Translate

Monday, June 29, 2015

Vitu 8 vya kukusaidia kupata chooKuna kuwaga na malalamiko mengi mwezi Ramadhani kutoka kwa watu kuwa hawapati choo. Misemo kama, yaani siku ya nne leo sijapata choo, ni kawaida mno, na ata ukipata ni magumu mno. Wengine hulaumi kwasababu ya kushinda na njaa siku nzima, wengine hutumia hicho kama kisingizio cha kuto kufunga kabisa. Basi isiwe tabu, post ya leo nawapa vitu 8 vya kukusaidia upate choo laini.

1. Maji
Kama ile picha ya juu inavyo elezea, choo kigumu kinatokana na kutokua na maji ya kutosha ili choo kilainike. Time ya kufungua, piga glass zako mbili  za haraka, alafu kunywa maji usiku mpaka ufikishe angalau lita mbili au glasi nane.

2. Matundaa

Matunda yana Fiber ambayo, yenyewe haina virutubisho, lakini kazi yake maalum ni kusukuma chakula tumboni ili kiweze kutoka haraka. Ni vizuri ukiyala kwenye tumbo ambalo halina chakula, yaani kula matunda kwanza kabla ya mlo mwingine. Alafu subiri kidogo kwa muda wa kama lisaa hivi ili chakula kisagike. Kuna Sababu Mtume alikuwa anafungua na Tende na Maji jamani, sio mkate na asali, formula tunayo ni juu yetu kuitumia sawa.
3. Mboga
Mboga za aina yote, ni nzuri kwasababu kama matunda, zina fiber nyingi. Kama kwenu watu hawapendi mboga za majani, then zidisha kachumbari ui serve kama side dish na yenyewe. Biringanya, bamia na kadhalika, ata viazi pia ni mboga.

4.Kunde
Maharage, Njegere, choroko, dengu na kadhalika. Kiufupi kunde za aina yote, hakikisha futari yako haikosi aina moja hapo juu. Nazo zina fiber nyingi mno, na mambo yako yatakuwa swafi.

5.Maziwa ya Mgando
Si kama ice cream hiyo jamani. Maziwa mgando yana vijidudu vizuri ambayo digestive system yetu inahitaji kutusaidia kusaga chakula. Hii pia ule kwenye tumbo ambalo halina chakula, vizuri kufungulia nayo pia.

6. Zoezi
Mazoezi husaidia kuamsha mwili mzima ikiwemo na utumbo wako. Fanya mazoezi pia kwa afya yako.

7. Mafuta ya Zeituni
Kama umefanya 1-6 na vikagoma, basi kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Zeituni, na kijiko kimoja cha ndimu kwenye tumbo tupu.

8. Castor Oil
Hii ni kiboko inasafisha utumbo mzima. Kunywa kijiko kimoja cha chai kwenye tumbo tupu. Mama yangu aliniambia ndio dawa waliyokuwa wanapewa na wazazi wao kusafisha tumbo. Sema hakikisha unanua ambayo ni asilimia 100 castor oil, na cold pressed(mafuta mabichi) ndio mazuri zaidi. Zina patikana kwenye maduka ya dawa.

Zipe muda hizi nilizoziweka hapo juu kufanya kazi, yaani usitegemea utapata choo baada ya lisaa limoja, labda kesho yake, kua mwenye subira kidogo. Kama siku ya pili baada ya kujaribu ya hapo juu mambo bado, basi nenda duka la dawa upate dawa kali zaidi ya kukusadia.

 Swaumu Njema jamani!

No comments:

Post a Comment