Pages

Wednesday, July 30, 2014

Hadithi ya Leo - Kufunga Sita baada ya Ramadhani

Abu Ayub alihadithia kwamba:
Mtume wa Allah alisema:" Yeyote anayefunga Ramadhani, alafu akaendelezea na siku sita za mwezi wa Shawwal, basi ni sawa na kufunga kila siku.


Abu Ayub narrated that :
the Messenger of Allah said: "Whoever fasts Ramadan, then follows it with six from Shawwal, then that is (equal in reward) to fasting everyday." (Tirmidhi 759)

Eid Mubarak kutoka Tanzania!

Arusha
Salaam za Eid kutoka kwa mdau wangu wa Arusha

Mdau wangu mwingine anasema walifungua vinywa....
wakamalizia na biriani


Picha zote hapo chini zinazofuata nimezitoa kwa michuzi media
Iringa

Zanzibar



Dar-Es-Salaam



Monday, July 28, 2014

Sunday, July 27, 2014

Eid Mubarak!

Saudi has announced Eid to be on Monday July 28th, so Eid Mubarak to them and all countries following them as well as countries that follow the Fiqh Council of North America/Islamic Society of North America, the European Council for Fatwa and Research , the Federation of Islamic Association of New Zealand and Jamiatal Ulama in South Africa.

For those countries following local sighting, Eid will be on Tuesday July 29th, so Eid Mubarak to you guys as well. 

A note from Moonsighting.com
Sunday, 27 July 2014:
    Moon is not expected to be seen in almost the whole world except with difficulty in South America, and with ease in Polynesian Islands, where there are not many Muslims reporting moonsighting. There is a small possibility in South Africa but only experienced observers may see it. 
    Mwezi hautegemewi kuonekana karibia dunia nzima, kasoro kwa shida South America, na kwa urahisi visiwa vya Polynesian, ambapo hamna waislamu wengi wakutoa repoti kwa moonsighting. Kuna uwezekano mdogo wa kuuona mwezi Afrika kusini, lakini na watu wenye ujuzi na uzoefu kwa kutafuta mwezi.

Air Algerie Plane Crash Flight AH5017 Crashes | Missing Plane with 116 A...


Inna lillahi waina illahi rajiun.
To God we belong and to him is our return.
May Allah accept the souls of the departed to his heaven and may he give peace to their remaining families.

Saturday, July 26, 2014

It's Official - We are starting our Eid Countdown......

What better way to launch this countdown then a past Eid Event of muslims flooding the streets of Moscow to kick off the Eid celebration with the morning Eid prayer.

God is truly great!
I think its apparent, Moscow needs more mosques.

Friday, July 25, 2014

Aya za Leo - Wana Wawili wa Adamu(The two Son's of Adam)

Na wasomee habari ya wana wawili wa Adam kwa ukweli. Walipo toa sadaka, ukakubaliwa wa mmoja wao, na wa mwengine haukukubaliwa. [Moja]Akasema: "Nitakuuwa". Akasema mwengine: "Mwenyezi Mungu huwapokelea wachamngu,ukininyooshea mkono wako kuniuwa, mimi sitakunyooshea mkono wangu kukuuwa. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote.Mimi nataka ubebe dhambi zangu na dhambi zako, kwani wewe utakuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Na hayo ndiyo malipo ya wenye kudhulumu". Basi nafsi yake ikampelekea kumuuwa nduguye, akamuuwa na akawa miongoni mwa wenye hasara. Hapo Mwenyezi Mungu akamleta kunguru anaye fukua katika ardhi ili amwonyeshe vipi kumsitiri nduguye. Akasema: Ole wangu! Nimeshindwa kuwa kama kunguru huyu nikamsitiri ndugu yangu? Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta.


