Pages

Friday, July 20, 2012

Surah Al-faatiha

Ningependa kuanza blog hii na hii sura ambayo kila muislamu anaijuia. Nini zaidi ya Suratul Al-faatiha au Alhamdu? Hii sura aliteremshiwa Mtume Mohamed(S.A.W) akiwa Makka kabla ya Hijra(Safari yake ya kuhamia Medina kutoka Makka).Pia ni sura ya kwanza kwenye Msahafu, so enjoy!



KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA NA MWENYE KUREHEMU. 

 Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote;

 Mwingi wa Rehema  na Mwenye Kurehemu; 

 Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. 

Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. 

Tuongoze njia iliyo nyooka, 

Njia ya ulio waneemesha, sio ya walio kasirikiwa, wala walio potea.

AMIN!



1 comment: