Pages

Wednesday, July 23, 2014

Msomi wa Leo - Sh. Mishary bin Rashid Al-afasi


Amezaliwa September 5 mwaka 1976 Kuwait. Sh.Al-Afasi ana shahada kutoka chuo kikuu cha Madina, na utaalamu wake ulikuwa kwenye aina 10 za kusoma Qur'ani na tafsiri zake.  Alisha soma Qur'ani mbele ya wasoma Qur'ani wakubwa kama Sheikh Ahmed Abdulaziz Al-Zaiat, Sheikh Ibrahim Ali Shahata Al-Samanodei na Sheikh Abdurarea Radwan.Sheikh ana mke na watoto wawili wa kike.

Sheikh ameshaswalisha Taraweh Islamic Center ya Irvine California Marekani.  Sheikh anaonekana kwenye channel mbili za dini, ambayo moja ni Alafasy TV. Sasa hivi Sheikh ni Imam wa Msikiti wa Al-Kabir(Msikiti Mkuu) uliokuwa mji wa Kuwait, na huswalisha Taraweh mwezi wa Ramadhani. Sheikh pia ni msoma mashairi au tuseme muimba Qaswida, na Qaswida yake moja nilishaipostigi hapa ...>>>


Msikilize Sheikh hapo chini anavyo kusomea Sura Yasin.

Mashallah! Mwenyezi Mungu amzidishie Elimu ya Dini na Dunia.


No comments:

Post a Comment