And recite to them the story of Adam's two sons, in truth, when they both offered a sacrifice [to Allah ], and it was accepted from one of them but was not accepted from the other. Said [the latter], "I will surely kill you." Said [the former], "Indeed, Allah only accepts from the righteous [who fear Him]. If you should raise your hand against me to kill me - I shall not raise my hand against you to kill you. Indeed, I fear Allah , Lord of the worlds.Indeed I want you to obtain [thereby] my sin and your sin so you will be among the companions of the Fire. And that is the recompense of wrongdoers."And his soul permitted to him the murder of his brother, so he killed him and became among the losers.Then Allah sent a crow searching in the ground to show him how to hide the disgrace of his brother. He said, "O woe to me! Have I failed to be like this crow and hide the body of my brother?" And he became of the regretful.(Qur'an 5:27-31)

Thursday, July 24, 2014

Chakula Bora cha Leo - Tikiti Maji

 Haya Ramadhani ndo hiyo inaishia ishia, tuangalie faida za kula Tikiti Maji.
1. Ina zuiwa Pumu - Ina asimilia kubwa ya Vitamin C
2. Ina punguza Blood Pressure
3. Ina zuia Saratani
4. Ina saidia kupata choo kizuri(Tena kwa ramadhani mambo si ndo hayo)
5. Ina kupatia maji ya kutosha ili mwili uweze kujiendesha vizuri zaidi.
6. Ina zuia uvimbe wa mwili - Ina Choline ambayo husaidia mwili kulala, misuli, kujifunza na kuwa na kumbukumbu nzuri.
7. Huzuia Maumivu ya Misuli - Ina L-citrulline ambayo husaidia na kupunguza maumivu ya Misuli.
8. Ngozi nzuri - Ina Vitamin A ambayo inasaidi kuimarisha ngozi na nywele.


Aya ya Leo- Usiku wa Nguvu(Laylatul Qadri)

Usiku wa Nguvu ni bora kuliko miezi elfu.

The Night of Power is better
 than a thousand months.(Qur'an 97:3)

Read an earlier post that I talked about The night of power, here...>>>

Wednesday, July 23, 2014

Msomi wa Leo - Sh. Mishary bin Rashid Al-afasi


Amezaliwa September 5 mwaka 1976 Kuwait. Sh.Al-Afasi ana shahada kutoka chuo kikuu cha Madina, na utaalamu wake ulikuwa kwenye aina 10 za kusoma Qur'ani na tafsiri zake.  Alisha soma Qur'ani mbele ya wasoma Qur'ani wakubwa kama Sheikh Ahmed Abdulaziz Al-Zaiat, Sheikh Ibrahim Ali Shahata Al-Samanodei na Sheikh Abdurarea Radwan.Sheikh ana mke na watoto wawili wa kike.

Sheikh ameshaswalisha Taraweh Islamic Center ya Irvine California Marekani.  Sheikh anaonekana kwenye channel mbili za dini, ambayo moja ni Alafasy TV. Sasa hivi Sheikh ni Imam wa Msikiti wa Al-Kabir(Msikiti Mkuu) uliokuwa mji wa Kuwait, na huswalisha Taraweh mwezi wa Ramadhani. Sheikh pia ni msoma mashairi au tuseme muimba Qaswida, na Qaswida yake moja nilishaipostigi hapa ...>>>


Msikilize Sheikh hapo chini anavyo kusomea Sura Yasin.

Mashallah! Mwenyezi Mungu amzidishie Elimu ya Dini na Dunia.


Tuesday, July 22, 2014

Qiyamul Layl (the night prayer) AKA Taraweh during Ramadhan

Sheikh Muhammad Al-Mukhtar Ash-Shinqitee: Qiyamul Layl (the night prayer)

Aya ya Leo - Mzigo


Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine. Na aliye zidiwa na mzigo wake akiomba uchukuliwe hautachukuliwa hata kidogo, hata kama ni ndugu yake wa karibu. Hakika wewe unawaonya wale wanao muogopa Mola wao bila kumuona, na wanashika Sala. Na anaye jitakasa, basi anajitakasa kwa ajili ya nafsi yake. Na marejeo ni kwa Mwenyezi Mungu.

And no bearer of burdens will bear the burden of another. And if a heavily laden soul calls [another] to [carry some of] its load, nothing of it will be carried, even if he should be a close relative. You can only warn those who fear their Lord unseen and have established prayer. And whoever purifies himself only purifies himself for [the benefit of] his soul. And to Allah is the [final] destination. 

