Pages

Friday, January 16, 2015

Wapiga ramli kupigwa marufuku TZ

Mwaka Mpya Mambo Mapya.

Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.
Waziri wa mambo ya ndani, nchini humo, Mathias Chikawe amesema kwamba msako wa kitaifa utaanza hivi karibuni kuwakamata waganga hao na kuwafikisha mahakamani ikiwa wataendelea na kazi zao.
Watu wenye ulemavu wa ngozi, wanakabiliwa tisho kubwa juu ya maisha yao, kwani wamekuwa wakilengwa kwa sehemeu zao za mwili na waganga pamoja na wapiga ramli wanaoamini kwamba viungo hivyo huleta bahati ya kupata mali.
Chama cha maalbino nchini humo kimesifu uamuzi wa serikali kuwapiga marufuku waganga hao.
"ikiwa kutakuwepo ushirikiano kati yetu na serikali, itakuwa ndio mwanzo wa nguvu mpya ya kupambana na ukatili unaotendewa walemavu wa ngozi,'' alisema mwenyekiti mmoja wa chama hicho Ernest Njamakimaya.
"ninaamini hii ndio njia ya pekee ambayo tunaweza kutumia kupambana na ukatili huo na kuukomesha kabisa.''
'ushahidi unavyovurugwa''
Soma Habari zaidi hapa ....

Ijumaa Njema Wadau!

No comments:

Post a Comment