Pages

Thursday, July 3, 2014

Chakula Bora cha Leo - Parachichi

 Parachichi ni moja ya yale matunda ambayo unayapita sokoni bila hata kuyatupia jicho la pili, na roho wala haishtuki. Kwa maana nyingine, huna uzoefu nalo sana. Halina ladha yoyote, mara nyingi watu huongezea chumvi au sukari kuipa ladha fulani hivi. Lakini, Parachichi ni moja ya chakula bora duniani, ngoja tuangalie faida zake.

1. Husadia kuboresha Moyo.
2. Ina beta-sitosterol ambayo husaidia kupunguza cholesterol kwenye moyo.
3. Ina Potassium ambayo husaidia na blood pressure.
4. Ina Carotenoid lutein amabayo husaidia kuzuia cataract na magonjwa ya uzee ya macho.
5. Ina sawazisha sukari kwenye damu
6. Ina folate na folic acid ambayo husaidia kupigana na maradhi ya watoto kuzaliwa na vilema au kasoro za mwili, nzuri haswa kwa wale akina mama wajawazito.
7. Husaidia kulinda na stroke ya mwili
8. Huzuia kukua kwa viini vya saratani.
9. Husaidia kupunguza kuzeeka kwa mwili.
10. Husafisha tumbo ambacho ndo chanzo cha ulimi na mdomo kunuka.
11. Husaidia mwili kuvuta virutubisho vya chakula kwenye mwili vizuri.
12. Huboresha ngozi na kutibu magonjwa mengi ya ngozi.

Usijisahau lakini ukalila kwa wingi kwani lina nenepesha pia ukilila sana, lakini ukiweza kula nusu kwa siku si mbaya badala ya yale maandazi ya saa nne. Pia unaweza kulitupia kwenye kachumbari kama hivi, familia yako yote ikafaidika.
Au ukainyunyuzia chumvi na limao pia ni tamu, na tulishaona faida za limao posti ya nyuma. 

Futari Njema!

B6 and folic acid, which help regulate homocysteine levels. High level of homocysteine is associated with an increased risk of heart disease. Avocado also contains vitamin E, glutathione, and monounsaturated fat, which help in maintaining a healthy heart.
- See more at: http://www.undergroundhealth.com/15-amazing-health-benefits-of-eating-avocados/#sthash.Jr0CkxE8.dpuf

No comments:

Post a Comment