Translate

Monday, June 22, 2015

Aya za Leo - The Story of Ibrahim Part 2(The Dialogue)



(Qur'an 26:69-104)
Na Wasomee habari za Ibrahimu. 
Alipomwambia baba yake na kaumu yake, "mnaabudu nini?"
Wakasema, "Tunaabudu masanamu, daima tunawaabudu."
Akasema, "Je, yanakusikieni mnapoyaita? Au yanakufaeni (mkiyaabudu) au yanakudhuruni (Mkiacha kuyaabudu)?
Wakasema, "Hayafanyi haya lakini tumewakuta baba zetu wakifanya hivi."
Akasema, "Je, mumewaona hawa mnaowaabudu nyinyi na wazee wenu waliotangulia? Bila shaka hao ni adui zangu ila Mola wa walimwengu wote, ambaye ameniumba na yeye ndio ananiongoza. Na ambaye ndiye anayenilisha na kuninywesha. Na ninapougua, yeye ndiye anayeniponesha. Na ambaye atanifisha kisha atanihuisha.Na ndiye ninayemtumaini kwamba atanisamehe makosa yangu siku ya malipo.

Mola wangu! nipe hukumu na uniunge pamoja na watendao mema. Na unijaalie katika warithi wa mabustani ya neema. Na umsamehe baba yangu, bila shaka yeye ni miongoni mwa waliopotea. Wala usinifedheheshe siku watakayofufuliwa, siku ambayo hayatafaa mali wala watoto.

Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo safi, na pepo itasogezwa kwa wacha Mungu, na Jahanamu itadhihirishwa kwa wapotofu.

Na wataambiwa, "wapo wapi mliokuwa mkiwaabudu? Badala ya Mwenyezi Mungu! Je, wanaweza kukusaidieni au kujisaidia wenyewe? Basi watatupwa humo wao na maasi, na majeshi ya Ibilisi yote. Watasema, 'na hali ya kuwa wanagombana humo, 'Wallahi, kwa yakini tulikuwa katika upotofu ulio dhahiri. Tulipokuwa tukikufanyeni sawa na Mola wa walimwengu wote.'

Na hawatakupoteza ila wale waovu.
 'Basi hatuna waombezi wala rafiki halisi. Laiti kama tungelikuwa na marejeo tungekuwa waumini.'"

Bila shaka pana katika haya mazingatio, lakini wengi katika wao si wenye kuamini. Na kwa yakini Mola wako ndiye Mwenye nguvu, Mwenye rehema.

No comments:

Post a Comment