Monday, July 21, 2014

Hadithi ya Leo - Destiny

 
Kwa mamlaka ya Abu Abbas Abdullah bin Abbas(Mwenyezi Mungu aridhike nae) Alisema:
 
Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume(S.A.W) kanipakia kwenye ngamia wake, akaniambia, "kijana, nitakupa ushauri: Mkumbuke Allah na Allah atakulinda. Mkumbuke Allah na utamkuta mbele yako. Ukiomba, basi muombe Allah pekee, na tafuta msaada, basi tafuta msaada kutoka kwa Allah. Na jua taifa zima liki kusanyika kukusaidia na chochote, hawatukasaidia ila Allah alichokupangia. Na wakikusanyika kukudhuru na chochote, hawata kudhuru ila Allah alichokupangia. Wino umesha inuliwa, na karatasi zimesha kauka.
 
 
On the authority of Abu Abbas Abdullah bin Abbas (may Allah be pleased with him) who said:

One day I was behind the Prophet (peace and blessings of Allah be upon him) [riding on the same mount] and he said, “O young man, I shall teach you some words [of advice]: Be mindful of Allah and Allah will protect you. Be mindful of Allah and you will find Him in front of you. If you ask, then ask Allah [alone]; and if you seek help, then seek help from Allah [alone]. And know that if the nation were to gather together to benefit you with anything, they would not benefit you except with what Allah had already prescribed for you. And if they were to gather together to harm you with anything, they would not harm you except with what Allah had already prescribed against you. The pens have been lifted and the pages have dried.” 

Bukhari - Hadith 19

Sunday, July 20, 2014

Malaysia Airlines Flight MH 17 Crash: Who Shot Down Malaysian Plane Airl...


This is absolutely sad news! A tragic accident at best. The question still remains, why clear a plane for landing in an active war zone? Inge kuwa Africa, ungesikia ndege zime simamishwa, heck, ndege nzima ina geuzwa kwa uwoga tu, majirani zetu Kenya can attest to that. Lakini, ulaya, vita vinaendelea, bado ndege zinaruka tu bila tatizo. Anywho, kila mtu ana makosa kwenye hili Janga.
Inna lillahi waina illahi rajiun!
To God we belong and to him is our return.
May Allah rest the souls of the departed, and grant peace to their families.

Saturday, July 19, 2014

Fungo Kumi la Mwisho la Ramadhani

Alhamdulillah! tumefika fungo kumi la mwisho, na sasa countdown yenyewe ndo inaanza. Ni wakati huu watu wengi hua swaum ina leta shida kidogo, ukali unazidi, na siku zinaonekana ndefu zaidi. Lakini hizi siku kumi za mwisho ni za kuomba Allah akukinge na Moto wa Jahanamu. Usiku wa laylatul kadri, usiku wa nguvu ambaye Jibril mwenyewe anashuka na Malaika wengine kwa ruhsa ya mwenyezi mungu duniani, na wote tunajua Jibril ni mkubwa wa Malaika. Kwahiyo tuzidishe ibada, tujitahidi kufanya itkaf (kufanya ibada usiku)misikitini kama utaweza, na tujitahidi kutoa sadaka sana.

Usiku wa Laylatul Kadri uta angukia kati ya Ramadhani 21,23,25 au 27, ambazo ni usiku wa Julai 18,20,22,24 na 26. In'shaa'llah, Allah atatusamehe madhambi yetu na atajibu maombi yetu.

Qaswida kutoka Kuwait Leo- Othman al Rashidi


Born in Kuwait in 1989 
Student at the college of Education - Kuwait University

Aya ya Leo - Miili Miwili ya Maji

  Na miili miwili ya maji hayafanani. Moja ni matamu yenye ladha, mazuri kunywa. Na nyingine ni ya chumvi, machungu. Na kutoka kila moja mnakula nyama laini (isiyo chacha). Na mnatoa mapambo mnayo yavaa. Na unaona ndani yake meli zinapita, ili mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.

And not alike are the two bodies of water. One is fresh and sweet, palatable for drinking, and one is salty and bitter. And from each you eat tender meat and extract ornaments which you wear, and you see the ships plowing through [them] that you might seek of His bounty; and perhaps you will be grateful. (Qur'an 35:12)

الحرم المكي- Live Video Stream from Makkah

Haya Jamani live video stream kutoka Makka, kumbukeni hatujapishana masaa na makka, sema maghrib yao ni saa moja na isha ni saa tatu. Kwahiyo wadau taraweh live hapo.

