Translate

Friday, January 25, 2013

Happy Birthday Prophet Mohammed (S.A.W) 2013

Maulid Celebration for the birth of Prophet Mohamed(S.A.W) that occurred in Zanzibar, Tanzania. I nabbed this from matukio-michuzi. Enjoy!

  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.
[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia ubani kama ishara ya ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Mtafsiri Lugha kwa njia ya alama akitoa tafsiri ya maneno yanayozungumzwa wakati wa Hafla ya sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Wake za Viongozi na Akinamama wakisikiliza Maulid Barzanj ya Kuzaliwa kwa yaliyosomwa na wasomaji mbali mbali na Qasida katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.

Ustadh Ali Twalib Mohamed,wa Kibanda Hatari Mjini Zanzibar akisoma Maulid Barzanj Mlango wa kwanza katika kusherehekea kwa kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Kwa Habari zaidi ingia hapa Matukio-michuzi 

And this is how folks in Zanzibar Celebrated the Birth of Prophet Mohammed(S.A.W). 


No comments:

Post a Comment