Translate

Tuesday, July 1, 2014

Chakula Bora cha Leo - Kachumbariiiiiiiii

Kachumbari ni moja ya ile chakula ambayo ni nyongeza fulani hivi, kikiwepo chakula kinazidi kuwa kitamu, kisipo kuwepo ni sawa pia. Lakini je unaijua thamani yake? Tuanze na kuangalia mboga zinazo patikana kwenye kachumbari.

Kitunguu
1. Ina phytochemical, ambayo husaidia Vitamin C kwenye mwili wako kufanya kazi.
2.Ina Chromium ambayo husaidi kusawazisha sukari kwenye damu.
3.Husaidia utengenzaji wa cholesterol nzuri mwilini.
4. Husaidia na kuzuia Kansa (Saratani).
5. Ni Dawa ya kungatwa na nyuki.







Nyanya
1. Vitamini A, C, folate na Potassium, vitamin B6, magnesium, phosphorus na copper.
2. Husaidia Blood pressure na ugonjwa wa moyo.
3.Ina Beta-Carotene ambayo husaidia kuimarisha ngozi na kupunguza ngozi kujikunja.
4.Ina Vitamin K ambayo husaidi kuimarisha mifupa.




Karoti
1. Ina Beta-Carotene ambayo hubadilika kwenye ini kuwa Vitamin A.Hii huboresha macho kusaidia kuona vizuri zaidi.
2. Husaidia kuzuia Kansa ya maziwa, mapafu na utumbo.
3. Husaidia kupunguza uzee.
4. Huimarisha ngozi yako na kuifanya ingare.
5. Hupunguza magonjwa ya moyo
6.Husaidia ini kutoa sumu kwenye mwili.








Pilipili Hoho
1. Ina Vitamin C ambayo husaidia kuupa mwili nguvu ya kujikinga.
2. Ina Beta-Carotene
3.Ina punguza Cholestral mbaya na inasaidia na kisukari.
4. Husaidia kupigana na Kansa.
5. Ina Vitamin E ambayo husaidia kuimarisha ngozi na nywele.
6. Ina Vitamin B6 ambayo husaidia kutengenza viini(cells) za mwili.
7. Hulinda macho kwa kupigana na Cataracts, ambavyo ni viini vinavyo ota machoni.

Matango

1. Husaidia na kiungulia
2. Husaidi kuondoa mawe kwenye figo
3. Inakupa nguvu kwenye mwili wa kujikinga.
4. Huzuia saratani
5.  Husaidia na blood pressure
6. Husaidia na magonjwa ya finzi
7. Huimarisha ngozi na nywele
8. Hupunguza maumivu ya viungo na misuli
9. Husaidia maini
10. Husaidia watu wenye kisukari kutengeneza insulin.
Ndimu na Limao
1. Husaidia na kutibu Mafua
2. Husaidia ini kutoa sumu mwilini.
3. Husaidia kutoa choo
4. Husaidia kuyeyusha mawe kwenye figo.
5. Husaidia kupigana na uzee.
6. Huuwa minyoo mwilini
7. Husaidia kuua vidudu vya Malaria, Kipindupindu, typhoid na magonjwa mingine
8. Hujenga na kuimarisha mishipa ya damu
9. Hupigana na Kansa







Giligilani
1. Huuwa vidudu vya salmonella, ambavyo husababisha sumu ya chakula(Food poison).
2. Hupigana na viini vya Saratani
3. Ni dawa ya fungus, bacteria na yeast infection
4. Ina Omega 3 na Omega 6 ambayo husaidia kulinda mwili.
5. Husaidia kuendesha sukari mwilini.
6. Ina Calcium ambayo husaidia kujenga mifupa
7. Hupunguza cholesterol mbaya mwilini.
8. Hupunguza Mercury, Lead na aluminium mwilini.
9. Huupa mwili nguvu uweze kujilinda
10. Husadia kulala kwa wale wasio weza kulala
11. Husaidia kutoa mawe kwenye figo.

Haya Jamani, habari ndio hiyo. Tuwache kuifanya kachumbari kama ni sunna ya mlo, bali tuanze kuifanya ni moja ya mboga za kila siku, kwani ni dawa ya mwili. Tujitahidi kuiweka kwenye kila mlo, na ikiwazekana robo au nusu ya sahani yako iwe ni kachumbari. Haya basi InShaa'llah, futari zetu kuanzia leo moja ya mboga ni Kachumbari.

Futari njema wadau!

No comments:

Post a Comment