Pages

Tuesday, July 31, 2012

Ebola yazuka Uganda

Hivi tunafuatilia yaliyo wakumba majirani zetu Uganda? Ebola imewarudia tena kwenye wilaya ya Kibaale, na watu 14 wamesharifiki mwezi huu. Moja kati ya hao, alikufia Kampala. Sasa najua wabongo tume relax, kwasababu haipo bongo, lakini, kaa ufikirie watu wangapi huvuka mipaka ya Tanzania na Uganda?

Huu ugonjwa ni Hatari na watu wakiupata ni kukutana na Mola wako tu, hamna namna. Ni muhimu kuelimishana. Hili gonjwa linasababishwa na virusi vya aina nne. Una ambukizika kwa mkutanisho wa maji ya mwili au na kitu chochote kilicho chafuliwa na maji yenye virusi hivi. Mwanzo wake utadhana unapata Malaria vile, homa, kuishiwa nguvu, viungo mwilini kuuma, kichwa na koo pia huuma. Stage ya pili, unaanza kutapika, kuharisha na tumbo linauma.Stage ya tatu wagonjwa wengine hupata vipele, macho huwa mekundu, na unaanza kutokwa na damu ndani na nje wa mwili. Haina tiba, na unakufa fasta fasta. Mwaka 2000 huu ugonjwa uliuwa watu 224 upande wa kaskazini wa Uganda, 2007 ukauwa 42 Magharibi wa Uganda, na 2011 ukauwa 1 pande za Kati wa Uganda.


Hivi jipige picha, unaumwa, lakini umetenganishwa na watu hata ndugu zako hawataweza kukuona mpaka roho unakata. Haya tuyaache hayo, wewe nurse hospitalini, umemtibu mgonjwa wa Ebola bila kujua, unajikuta na wewe pia umetengwa, kwako huwezi kurudi incase na wewe umeambukizwa. Ni uwoga gani utakuwa nao? Yaani jamani kumuomba tu Mungu akuepusha na haya majangwa mengine. Saa nyingine najiuliza, hivi ma professors wetu wote na ma scientists, kwanini hawa dedicate research kutafuta tiba la hili gonjwa? Tunao athirika ni sisi waafrika, na gonjwa hili limetoka Ukimwi kwa vitisho. Yaani hata maiti pia bado ya ambukiza, sasa kuna cha kumuosha na kumtayarisha maiti hapo?

Nawaacha na hii picha, kama Mexico ingekuwa Uganda, wananchi wake wote wangetoka na vazi hili. 
Bado gloves na miwani tu hapo.


Sunday, July 29, 2012

University of Medina - Free Everything!!!!

Free Everything? Yup you heard me right! KILA KITU BUREEEE! The Islamic University of al-Madinah al-Munawarah That was founded by the government of Saudi Arabia in 1961 is offering free college education to everybody including International Students.

Students May Study Sharia, Quran, Dawah, Usul al-din, Hadith and Arabic.  The school offers a Bachelors of Arts degree, Masters and Doctorate degrees. They review the applications yearly and the academic year starts in September and ends in June.Students who don't know Arabic have to take a two year Arabic institute in the same University, and pass with an 80% or greater to advance to the university program.


Now get this, not only do you get Free Tuition, are you ready for this? They pay you a monthly Salary of $225, which is enough for a single student's living. Now it doesn't stop there, THEY GIVE YOU A FREE ROUND TRIP TICKET ONCE A YEAR TO YOUR HOME COUNTRY!  Dude that's like a gig, So what are you waiting for? The requirements are a bit strict, you have to have a high school certificate. I suggest you contact your nearest Saudi Embassy for the application and do it fast.
The video below shows the life of a student at The Islamic University of Al-Madinah. Enjoy!

For More Information Go Here


Ramadhan Laugh

Are you a Ramadhan Muslim? Check the Video Below, Things Muslims say in Ramadhan, its hilarious.


Friday, July 27, 2012

FUTARIIIIIIII!!!!!!!!!!! PART 2

Kwanza naanza na kumshukuru Mungu Alhamdullilah kwa kutufikisha mpaka tukamaliza wiki ya kwanza ya Ramadhani. Enhe! Sasa wiki imesha katika, vipi mmeongeza makilo mangapi mpaka leo hii? Mimi kwa upande wangu mambo yalikuwa moto moto, ni MAFUTARIIIII ya nguvu.

Basi mimi sisemi mengi, nitawaacha tu na mapicha ya mafutari niwape mawazo, labda itajibu maswali yenu ya tule nini leo?
SAMBUSAAAA!!!!
Huwa ni Kitafunio kinachopendwa na wote. 
Sambusa Volcanic Mountain, about to erupt.
Helicopter view of the Volcanic mountain.hahahha!
Kuna mtu moja nilienda kula futari kwao, nikakuta wanapika sambusa, akaniambia wao kwao
sambusa ikikosekana, hakieleweki. Na mimi nikambwambia sisi kwetu, bila Kalmati, hapakaliki.
Mambo ndio haya ya Chapati ya Maji.
This is a hit in every household.
Vibibi mnavijua jamani?
Nyongeza nyingine hii ya sukari, kubadilisha mlo.
Le manioc de noix de coco, MMPO?
Muhogo wa Nazi
Tambi et Kuku?
Mihogo unapendeza na nyama ya kukaanga, watu hupenda mbuzi au ngombe, lakini kuku pia inaenda.

