Pages

Tuesday, July 8, 2014

Chakula Bora Cha Leo - Chachandu

picha nimeitoa blogu ya matukiodaima

Chachandu ni chakula ambacho hatukifikirii kama ni chakula bali ni nyongeza kwenye chakula ili ipate ladha zaidi. Kwa wale wanao ogopa pilipili, hii kitu hawaigusi, lakini pia unaweza kuitengeneza mwenyewe bila kuongezea pilipili, sema raha yake iwashe kidogo bwana. Haya tuangalia kwanini hichi chakula kiko kwenye orodha ya vyakula bora.

Chachandu ni mchanganyiko wa mboga kadhaa ambavyo ni dawa kwenye mwili. Hivyo vyakula ni kama ifuatavyo.

Nyanya, Kitunguu na Ndimu- Nilisha ongelea faida zao kwenye post ya kachumbari cheki hapa....

Kitunguu Swaumu

1. Husaidia watoto tumboni kuongeza uzito.
2.Huimarisha mwili kupigana na magonjwa yakifua na baridi
3. Ina Iodine ambayo husaidia kutibu goita(Hyperthyroid).
4.Ina Vitamin C ambayo hutibu Kiseyeye (Scurvy)
5. Ina punguza magonjwa ya moyo
6.Hutibu vidonda na fungus
7. Ina Vitamin B6 ambayo hujenga viini vya mwili
8. Ina saidia kuzuia Kansa
9. Husaidia kuendesha damu mwilini.

Pilipili Mbuzi
1. Ina sawazisha sukari mwilini
2. Ina pigana na vidudu vya saratani mwili
3. Ina zuia magonjwa ya moyo.
4. Ina zuia magonjwa ya viungo mwilini kama Arithritis.





Usiipike lakini chachandu yako, kwani ukiipika unaua viini vyake vyenye kusaidia kusaga chakula mwilini, na pia hupunguza nguvu yake mwilini. Tujitahidi kula chachandu jamani, ata ukiondoa pilipili bado unapata faida zake.

Futari Njema Wadau!




No comments:

Post a Comment