Pages

Sunday, July 13, 2014

Msomi wa Leo - Sheikh Syed Muhammad Naquib Al-Attas

Sheikh Al-Attas amezaliwa Septemba 5 mwaka 1931, Bogor, Java(Indonesia). Ni Msomi wa dini wa kisasa, ambaye utaalamu wake upo kwenye sayansi ya kiislamu, na jinsi ya kuitumia kwenye maisha ya sasa. Nia yake ni moja, Kusilimisha akili, mwili, nafsi na jinsi inavyo tuendesha kwenye maisha yetu na waislamu wote na wasio waislamu. Ni mwandishi wa vitabu 27 kwenye topic tofauti ya uislamu na maendeleo ya watu.

Alimaliza shule ya sekondari mwaka 1951, na kuingia jeshi Malaysia ambapo alichaguliwa kusoma Eaton Hall, Chester Uingezera, na baadae alisoma the Royal Military Academy, Sandhurst, Uingereza mpaka alipomaliza mwaka 1955. Alipata fursa ya kusafiri kwenda Spain, na Afrika ya kaskazini, akawa bado anahamu ya kujielimisha zaidi kidini, ndo alipo acha kazi yake, na kurudi kusoma chuo kikuu cha Malaya Singapore mwaka 1957-1959. 

Alipokuwa shule aliandika thesis, iliyomfanya apate fellowship kwenye Chuo Kikuu cha McGill, Montreal Canada. Alipata Shahada yake ya pili kwenye masomo ya filosofia ya kiislamu mwaka 1962. Alipomaliza hapo, akaenda kusoma Uingereza kwenye Chuo kikuuu cha London na kuchukua shahada yake ya tatu kwenye College ya Oriental and African Studies. Mwaka 1965, alirudi Malaysia, na akawa Mkuu wa shule ya Fasihi kwenye Chuo Kikuu cha Malay, Kuala Lumpur. Mwaka 1968-1970 alikuwa Dean wa Faculty of Arts. Alihamia National University of Malaysia, mwaka 1973, kama mkuu wa Idara ya Lugha ya Malay na Fasihi, baadae akawa Dean wa Faculty ya Arts. 1987 alianzisha the International Institute of Islamic Thought and Civilization, Kuala Lumpur Malaysia.

Sheikh pia ni mchoraji mzuri wa maandishi ya kiislamu, na kazi zake zime onyeshwa Tropen Museum, Amsterdam. Sheikh kashiba haswa kwenye masoma ya dini na dunia. Msikilize mwenyewe hapo chini anakuwa interviewed na sheikh Hamza Yusuf.


Masha'allah! Mwenyezi Mungu amzidishie Elimu ya Dunia na Akhera, na amfungulie milango yake ya kheri hapa duniani na Akhera.

No comments:

Post a Comment