Pages

Thursday, October 29, 2020

Qasida Kutoka Tanzania Leo -Uso Wa Mtume

Tumsalie Mtume (Salāt ‘alā al-Nabī)

Allāhumma salli ‘alā Muhammadin wa ‘alā āli Muhammad, 
kamā sallayta ‘alā Ibrāhīma wa ‘alā āli Ibrāhīm. 
Wa bārik ‘alā Muhammadin wa ‘alā āli Muhammad, 
kamā bārakta ‘alā Ibrāhīma wa ‘alā āli Ibrāhīm.
Fil-’ālamīn, innaka Hamīdun Majīd.
 
Happy Maulid al-Nabī

Friday, October 23, 2020

Aya ya Leo - Ujasiri(Courage)

 


 Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini. 

So do not weaken and do not grieve, and you will be superior if you are [true] believers.  (Qur'an 3:139)

Jumaa Mubarak!

Friday, October 9, 2020

Aya ya Leo - Utofauti (Diversity)

 

 Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.

And of His signs is the creation of the heavens and the earth and the diversity of your languages and your colors. Indeed in that are signs for those of knowledge.(Qur'an 30:22)

Jumaa Mubarak!  

Wednesday, August 26, 2020

Hadithi ya Leo - Kufunga Ashura

 

Imehadithiwa na Aisha:

Mtume wa Allah aliwa amrisha waislamu wafunge siku ya Ashura, na kufunga mwezi wa Ramadhani ulivyo faradhishwa, ikawa hiari kufunga siku ya Ashura.
 
Narrated `Aisha:

Allah's Messenger (ﷺ) ordered (the Muslims) to fast on the day of 'Ashura', and when fasting in the month of Ramadan was prescribed, it became optional for one to fast on that day ('Ashura') or not.

(Bukhari 2001)

Friday, August 14, 2020

Aya ya Leo - Jahannam (Hell)

 



Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika.

And surely, We have created many of the jinns and mankind for Hell. They have hearts wherewith they understand not, they have eyes wherewith they see not, and they have ears wherewith they hear not (the truth). They are like cattle, nay even more astray; those! They are the heedless ones.
(Qur'an 7:179)
Jumaa Mubarak! 

Wednesday, August 12, 2020

Earth Quake in Dar-Es-Salaam, Tanzania 2020

Ufafanuzi wa tetemeko lililotokea maeneo mbalimbali nchini

Friday, July 31, 2020

Hajj 2020 Takbeerat & Labbayk | Eid al-Adha

Alhamdulillah for being alive. May Allah protect us all.
 
Eid Mubarak!

Aya ya Leo - Uzito (Hardship)

Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi.
For indeed, with hardship [will be] ease. 
 (Qur'an: 94:5)
Jumaa Kareem!

Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa - Afariki Dunia

To God we belong and to him is our return. 
Tumetoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.

May his Soul Rest in Peace.

Wednesday, July 22, 2020

Allah is sufficient for me

We cannot think of Hajj without talking about Prophet Ibrahim and how he was tested.May Allah be pleased with him the father of prophets.

Hatuwezi kuufikiria Hajj bila kumuongelea Nabi Ibrahim na mitihani aliyopata. Allah aridhike nae baba wa mitume.

When Abraham was Catapulted Into a Fire | A Voice in the Desert

Friday, July 17, 2020

President Erdogan's public address on Hagia Sophia

The Turkish court has ruled to convert the Hagia Sophia from a Museum to a Mosque.

First Friday Prayer will be 24th of July 2020.
No Entry fees.
Still open to the public for Muslims and non Muslims just like any other mosque around the world.

Mahakama ya Uturuki imeamua Hagia Sophia kubadilishwa kutoka kuwa Makumbusho na kurudia kua msikiti.
Swala ya kwanza ya Ijumaa itakuwa  tarehe 14 Julai 2020.
Hutahitaji pesa ya kuingilia.
Na bado itakuwa wazi kwa waislamu na wasio waislamu, kama misikiti mengine duniani.




