana ubaya kwenu mkitoa mlicho ahidi kwa mujibu wa ada. Na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayo yatenda.

Mothers may breastfeed their children two complete years for whoever wishes to complete the nursing [period]. Upon the father is the mothers' provision and their clothing according to what is acceptable. No person is charged with more than his capacity. No mother should be harmed through her child, and no father through his child. And upon the [father's] heir is [a duty] like that [of the father]. And if they both desire weaning through mutual consent from both of them and consultation, there is no blame upon either of them. And if you wish to have your children nursed by a substitute, there is no blame upon you as long as you give payment according to what is acceptable. And fear Allah and know that Allah is Seeing of what you do.(Qur'an 2:233)
Jumaa Mubarak!

Aya ya Leo - Imani (Belief)


Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake.

Na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako.

The Messenger has believed in what was revealed to him from his Lord, and [so have] the believers. All of them have believed in Allah and His angels and His books and His messengers, [saying], "We make no distinction between any of His messengers." 

And they say, "We hear and we obey. [We seek] our forgiveness, our Lord, and to You is the [final] destination." (Qur'an 2:285)
Ijumaa Njema!

Wednesday, June 14, 2017

Msomi wa Leo - Ibn Arabī

Abū 'Abdullāh Muḥammad ibn 'Alī ibn Muḥammad ibn `Arabī al-Ḥātimī aṭ-Ṭāʾī, alizaliwa Murcia, Spain tarehe 26 Juli 1165. Ibn Arabi alikuwa ni Mwandishi na Msomi mzuri wa dini.

Alianza elimu yake Seville mwaka 1182-1183. Walimu wake walikuwa ma imaam wa karne ya Almohad na wengine walikuwa ma qadi au khatib. Imaam wake wa dini alikuwa
Sheikh Mohammed ibn Qasim Al-Tamimi wa Morocco.Alimaliza masomo yake Morocco mwaka 1200 chini ya mwalimu wake Yusuf Al-Kumi.

Mwaka 1201, Ibn Arab alienda Hija, na akaishi Makkah kwa muda wa miaka mitatu. Hapo ndo alipoanza kuandika kazi yake ya Al-Futuhat al-Makkiyaa.
Baada ya kukaa Makka, alitembelea sehemu nyingi za Syria, Palenstine, Iraq,Anatolia, Baghdad na Madina. Ibn Arabi aliandika vitabu vyake Tanazzulāt al-Mawṣiliyya, Kitāb al-Jalāl wa’l-Jamāl na Kunh mā lā Budda lil-MurīdMinhu, alipoenda kutembelea Mosul na kufunga Ramadhani yake hapo.

Ibn Arabi aliendelea na safari zake na akatembelea Jerusalem, Makka, Misri, Aleppo na Damascus. Mwishoni alirejea Makka ambako aliendelea masomo yake na kudandika kwa muda wa miaka 4 hadi 5, na ni kwenye hii miji ndipo pia alikuwa akifanya ziara ya vitabu vyake. Alifariki dunia tarehe 8 Juli 1240.

Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na amlaze mahali pema peponi.

Tuesday, June 13, 2017

Aya ya Leo - Sala (Prayer)

Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea).

Maintain with care the [obligatory] prayers and [in particular] the middle prayer and stand before Allah, devoutly obedient.(Qur'an 2:238)

Sunday, June 11, 2017

Aya ya Leo - Riba(Interest)

Wale wanaokula riba hawatasimama [Siku ya Kiyama] ila kama anavyo simama anayepigwa na Shetani mpaka kuchanganyikiwa. Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.
Basi aliye fikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake Mlezi, kisha akajizuia, basi yake ni yaliyo kwisha pita, na mambo yake yako kwa Mwenyezi Mungu. Na wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.

Those who consume interest cannot stand [on the Day of Resurrection] except as one stands who is being beaten by Satan into insanity. That is because they say, "Trade is [just] like interest." But Allah has permitted trade and has forbidden interest. 
So whoever has received an admonition from his Lord and desists may have what is past, and his affair rests with Allah . But whoever returns to [dealing in interest or usury] - those are the companions of the Fire; they will abide eternally therein. (Qur'an 2:275)

Saturday, June 10, 2017

Aya ya Leo - Wealth (Mali)

Mfano wa wanao tumia mali zao katika Njia ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa punje moja iliyo chipuza mashuke saba. Katika kila shuke zimo punje mia.
Na Mwenyezi Mungu humzidishia amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mwenye kujua.

The example of those who spend their wealth in the way of Allah is like a seed [of grain] which grows seven spikes; in each spike is a hundred grains.
And Allah multiplies [His reward] for whom He wills. And Allah is all-Encompassing and Knowing.
(Qur'an 2:261)

Friday, June 9, 2017

Aya ya Leo - Mkopo kwa Allah (A Loan to Allah)

Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili amzidishie mzidisho mwingi, na Mwenyezi Mungu hukunja na hukunjua. Na Kwake Yeye mtarejea.

Who is it that would loan Allah a goodly loan so He may multiply it for him many times over? And it is Allah who withholds and grants abundance, and to Him you will be returned.(Qur'an 2:245)

Thursday, June 8, 2017

Qaswida ya Leo kutoka Sweden na mix ya Africa Kusini

Mashaallah! Africa is Beautiful! Alhamdulillah!

Maher has taken his music to another level.
The scenery is beautiful and the Zulu choir Amakhono We Sintu, added a nice touch to the song. Beautiful! Mashaallah!

Aya za Leo - Udanganyifu (Deception)



Na katika watu, wako wasemao: Tuna mwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, wala wao si wenye kuamini.Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.  Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo.

