Translate

Thursday, April 30, 2015

Msomi wa Leo - Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani (1919 - 2006)

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani, ni mshairi, msomi wa dini na mwanasiasi. Sheikh alizaliwa Stone town,Zanzibar tarehe 13 January 1919. Alifundishwa dini na baba yake Sheikh Muhsin bin Ali (1878-1953) na wanazuoni wengine wa Afrika ya Mashariki.

Sheikh alivyo maliza sekondari akiwa na miaka 18, aliendelea na elimu ya dunia kwenye Chuo Kikuu cha Makerere Uganda na kusomea ukulima.

Mwaka 1942 Sheikh aliajiriwa na serikali kama afisa msaidizi wa kilimo mwangapani.  Mwaka 1947 Sheikh aliacha kazi ya serikali na akawa Mhariri Mkuu wa gazeti la Mwongozi kwa muda wa miaka kumi na tano.  Mwongozi lilikuwa ni gazeti la siasa, la ijtimaa na la dini. Na lilikuwa maarufu kwa kazi yake kubwa ya kudai haki za wananchi na kutapakaza misingi ya Kiislamu huko Zanzibar na sehemu mbali mbali za Afrika ya Mashariki.

Sheikh Al-Barwani alijiunga na chama cha Zanzibar Nationalist Party na alifanya juhudi nyingi ili  Zanzibar ipate Uhuru kutoka kwa Muingereza. Hapo alikuwa maarufu kwa jina la "Zaim" yaani Mwongozi. Mwaka 1961 Sheikh alichaguliwa kuwa Waziri wa Elimu na Waziri wa Mambo ya Ndani, kisha akawa Naibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje katika serekali ya kidemokrasia ya Zanzibar. Wakati wa Uongozi wake, alikuwa katika harakati za kuondoa ubaguzi zenj, na aka hamasisha uchaguzi wa kura na aka hakikisha walimu wanapewa likizo ya uzazi na kulipwa.

Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Sheikh aliwekwa jela kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bila ya mashtaka, kwa sababu ya fikra zake za kisiasa.Alivyo achiwa, alihamia Kenya, alafu akaenda Misri, baada ya muda akarudi Kenya na mwisho yeye na familia yake wakahamia Dubai.  Mwaka 1989 mke wake wa zaidi ya miaka 25 alifariki dunia.
 

Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ameandika vitabu vingi vya dini, lakini anajulikana kwa kazi yake kubwa ya kutafsiri Qur'an kwa kiswahili cha ki unguja, pamoja na kitabu chake cha utenzi cha mashairi ya Kiswahili wa beti 1300 juu ya maisha ya Mtume (s.a.w.).

Sheikh Alifariki dunia tarehe 20 March mwaka 2006 akiwa na miaka 86, Mji wa Muscat, Oman. 
Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake, amwekee Nuru kwenye Kaburi lake na ampokee Kwenye Pepo yake. 

Read his story in English here>>> 

No comments:

Post a Comment