Thursday, July 17, 2014

Aya ya Leo - Allah


Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi, aliyewafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa, mbili mbili na tatu tatu, na nne-nne. Huzidisha katika kuumba apendavyo. Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.

Praise be to Allah, Who created (out of nothing) the heavens and the earth, Who made the angels, messengers with wings,- two, or three, or four (pairs): He adds to Creation as He pleases: for Allah has power over all things.(Qur'an 35:11)

Wednesday, July 16, 2014

Aya ya Leo - Hadithi(The Stories)


Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.

Truly Pharaoh elated himself in the land and broke up its people into sections, depressing a small group among them: their sons he slew, but he kept alive their females: for he was indeed a maker of mischief. [Quran 28:4]

Monday, July 14, 2014

Hadithi ya Leo - Hasira


Kwa mamlaka ya Abu Huraira( Allah aridhike nae):
Mtu alimwambia Mtume(S.A.W), "nishauri", Mtume akamwambia, "Usiwe na Hasira", yule mtu akarudia ombi lake mara kadhaa, na kila mara Mtume alimjibu, "Usiwe na Hasira".

 
On the authority of Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him):
A man said to the Prophet (peace and blessings of Allah be upon him), “Counsel me,” so he (peace and blessings of Allah be upon him) said, “Do not become angry.” The man repeated [his request for counsel] several times, and [each time] he (peace and blessings of Allah be upon him) said, “Do not become angry.” 

Bukhari - Hadithi 16





Sunday, July 13, 2014

Msomi wa Leo - Sheikh Syed Muhammad Naquib Al-Attas

Sheikh Al-Attas amezaliwa Septemba 5 mwaka 1931, Bogor, Java(Indonesia). Ni Msomi wa dini wa kisasa, ambaye utaalamu wake upo kwenye sayansi ya kiislamu, na jinsi ya kuitumia kwenye maisha ya sasa. Nia yake ni moja, Kusilimisha akili, mwili, nafsi na jinsi inavyo tuendesha kwenye maisha yetu na waislamu wote na wasio waislamu. Ni mwandishi wa vitabu 27 kwenye topic tofauti ya uislamu na maendeleo ya watu.

Alimaliza shule ya sekondari mwaka 1951, na kuingia jeshi Malaysia ambapo alichaguliwa kusoma Eaton Hall, Chester Uingezera, na baadae alisoma the Royal Military Academy, Sandhurst, Uingereza mpaka alipomaliza mwaka 1955. Alipata fursa ya kusafiri kwenda Spain, na Afrika ya kaskazini, akawa bado anahamu ya kujielimisha zaidi kidini, ndo alipo acha kazi yake, na kurudi kusoma chuo kikuu cha Malaya Singapore mwaka 1957-1959. 

Alipokuwa shule aliandika thesis, iliyomfanya apate fellowship kwenye Chuo Kikuu cha McGill, Montreal Canada. Alipata Shahada yake ya pili kwenye masomo ya filosofia ya kiislamu mwaka 1962. Alipomaliza hapo, akaenda kusoma Uingereza kwenye Chuo kikuuu cha London na kuchukua shahada yake ya tatu kwenye College ya Oriental and African Studies. Mwaka 1965, alirudi Malaysia, na akawa Mkuu wa shule ya Fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Malay, Kuala Lumpur. Mwaka 1968-1970 alikuwa Dean wa Faculty of Arts. Alihamia National University of Malaysia, mwaka 1973, kama mkuu wa Idara ya Lugha ya Malay na Fasihi, baadae akawa Dean wa Faculty ya Arts. 1987 alianzisha the International Institute of Islamic Thought and Civilization, Kuala Lumpur Malaysia.

Sheikh pia ni mchoraji mzuri wa maandishi ya kiislamu, na kazi zake zime onyeshwa Tropen Museum, Amsterdam. Sheikh kashiba haswa kwenye masoma ya dini na dunia. Msikilize mwenyewe hapo chini anakuwa interviewed na sheikh Hamza Yusuf.


Masha'allah! Mwenyezi Mungu amzidishie Elimu ya Dunia na Akhera, na amfungulie milango yake ya kheri hapa duniani na Akhera.

Saturday, July 12, 2014

Mafutariiii!!!!