  BIRIANIII!!!!!! 
Siku nyingine ni kupumzisha vyakula vya hapo juu, na ku weka vitu simple.
I hate to say this, but ni vigumu mtu kukonda aisee. Jaribu tu kutoshindilia.
Huu mlu ni mzuri kwa kuficha matunda na saladi, bila watu kujua wanayala kwa style hii.
CheeseCake - Mara moja moja pia Rukhsa.
Wiki ndio ilimalizika hivi. Wewe je?
Ukifuata ile style ya kula nilioisema ile post ya kwanza, mtaweza tu kuzi maintain hizo kilo.

Thursday, July 26, 2012

Shairi la Leo - Msomaji Hadija Binti Omari

Kuna wakati mwingine mtu anakupatia ujumbe wa mwenyezi mungu kwa kuongea tu, una sikilizi ikiisha unaendelea zako na shughuli zako na wala hukumbuki alichokisema. Lakini akiimba kwa style ya Shairi na sauti nzuri, maneno yale yale ya mwanzo, unaguswa zaidi hata chozi utatoa. Mwenyezi Mungu akikupa kipaji bwana, ni baraka juu ya baraka.

Nawaacha na Shairi hili la dini, lilosomwa na Hadija Binti Omari. Jamani tukumbukeni kufanya Ibada sana kwenye huu mwezi mtukufu.


 Masha'allah! Mwenyezi Mungu amzidishie elimu na imani huyu binti.






Wednesday, July 25, 2012

FREE COLLEGE EDUCATION!!!!!!!

Today I am soooo excited! I stumbled into this wonderful find. Free College Education! YES YOU HEARD ME RIGHT, CHUO KIKUU CHA BUREEEEE!!!!!!.
Islamic Online University is offering FREE Diploma Programs and Bachelors of Arts Degrees in Islamic Studies in English. Jamani mkaambizane, this is a great opportunity kwa ma ustadhi wetu wapate credentials and education.I went in and looked at their curriculum and they are offering proper Islamic classes with proper electives besides the intensive Islamic classes like Accounting, Psychology, Human Resources, Marketing, Mass Comm and etc. Yaani, the student will be getting a well rounded education for FREE. Lets be real people, you can't beat that. So spread the word, lets take advantage of this great opportunity.

Mambo yenyewe ndio kama haya hapo.

Monday, July 23, 2012

Aya of the Day - Ayatul Kursi

Out of the many Ayas that are found in the Quran, Ayatul Kursi or The Throne is one of the powerful ones. It is found in the Quran chapter two Suratul Al-Baqara verse 255. This verse talks about Allah's power over the entire universe. We Muslims are also advised to recite it at night, as Allah appoints a guard for you to stay with you throughout the night and no evil will come near you till morning, the same goes to one who recites it every morning will be in the protection and safety of Allah until the night. Prophet Mohammed(SAW) said, "The one who recites it after each of the obligatory prayers, then death will be the only thing preventing him from entering heaven." Abu Dhar(RA) said, "O Messenger of Allah, what is the greatest thing that has been revealed to you? The prophet said, Ayat AL-Kursi."  So have you memorized your Ayatul Kursi yet?

Here is a video that will help you learn this great Aya.

If you know how to read your Arabic letters, then the video below is for you.


Msomi wa Leo - Imam Saud Al-Shuraim

Imam (Dr.) Saud Al-Shuraim(PHD) ni moja wa imam wakuu wa Msikiti wa Makka Masjid al-Haram. Ni Professor na Mkuu wa Idara ya Sheria na masomo ya Kiislamu Chuo Kikuu cha Umm al-Qura Makka, na ni Hakimu wa Sheria pia Makka. Kaandika vitabu vingi tu vya kiislamu na mashairi, na ana swalisha pia kwenye msikiti wa Al-Haram. Kazaliwa mwaka 1964 na ana mke moja na watoto watatu(wavulana wawili na msichana moja).


Sikiliza Surah Ar-Ra'd - Qur'ani Kurasa 13 iliteremka Medina na imesomwa na Imam Saud Al-Shuraim
Mwenyezi Mungu amzidishie elimu na baraka za dunia na akhera.



Ukitaka tafsiri yake ya kiswahili, Nenda hapa.

Sunday, July 22, 2012

FUTARIIII!!!!!

Uji wa pili pili manga, kunde za nazi, maharage ya sukari, tambi, chapati, kalmati, mihogo, viazi vitamu, mzuzu wa nazi. Uwii jamani kuna muislamu asiyeiwaza futari toka akiamka japo muda wake haujafika? Jamani na mimi nipo kwenye huo mkumbo. Nikiangalia ramadhani hii watu wa Europe wanaanza kufungua kuanzia saa tatu usiku mpaka nne kasoro,  mmh! poleni maanake huo ni mtihani.

