Pages

Tuesday, July 31, 2012

Ebola yazuka Uganda

Hivi tunafuatilia yaliyo wakumba majirani zetu Uganda? Ebola imewarudia tena kwenye wilaya ya Kibaale, na watu 14 wamesharifiki mwezi huu. Moja kati ya hao, alikufia Kampala. Sasa najua wabongo tume relax, kwasababu haipo bongo, lakini, kaa ufikirie watu wangapi huvuka mipaka ya Tanzania na Uganda?

Huu ugonjwa ni Hatari na watu wakiupata ni kukutana na Mola wako tu, hamna namna. Ni muhimu kuelimishana. Hili gonjwa linasababishwa na virusi vya aina nne. Una ambukizika kwa mkutanisho wa maji ya mwili au na kitu chochote kilicho chafuliwa na maji yenye virusi hivi. Mwanzo wake utadhana unapata Malaria vile, homa, kuishiwa nguvu, viungo mwilini kuuma, kichwa na koo pia huuma. Stage ya pili, unaanza kutapika, kuharisha na tumbo linauma.Stage ya tatu wagonjwa wengine hupata vipele, macho huwa mekundu, na unaanza kutokwa na damu ndani na nje wa mwili. Haina tiba, na unakufa fasta fasta. Mwaka 2000 huu ugonjwa uliuwa watu 224 upande wa kaskazini wa Uganda, 2007 ukauwa 42 Magharibi wa Uganda, na 2011 ukauwa 1 pande za Kati wa Uganda.


Hivi jipige picha, unaumwa, lakini umetenganishwa na watu hata ndugu zako hawataweza kukuona mpaka roho unakata. Haya tuyaache hayo, wewe nurse hospitalini, umemtibu mgonjwa wa Ebola bila kujua, unajikuta na wewe pia umetengwa, kwako huwezi kurudi incase na wewe umeambukizwa. Ni uwoga gani utakuwa nao? Yaani jamani kumuomba tu Mungu akuepusha na haya majangwa mengine. Saa nyingine najiuliza, hivi ma professors wetu wote na ma scientists, kwanini hawa dedicate research kutafuta tiba la hili gonjwa? Tunao athirika ni sisi waafrika, na gonjwa hili limetoka Ukimwi kwa vitisho. Yaani hata maiti pia bado ya ambukiza, sasa kuna cha kumuosha na kumtayarisha maiti hapo?

Nawaacha na hii picha, kama Mexico ingekuwa Uganda, wananchi wake wote wangetoka na vazi hili. 
Bado gloves na miwani tu hapo.


No comments:

Post a Comment