Translate

Friday, June 26, 2015

Aya za Leo - Hadithi ya Lut (The Story of Lut)

Lut'i akamuamini, na akasema: Mimi nahamia kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.Na pale Lut'i alipo waambia watu wake: Hakika nyinyi mnafanya uchafu, ambao hapana mmoja katika walimwengu aliye kutangulieni kwa hayo.
Je! Nyinyi mnawaingilia wanaume, na mnaikata njia? Na katika mikutano yenu mnafanya maovu? Basi haikuwa jawabu ya watu wake isipo kuwa kusema: Tuletee hiyo adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa wewe ni katika wasemao kweli.Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ninusuru na watu mafisadi hawa! Na wajumbe wetu walipo mjia Ibrahim na bishara, walisema: Hakika sisi hapana shaka tutawahiliki watu wa mji huu, kwani watu wake hakika wamekuwa madhaalimu.Akasema: Hakika humo yumo Lut'i. Wao wakasema: Sisi tunajua zaidi nani yumo humo. Hapana shaka tutamwokoa yeye na ahali zake, isipo kuwa mkewe aliye miongoni mwa watao kaa nyuma. Na wajumbe wetu walipo mfikia Lut'i, alihuzunika kwa ajili yao, na moyo uliona dhiki kwa ajili yao. Wakasema: Usiogope, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, ila mkeo aliye miongoni mwa watao kaa nyuma.Kwa yakini sisi tutawateremshia watu wa mji huu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya uchafu wanao ufanya.Na tumeacha katika mji huo Ishara ilio wazi kwa watu wanao tumia akili zao.

But Lut had faith in Him: He said: "I will leave home for the sake of my Lord: for He is Exalted in Might, and Wise." And (remember) Lut: behold, he said to his people: "Ye do commit lewdness, such as no people in Creation (ever) committed before you.
"Do ye indeed approach men, and cut off the highway?- and practise wickedness (even) in your councils?" But his people gave no answer but this: they said: "Bring us the Wrath of Allah if thou tellest the truth."He said: "O my Lord! help Thou me against people who do mischief!"When Our Messengers came to Abraham with the good news(his wife getting a baby), they said: "We are indeed going to destroy the people of this township: for truly they are (addicted to) crime." He said: "But there is Lut there." They said: "Well do we know who is there : we will certainly save him and his following,- except his wife: she is of those who lag behind!".And when Our Messengers came to Lut, he was grieved on their account, and felt himself powerless (to protect) them: but they said: "Fear thou not, nor grieve: we are (here) to save thee and thy following, except thy wife: she is of those who lag behind."For we are going to bring down on the people of this township a Punishment from heaven, because they have been wickedly rebellious."And We have left thereof an evident Sign, for any people who (care to) understand.
(Qur'an 29:26,28-35)
Ijumaa Njema Wadau!



No comments:

Post a Comment