Pages

Saturday, July 21, 2012

Allah ni nani?

Hapa karibuni katika kupita pita kwangu youtube, nimekuta misconception kubwa kuhusu Allah mungu wa waislamu. Sijui tunaabudu mwezi ,mara jiwe jeusi Makka na kadhalika. Kwahiyo nimeamua kuandika kipande hiki kidogo tu, kuwaeleza kuhusu Allah.

Allah ni mungu kwa lugha ya kiarabu, ukishika biblia yoyote ya kiarabu, utaona mungu anaitwa Allah. Waislamu tunaamini Mungu ni mmoja. Ni Mungu huyo huyo wa nabii Ibrahim(A.S),nabii Musa(A.S), nabii Noah(A.S), nabii Daudi(A.S) na nabii Issa (A.S). Tofauti yetu sisi Waislamu na Wayahudi na Wakristo ambaye kwenye Kurani, wanaitwa watu wa Kitabu (Biblia), ni jinsi tunavyo amini asili ya Mungu. Waislamu sisi tuna amini umoja wa mungu, hajazaa wala hajazaliwa na tunaamini hana anaye fanana naye hata moja(Quran Sura 112). Hatuabudu Mungu Mwezi wala hatuamini Mungu jiwe lililoko Makka.

Nawaacha na Surah An Nur Kurani 24 Aya 35, moja ya aya ninayoipenda mimi binafsi, mwenyezi mungu anatuelezea asili yake.


"Mwenyezi Mungu ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake ni kama shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa. Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wa mashariki wala magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung'aa wenyewe ingawa moto haujayagusa - Nuru juu ya Nuru. Mwenyezi Mungu humwongoa kwenye Nuru yake amtakaye. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Aya Imetafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani.


1 comment:

  1. Beautiful Surah Thank you. Waisilamu wanaamini mungu Mmoja sio jiwe wala sanamu!

    ReplyDelete