Pages

Saturday, July 19, 2014

Fungo Kumi la Mwisho la Ramadhani

Alhamdulillah! tumefika fungo kumi la mwisho, na sasa countdown yenyewe ndo inaanza. Ni wakati huu watu wengi hua swaum ina leta shida kidogo, ukali unazidi, na siku zinaonekana ndefu zaidi. Lakini hizi siku kumi za mwisho ni za kuomba Allah akukinge na Moto wa Jahanamu. Usiku wa laylatul kadri, usiku wa nguvu ambaye Jibril mwenyewe anashuka na Malaika wengine kwa ruhsa ya mwenyezi mungu duniani, na wote tunajua Jibril ni mkubwa wa Malaika. Kwahiyo tuzidishe ibada, tujitahidi kufanya itkaf (kufanya ibada usiku)misikitini kama utaweza, na tujitahidi kutoa sadaka sana.

Usiku wa Laylatul Kadri uta angukia kati ya Ramadhani 21,23,25 au 27, ambazo ni usiku wa Julai 18,20,22,24 na 26. In'shaa'llah, Allah atatusamehe madhambi yetu na atajibu maombi yetu.

No comments:

Post a Comment