1. Raisi wa Zanzibar Dr.Shein afuturisha wananchi kaskazini Pemba.
Dr.Shein wa tatu kutoka kushoto.

Picha na Ramadhani Othman.
2. Maalim Seif afuturisha watendaji wa CUF Nyumbani kwake.

Picha na Salim Said

Friday, July 11, 2014

Mawaidha ya leo kutoka kwa Sh.Nassor Bachu

FAIDA ZA SWAUM SH NASSOR BACHU

Sheikh anakwambia wewe ukiwa kila siku unashiba tu utawezaje kumjua
mwenye njaa?
 Tukumbukeni nyumba ambazo majiko hayawashwi jamani.

Thursday, July 10, 2014

Chakula Bora cha Leo - Ndizi Mbivu


Ndizi kwa sisi wabongo, tunaweza kusema ni dessert. Si unajua hizi desturi za ma keki na cream for dessert, sio style yetu tumeletewa tu, sisi ni matunda kwa kwenda mbele.  Ndizi inafaida nyingi sana, nitajaribu kuzi orodhesha hapa.
1. Ina tryptophan ambayo hubadilika kuwa seratonin, hii husaidia kukuweka kwenye mood nzuri
2. Inazuia Misuli isiji kaze
3. Ina jenga mifupa.
4.Ina punguza uvimbe wa mwili na inakulinda na kisukari
5.Ina Iron ambayo hujenga damu
6.Ina Potassium ambayo hukulinda na stroke, magonjwa ya moyo, na blood pressure.
7. Inakusadia kulainisha choo
8. Ina saidia kusaga chakula mwilini.
9.Ina saidia na kiungulia na kupooza madonda ya tumbo
10. Ina ondoa homa mwilini

Pia ni nzuri kweli wakati wa kufungulia futari, kabla ya swalaa ya maghribi.
Kuna Sababu manyani wameweza kuishi miaka yote hiyo na hili tunda kama chakula chao cha kilasiku.

Futari Njema!

China bans Ramadhan fasting in Muslim province

Serikali ya China, imewapiga marufuku wanafunzi na wafanyakazi wa serikalini wa kiislamu kufunga mwezi wa Ramadhani kwenye mji wa Xinjiang. Xinjiang ni mji ambao una asilimia karibia 60 ya waislamu.Soma habari yote kutoka Associated Press hapo chini.

Watu wakisubiri time ya kufungua kwenye msikiti wa Niujie, Beijing.













BEIJING (AP) — Students and civil servants in China's Muslim northwest, where Beijing is enforcing a security crackdown following deadly unrest, have been ordered to avoid taking part in traditional fasting during the Islamic holy month of Ramadan.
Statements posted in the past several days on websites of schools, government agencies and local party organizations in the Xinjiang region said the ban was aimed at protecting students' wellbeing and preventing use of schools and government offices to promote religion. Statements on the websites of local party organizations said members of the officially atheist ruling party also should avoid fasting.
"No teacher can participate in religious activities, instill religious thoughts in students or coerce students into religious activities," said a statement on the website of the No. 3 Grade School in Ruoqiang County in Xinjiang. Read the rest of the article here...

Wednesday, July 9, 2014

Mashindano ya Qur'ani - Julai 13, 2014



Aisha Sururu Foundation inakukaribisheni kwenye mashindano ya Qur'ani.

Lini? Jumapili hii tarehe 13 Julai.
Wapi?  Diamond Jubilee Hall Upanga, Dar-Es-Salaam.
Muda? Saa tatu(9am) asubuhi .

Basi jitahidi kwenda kuwa support watoto kutoka madrasa tofauti, ili na wao wapate moyo jamani.

Aisha Sururu Foundation cordially invites you to attend the Qur'an competition.

When? This coming Sunday the 13th of July, 2014. 
Where? Diamond Jubilee Hall in Upanga, Dar-Es-Salaam.
Time?   9am. 
Come out and support the kids from different Madrasas competing at different levels!

For further Questions please call +255 715 279 274, +255 784 279 274

Tuesday, July 8, 2014

Aya ya Leo - Rehema

Leo tumemaliza fungo 10 la mwanzo wa Mwezi wa Ramadhani, ambazo ni siku za Rehema. Basi tumuombe mwenyezi Mungu atusamehe madhambi yetu na aya hiyo hapa kutoka kwenye Qur'ani.