Friday, May 29, 2020

Marudio(Repost):::Sura ya Leo - Masaa ya Asubuhi (The Morning Hours)


Naapa kwa mchana!
Na kwa usiku unapo tanda!
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
Na akakukuta umepotea akakuongoza?
Na Akakukuta fakiri akakutajirisha?
Basi usimwonee yatima!
Wala usimkaripie aulizaye
Na Neema ya Mola wako isimulie (kwa kushukuru na kwa kufanya amali njema)

By the morning brightness
And [by] the night when it covers with darkness,
Your Lord has not taken leave of you, [O Muhammad], nor has He detested [you].
And the Hereafter is better for you than the first [life].
And your Lord is going to give you, and you will be satisfied.
Did He not find you an orphan and give [you] refuge?
And He found you lost and guided [you],
And He found you poor and made [you] self-sufficient.
So as for the orphan, do not oppress [him].
And as for the petitioner, do not repel [him].
But as for the favor of your Lord, report [it].
(Qur'an Chapter 93)


This is one of my favorite Suras in the Quran. Kwasababu inaelezea ubinadamu wa Mtume Mohammed(S.A.W), na unaona vile mwenyezi Mungu alivyokuwa akiwaliwaza mitume wake kwa kazi ngumu waliokuwa wakiifanya. Hii Sura iliteremka Makka, na ni kati ya sura za mwanzoni kushuka. Ulikuwa umepita muda mrefu wa ukimya, Mtume alikuwa na huzuni akifikiri kwamba kuna jambo ametenda lililomuuzi Mwenyezi Mungu. Unacheki vile Mitume wetu walivyo kuwa na heshima na mapenzi ya Mola wao? Akina sisi hapa sijui tuna muudhi mara ngapi na wala mishipa ya damu haituchezi.

Basi Mwenyezi Mungu kumliwaza, akamshushia hii Sura kuvunja ukimya, baada ya hapo, Jibril (Gabriel) akawa anashuka na maneno ya Qur'an mpaka mauti yalipomkuta Mtume Mohammed(S.A.W).  
Isilikize
Natumaini Ijumaa yako leo itaanza vizuri.


Saturday, May 23, 2020

Eid Mubarak!

Alhamdullilah! We made it, another Ramadhan down.
May Allah bless us with good health to see many more Ramadhans, and May he bless us with the good of this world and the hearafter.

SHEIKH MKUU ATANGAZA KUANDAMA KWA MWEZI

The moon has been sighted in Tanzania on the eve of May 23rd, so Eid al-Fitr will be celebrated on Sunday May 24th.

Eid Mubarak Everyone!
Tukumbuke kuzitoa hizo zakatul fitr kabla ya swala ya Eid.

Friday, May 22, 2020

Aya ya Leo - Majaribu (Trials and Tribulations)


Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume wao na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.

Or do you think that you will enter Paradise while such [trial] has not yet come to you as came to those who passed on before you? They were touched by poverty and hardship and were shaken until [even their] messenger and those who believed with him said,"When is the help of Allah ?" Unquestionably, the help of Allah is near. (Qur'an 2:214)

Happy Last Friday of Ramadhan! 
It has been a ride this year, but I hope you took advantage of the pace Allah set for you to reflect this Ramadhan. If you did not take advantage of it, you still have time and also you can continue on with the 6 days after Ramadhan. 
May Allah accept our prayers, fasts and good deeds. 
May He bless us with the good of this world and the hereafter and make us all meet each other on the day of judgement with the best of people under his shade.
 Don't forget to donate your Zakatul fitr before the Eid Prayer to your community so we can all have a joyful Eid.  





URGENT! DUA FOR HEALTH دعاء للصحة والعافية



The night of power is upon us, May Allah accept all our prayers and bless us with good health, wealth and family.

Saturday, May 16, 2020

Ya Tawwab

Tuzidishe Ibada Kwenye Kumi la Mwisho.