Na wanapo ambiwa: Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji.
Hakika wao ndio waharibifu, lakini hawatambui.

And of the people are some who say, "We believe in Allah and the Last Day," but they are not believers.They [think to] deceive Allah and those who believe, but they deceive not except themselves and perceive [it] not. In their hearts is a disease, so Allah has increased their disease; and for them is a painful punishment because they [habitually] used to lie.

And when it is said to them, "Do not cause corruption on the earth," they say, "We are but reformers."
Unquestionably, it is they who are the corrupters, but they perceive [it] not. (Qur'an 2:8-2:12)

Tuesday, June 6, 2017

Al Hikma Inawaletea Mashindano Ya Quran

Mwezi wa Qur'ani, jamani I love it, Quran competitions all over the place.
Jamani Hii siyo ya kukosa, sheikh Sudais in Dar? What a treat.
Mashindano ya Qur'an yatakuwa uwanja wa taifa, fanyeni muende, kiingilio ni bureee.
Ukitaka kumjua Sheikh Sudais, soma hii posta yangu ya nyuma ya msomi wa leo.
Alafu msisahau kwenda na ya diamond jubilee hall pale kwenye mashindano madogo yake ya Qur'an ya bi Aisha Sururu foundation.

Monday, June 5, 2017

Aya ya Leo - Ukweli na Uongo (Truth and Lies)

Na Usichanganye Ukweli na Uongo au kuficha ukweli wakati unaujua.  

And do not mix the truth with falsehood or conceal the truth while you know [it].
(Qur'an 2:42)

Friday, June 2, 2017

Aya ya Leo - Dua


Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu

Our Lord, and make us Muslims [in submission] to You and from our descendants a Muslim nation [in submission] to You. And show us our rites and accept our repentance. Indeed, You are the Accepting of repentance, the Merciful.
(Qur'an 2:128)
Jumaa Kareem!

Wednesday, May 31, 2017

1st Makkah Iftaar Ramadhan 1438 ~ Adhaan by Sheikh Fallaatah

Hadithi ya Leo - Qur'an (Al-Baqara na Al-Imran)




Abu Umama alisema alimsikia Mtume wa Allah (S.A.W) akisema:

Soma Qur'ani, kwani siku ya kiyama itakuja kama mwombezi kwa wale wanaoisoma. Some zile mbili zenye mwanga Al-Baqara na Surah Al Imran, kwani siku ya kiyama zitakuja kama mawingu mawili au vivuli viwili au makundi mawili ya ndege, kuwaombea wale waliokuwa wanazisoma. Soma Surah Al-Baqara, kwani kuikimbilia ni baraka na kuikatia tamaa ni chanzo cha huzuni, na waganga hawawezi kukabiliana nayo.

Abu Umama said he heard Allah's Messenger (S.A.W) say:

Recite the Qur'an, for on the Day of Resurrection it will come as an intercessor for those who recite It. Recite the two bright ones, Al-Baqara and Surah Al 'Imran, for on the Day of Resurrection they will come as two clouds or two shades, or two flocks of birds in ranks, pleading for those who recite them. Recite Surah al-Baqara, for to take recourse to it is a blessing and to give it up is a cause of grief, and the magicians cannot confront it. (Mu'awiya said: It has been conveyed to me that here Batala means magicians.)
(~Muslim Book 6, Hadith 302)

Friday, May 26, 2017

Vitu vitano vitakavyo kufanikishia Funga Yako (Ramadhan Tips)

1. Usile chakula kingi. (Gawa utombo sehemu tatu. 1/3 Maji, 1/3 Chakula, 1/3 ya kuhema)
2. Toa Sadaka kila siku kidogo kidogo. Ata ile kufuturisha kila siku pia ni sadaka.
3. Sali sala tano kila siku. Sala 5 zimelazimishwa na zina uzitu kuliko Salaa ya taraweeh ambayo ni sunna.
4. Soma Qur'an kwa utaratibu ili uweze kuilewa.
5.Kuwa na uamko wa Allah (Mcha Mungu). Hii itakusaidia usitende madhambi, kwa kuichunga nafsi yako na maovu.

Ramadhan Kareem Everybody! You got this.

Bosnia 1992: The Omarska Camp - Al Jazeera World

As we start this Ramadhan, let us remember our brothers and sisters that were massacred in the Omarska concentration camp in Bosnia. 
May Allah grant them eternal peace and elevate them to the highest of his heavens. 

Tuesday, May 23, 2017

Africa Uncovered - Mauritania: Fat or Fiction - 11 Aug 08 - Part 2

Well if they knew about processed foods, they wouldn't need to force feed anybody, the fat will come naturally. Okay jokes aside, real issues happening today, get educated.

Friday, March 24, 2017

Fish with Artistic Skills!

And here we thought the human beings are the only artistic beings on earth. How little do we know of God's creation. 

Jumaa Mubarak!

Friday, March 17, 2017

Aya ya Leo Mzigo(Burden)


Na mbebaji mzigo hata beba mzigo wa mwingine. Na aliye zidiwa na mzigo wake aki muomba mwingine amsaidie, hauto punguzwa, ata kama ni ndugu yake wa karibu. Unaweza kuwaonya wale wanao mcha Mola wao Mlezi kwa ghaibu na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu. 

And no bearer of burdens will bear the burden of another. And if a heavily laden soul calls [another] to [carry some of] its load, nothing of it will be carried, even if he should be a close relative. You can only warn those who fear their Lord unseen and have established prayer. And whoever purifies himself only purifies himself for [the benefit of] his soul. And to Allah is the [final] destination. (Qur'an 35:18)


Jumaa Mubarak!


Thursday, March 16, 2017