"Waqul rabbiighfir war-ham waanta khayru Arrahimeen"

Sema: " Ewe Mola Wangu, nisamehe na unirehemu kwani wewe ni mwingi wa kutoa Rehema".

So say: "O my Lord! grant Thou forgiveness and mercy for Thou art the Best of those who show mercy!" (Qur'an 23:118)

Chakula Bora Cha Leo - Chachandu

picha nimeitoa blogu ya matukiodaima

Chachandu ni chakula ambacho hatukifikirii kama ni chakula bali ni nyongeza kwenye chakula ili ipate ladha zaidi. Kwa wale wanao ogopa pilipili, hii kitu hawaigusi, lakini pia unaweza kuitengeneza mwenyewe bila kuongezea pilipili, sema raha yake iwashe kidogo bwana. Haya tuangalia kwanini hichi chakula kiko kwenye orodha ya vyakula bora.

Chachandu ni mchanganyiko wa mboga kadhaa ambavyo ni dawa kwenye mwili. Hivyo vyakula ni kama ifuatavyo.

Nyanya, Kitunguu na Ndimu- Nilisha ongelea faida zao kwenye post ya kachumbari cheki hapa....

Kitunguu Swaumu

1. Husaidia watoto tumboni kuongeza uzito.
2.Huimarisha mwili kupigana na magonjwa yakifua na baridi
3. Ina Iodine ambayo husaidia kutibu goita(Hyperthyroid).
4.Ina Vitamin C ambayo hutibu Kiseyeye (Scurvy)
5. Ina punguza magonjwa ya moyo
6.Hutibu vidonda na fungus
7. Ina Vitamin B6 ambayo hujenga viini vya mwili
8. Ina saidia kuzuia Kansa
9. Husaidia kuendesha damu mwilini.

Pilipili Mbuzi
1. Ina sawazisha sukari mwilini
2. Ina pigana na vidudu vya saratani mwili
3. Ina zuia magonjwa ya moyo.
4. Ina zuia magonjwa ya viungo mwilini kama Arithritis.





Usiipike lakini chachandu yako, kwani ukiipika unaua viini vyake vyenye kusaidia kusaga chakula mwilini, na pia hupunguza nguvu yake mwilini. Tujitahidi kula chachandu jamani, ata ukiondoa pilipili bado unapata faida zake.

Futari Njema Wadau!




Monday, July 7, 2014

Hadithi ya Leo - Ukarimu


Kwa mamlaka ya Abu Hurairah( Allah aridhike nae), alihadithia Mtume wa Allah(S.A.W) alisema:
Yule mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho, aongee mazuri au anyamaze.Na yule mwenye kumuamini Allah na siku ya mwisho awe Mkarimu kwa majirani zake, na yule mwenye kumuamini Allah na siku ya Mwisho, awe Mkarimu kwa wageni wake.

On the authority of Abu Hurayrah (may Allah be pleased with him), that the Messenger of Allah (peace and blessings of Allah be upon him) said:

Let him who believes in Allah and the Last Day speak good, or keep silent; and let him who believes in Allah and the Last Day be generous to his neighbor; and let him who believes in Allah and the Last Day be generous to his guest.  

 Bukhari - Hadith 15






Sunday, July 6, 2014

Maji au MAJII?

Kama we si mpenzi wa maji, jaribi kuloweka matunda(ya pondeponde ndani ya jagi) na maji ya kunywa usiku kucha, utaacha kunya soda. Okay maybe not, but atleast utapunguza kunywa yale maji ya sukari yaliyojazwa gesi. Tujitahidi kunywa glasi 6-8 za maji kwa siku, kwani maji husaidia kuendesha mwili na pia itakusaidia kupungua.