Leo nataka kuongelea maswala ya futari.Tuna tatizo sisi waislamu ya kubugia time ya futari mpaka unashindwa kufanya lingine lolote. Matokeo yake unabaki hupati choo vizuri, unanenepa mwezi wa ramadhani, which defeats the purpose of fasting. Tukumbukeni kula balanced diet na kula in moderation.

Basi ngoja niwaacheni na vi tips vya kuwapikia familia zenu time hizi za ramadhan.
Anza na matunda, hii itawa keep familia busy kidogo wakati wewe unamalizia futari.
Pia utawapa familia yako nutrition na fiber wanazohitaji.
Tafuta matunda yaliyo kwenye msimu, ndio matamu zaidi. 


Matunda kama Tende yanapatikana mwaka mzima, na hata mtume Mohammed(S.A.W) alikuwa anapenda kuanzia nayo. 
Wakimaliza kula matunda, suna tu sio kushiba sasa, waka swali magharibi :) 


Mzuzu wa kukaanga is usually a hit in my household, ukichanganya na mbuzi kidogo.

Baada ya matunda(Dessert kwanza) dish kama hili baada ya salaa magharibi. Ni vizuri zaidi upate mboga ya majani kidogo au lettuce, lakini sisi kwetu mchicha utaula mwenyewe, watu wanataka vya sukari tu na starch nyingi.

Nawaacha na futari spread kutoka msikitini USA, wenzetu watu wa nchi zingine kama USA, UK na Uarabuni, huwa wanafuturisha kwenye misikiti yao. Na sisi pia tujitahidi kupeleka hata maji na tende msikitini jamani watu waweze kufungua vinywa.





Saturday, July 21, 2012

Allah ni nani?

Hapa karibuni katika kupita pita kwangu youtube, nimekuta misconception kubwa kuhusu Allah mungu wa waislamu. Sijui tunaabudu mwezi ,mara jiwe jeusi Makka na kadhalika. Kwahiyo nimeamua kuandika kipande hiki kidogo tu, kuwaeleza kuhusu Allah.

Allah ni mungu kwa lugha ya kiarabu, ukishika biblia yoyote ya kiarabu, utaona mungu anaitwa Allah. Waislamu tunaamini Mungu ni mmoja. Ni Mungu huyo huyo wa nabii Ibrahim(A.S),nabii Musa(A.S), nabii Noah(A.S), nabii Daudi(A.S) na nabii Issa (A.S). Tofauti yetu sisi Waislamu na Wayahudi na Wakristo ambaye kwenye Kurani, wanaitwa watu wa Kitabu (Biblia), ni jinsi tunavyo amini asili ya Mungu. Waislamu sisi tuna amini umoja wa mungu, hajazaa wala hajazaliwa na tunaamini hana anaye fanana naye hata moja(Quran Sura 112). Hatuabudu Mungu Mwezi wala hatuamini Mungu jiwe lililoko Makka.

Nawaacha na Surah An Nur Kurani 24 Aya 35, moja ya aya ninayoipenda mimi binafsi, mwenyezi mungu anatuelezea asili yake.


"Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Aya Imetafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani.


Friday, July 20, 2012

Boti ya zama Tanzania.

Inasikitisha tuna anza mwezi huu mtukufu na huzuni. Boti ya MV Skagit inayo endeshwa na kampuni ya Seagull iliyokuwa inatoka Dar kwenda Zanzibar,yazama na inasemekana watu 31 wamefariki na miili iliyo patikana mpaka sasa ni 24. Kisa cha kuzama ni hali ya hewa mbaya na mawingu kuwa makubwa kusababisha boti kupinduka.


Hali ilivyo kuwa baada ya boti kupinduka.
  

Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea
maiti.
(Picha kwa hisani ya michuzi)
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.  "Kwakweli kwa mwenyezi mungu ndio tunakotoka na kwake ndio tutarejea."
Inasikitisha zaidi ukipata habari kuwa wengi walio fariki ni watoto. Mwenyezi mungu awasadie ndugu na jamaa waliopoteza watu kwenye hii ajali, na azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

Ramadhan Kareem Everybody! 2012

So its that time of year again, how else to better explain what Ramadhan is then this lovely video from Zaky and Friends. Enjoy!


Surah Al-faatiha

Ningependa kuanza blog hii na hii sura ambayo kila muislamu anaijuia. Nini zaidi ya Suratul Al-faatiha au Alhamdu? Hii sura aliteremshiwa Mtume Mohamed(S.A.W) akiwa Makka kabla ya Hijra(Safari yake ya kuhamia Medina kutoka Makka).Pia ni sura ya kwanza kwenye Msahafu, so enjoy!



KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA NA MWENYE KUREHEMU. 

 Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;

 Mwingi wa Rehema  na Mwenye Kurehemu; 

 Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. 

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. 

Tuongoze njia iliyo nyooka, 

Njia ya ulio waneemesha, sio ya walio kasirikiwa, wala walio potea.

AMIN!