Saturday, July 5, 2014

Nyumba za Udongo Palestina‏

Wa palestina kutokana na uhaba wa kupata Saruji na vifaa vya kujengea nyumba, ambazo wana zinunua kutoka Israel na nchi zingine za nje, wamechukua uamuzi wa kujenga nyumba za udongo. ShamsArd, Kampuni ya usanifu wa majengo palestina, ndo kampuni ya kwanza iliyochukua uamuzi wa kujenga hizi nyumba za udongo ili waweze kujitegemea wenyewe.  Nyumba hizi ni za bei ndogo, Hulinda mazingira, na pia kutokana na hali ya kivita ya hiyo sehemu ya west bank, kutwa nyumba zao hubomolewa. Gharama yake ya kuijenga tena nyumba kama hii ni ndogo ukilinganisha na nyumba ya saruji.

      Nyumba ya Ahmad Doud iliyokuwa mji wa Jericho, West Bank, Palestina.

In'Shaa'llah! wataweza kujitegemea na vitu vingine.


Friday, July 4, 2014

Aya ya Leo - Uwezo wa Nafsi

Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tuna maandishi yanayo onyesha ukweli. Nao hawatadhulumiwa.

On no soul do We place a burden greater than it can bear: before Us is a record which clearly shows the truth: they will never be wronged. [Quran Chapter 23 verse 62]

Thursday, July 3, 2014

Chakula Bora cha Leo - Parachichi

 Parachichi ni moja ya yale matunda ambayo unayapita sokoni bila hata kuyatupia jicho la pili, na roho wala haishtuki. Kwa maana nyingine, huna uzoefu nalo sana. Halina ladha yoyote, mara nyingi watu huongezea chumvi au sukari kuipa ladha fulani hivi. Lakini, Parachichi ni moja ya chakula bora duniani, ngoja tuangalie faida zake.

1. Husadia kuboresha Moyo.
2. Ina beta-sitosterol ambayo husaidia kupunguza cholesterol kwenye moyo.
3. Ina Potassium ambayo husaidia na blood pressure.
4. Ina Carotenoid lutein amabayo husaidia kuzuia cataract na magonjwa ya uzee ya macho.
5. Ina sawazisha sukari kwenye damu
6. Ina folate na folic acid ambayo husaidia kupigana na maradhi ya watoto kuzaliwa na vilema au kasoro za mwili, nzuri haswa kwa wale akina mama wajawazito.
7. Husaidia kulinda na stroke ya mwili
8. Huzuia kukua kwa viini vya saratani.
9. Husaidia kupunguza kuzeeka kwa mwili.
10. Husafisha tumbo ambacho ndo chanzo cha ulimi na mdomo kunuka.
11. Husaidia mwili kuvuta virutubisho vya chakula kwenye mwili vizuri.
12. Huboresha ngozi na kutibu magonjwa mengi ya ngozi.

Usijisahau lakini ukalila kwa wingi kwani lina nenepesha pia ukilila sana, lakini ukiweza kula nusu kwa siku si mbaya badala ya yale maandazi ya saa nne. Pia unaweza kulitupia kwenye kachumbari kama hivi, familia yako yote ikafaidika.
Au ukainyunyuzia chumvi na limao pia ni tamu, na tulishaona faida za limao posti ya nyuma. 

Futari Njema!


B6 and folic acid, which help regulate homocysteine levels. High level of homocysteine is associated with an increased risk of heart disease. Avocado also contains vitamin E, glutathione, and monounsaturated fat, which help in maintaining a healthy heart.
- See more at: http://www.undergroundhealth.com/15-amazing-health-benefits-of-eating-avocados/#sthash.Jr0CkxE8.dpuf
B6 and folic acid, which help regulate homocysteine levels. High level of homocysteine is associated with an increased risk of heart disease. Avocado also contains vitamin E, glutathione, and monounsaturated fat, which help in maintaining a healthy heart.
- See more at: http://www.undergroundhealth.com/15-amazing-health-benefits-of-eating-avocados/#sthash.Jr0CkxE8.dpuf

Wednesday, July 2, 2014

Hadithi ya Leo- Wema

Mtume(S.A.W) alisema; Hakuna kati yenu ni muaminifu wa kweli, mpaka ampendee ndugu yake anacho jipendea mwenyewe.

Prophet (peace and blessings of Allah be upon him) said:
None of you [truly] believes until he loves for his brother that which he loves for himself.  


Bukhari Hadith 13.


Tuesday, July 1, 2014

Chakula Bora cha Leo - Kachumbariiiiiiiii

Kachumbari ni moja ya ile chakula ambayo ni nyongeza fulani hivi, kikiwepo chakula kinazidi kuwa kitamu, kisipo kuwepo ni sawa pia. Lakini je unaijua thamani yake? Tuanze na kuangalia mboga zinazo patikana kwenye kachumbari.

Kitunguu
1. Ina phytochemical, ambayo husaidia Vitamin C kwenye mwili wako kufanya kazi.
2.Ina Chromium ambayo husaidi kusawazisha sukari kwenye damu.
3.Husaidia utengenzaji wa cholesterol nzuri mwilini.
4. Husaidia na kuzuia Kansa (Saratani).
5. Ni Dawa ya kungatwa na nyuki.







Nyanya
1. Vitamini A, C, folate na Potassium, vitamin B6, magnesium, phosphorus na copper.
2. Husaidia Blood pressure na ugonjwa wa moyo.
3.Ina Beta-Carotene ambayo husaidia kuimarisha ngozi na kupunguza ngozi kujikunja.
4.Ina Vitamin K ambayo husaidi kuimarisha mifupa.




Karoti
1. Ina Beta-Carotene ambayo hubadilika kwenye ini kuwa Vitamin A.Hii huboresha macho kusaidia kuona vizuri zaidi.
2. Husaidia kuzuia Kansa ya maziwa, mapafu na utumbo.
3. Husaidia kupunguza uzee.
4. Huimarisha ngozi yako na kuifanya ingare.
5. Hupunguza magonjwa ya moyo
6.Husaidia ini kutoa sumu kwenye mwili.








Pilipili Hoho
1. Ina Vitamin C ambayo husaidia kuupa mwili nguvu ya kujikinga.
2. Ina Beta-Carotene
3.Ina punguza Cholestral mbaya na inasaidia na kisukari.
4. Husaidia kupigana na Kansa.
5. Ina Vitamin E ambayo husaidia kuimarisha ngozi na nywele.
6. Ina Vitamin B6 ambayo husaidia kutengenza viini(cells) za mwili.
7. Hulinda macho kwa kupigana na Cataracts, ambavyo ni viini vinavyo ota machoni.

Matango

1. Husaidia na kiungulia
2. Husaidi kuondoa mawe kwenye figo
3. Inakupa nguvu kwenye mwili wa kujikinga.
4. Huzuia saratani
5.  Husaidia na blood pressure
6. Husaidia na magonjwa ya finzi
7. Huimarisha ngozi na nywele
8. Hupunguza maumivu ya viungo na misuli
9. Husaidia maini
10. Husaidia watu wenye kisukari kutengeneza insulin.
Ndimu na Limao
1. Husaidia na kutibu Mafua
2. Husaidia ini kutoa sumu mwilini.
3. Husaidia kutoa choo
4. Husaidia kuyeyusha mawe kwenye figo.
5. Husaidia kupigana na uzee.
6. Huuwa minyoo mwilini
7. Husaidia kuua vidudu vya Malaria, Kipindupindu, typhoid na magonjwa mingine
8. Hujenga na kuimarisha mishipa ya damu
9. Hupigana na Kansa







Giligilani
1. Huuwa vidudu vya salmonella, ambavyo husababisha sumu ya chakula(Food poison).
2. Hupigana na viini vya Saratani
3. Ni dawa ya fungus, bacteria na yeast infection
4. Ina Omega 3 na Omega 6 ambayo husaidia kulinda mwili.
5. Husaidia kuendesha sukari mwilini.
6. Ina Calcium ambayo husaidia kujenga mifupa
7. Hupunguza cholesterol mbaya mwilini.
8. Hupunguza Mercury, Lead na aluminium mwilini.
9. Huupa mwili nguvu uweze kujilinda
10. Husadia kulala kwa wale wasio weza kulala
11. Husaidia kutoa mawe kwenye figo.

Haya Jamani, habari ndio hiyo. Tuwache kuifanya kachumbari kama ni sunna ya mlo, bali tuanze kuifanya ni moja ya mboga za kila siku, kwani ni dawa ya mwili. Tujitahidi kuiweka kwenye kila mlo, na ikiwazekana robo au nusu ya sahani yako iwe ni kachumbari. Haya basi InShaa'llah, futari zetu kuanzia leo moja ya mboga ni Kachumbari.

Futari njema wadau!