Monday, May 11, 2020

Hadithi ya Leo - Geti la Ar-Raiyan (Gate of Ar-Raiyan)



Imehadithiwa na Sahl:

Mtume (ﷺ) alisema, "Kuna geti Akhera linaloitwa Ar-Raiyan, na wote wanaofunga wataingia kupitia geti hilo Siku Ya Kiyama, hamna wengine bali yao wataingia kupitia hapo. Itaulizwa,  'Wako wapi wale waliokuwa wakifunga?'
Watanyanyuka, na hakuna zaidi yao wataingia kupitia hapo.
Baada yao, geti litafungwa na hakuna mwingine atakayeweza kuingia kupitia geti hilo."

Narrated Sahl:

The Prophet (ﷺ) said, "There is a gate in Paradise called Ar-Raiyan, and those who observe fasts will enter through it on the
Day of Resurrection and none except them will enter through it. It will be said, 'Where are those who used to observe fasts?'
They will get up, and none except them will enter through it.
After their entry the gate will be closed and nobody will enter through it."
(Bukhari 1896)

Friday, May 8, 2020

Aya ya Leo - Hekima (Wisdom)


Yeye humpa hekima amtakaye; na aliye pewa hekima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hakuna atakayekumbuka isipokuwa wale wenye uelewa.

He gives wisdom to whom He wills, and whoever has been given wisdom has certainly been given much good. And none will remember except those of understanding.
(Qur'an 2:269)
Jumaa Kareem! 
Allah atukubalie funga na dua zetu. 

Wednesday, May 6, 2020

SHEIKH SULEIMAN KILEMILE AFARIKI DUNIA

Inna lillahi Waina Illahi Rajiun!
Mwenyezi Mungu ampe kauli dhabit, amsamehe madhambi yake na Amlaze mahali pema peponi.

Habari nilizopata ni sheikh amefariki kutokana na matatizo ya kisukari. 
Sasa kuna video ya mazishi yake iliyokua ikizunguka ikionyesha umati wa watu uliokusanyika kumzika sheikh wetu. 
Alhamdullilah amepumzishwa salama.

 Lakini jamani ndugu zangu ngoja tuongee leo kuhusu mazishi ya sheikh wetu mpendwa. Tumeambiwa kuna ugonjwa wa Corona na Serikali imekataza mikunsanyiko ya watu, sawa wengine walikuwa wamejikinga na barakoa na gloves, lakini lile jeneza watu wangapi wamelishika? Kuna mtu pale hakushika barakoa lake kulirekebisha kabla ya kuosha mikono yake au kutumia kitakasa mkono? Maana sio kama watu walikuwa kwenye kiyoyozi, lazima mtu alifuta jasho, au alitengeneza barakoa lake likae vizuri, yote hii ni kushika uso. Pia ule ukaribu wa watu haukuwa mita 2 au 3, na pale kulikuwa na wazee wetu na ma sheikh wetu ambao ni watu wazima, wengine wana matatizo ya pressure, kisukari, moyo nakadhalika.
Mwenyezi Mungu atustiri na siombei mabaya lakini naona kama majibu tutayapata baada ya siku 14.
Ndugu zangu najua ni vigumu lakini tujitahidini kufuata maagizo tunayo pewa na serikali. Sasa kwa vile yameshatokea, kama ulikuwepo, kajitenge kwa siku 14 ukitunza afya yako ili usiambukize familia yako.
Allah Atustiri!

Monday, May 4, 2020

Hadithi ya Leo - Jira Nyeusi/Habar Soda (Black Seed)


Imehadithiwa na Abu Huraira"
Nilisikia Mtume wa Allah (ﷺ) akisema, "Kuna tiba kwenye jira nyeuse(Habar Soda) kwa magonjwa yote isipokuwa kifo."

 Narrated Abu Huraira:
I heard Allah's Messenger (ﷺ) saying, "There is healing in black cumin for all diseases except death." (al-Bukhari 5688)

Friday, May 1, 2020

Aya ya Leo -Rekodi (The Register)

 Hakika Sisi tunawafufua wafu, na tunayaandika wanayo yatanguliza, na wanayo yaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari asli lenye kubainisha.

Indeed, it is We who bring the dead to life and record what they have put forth and what they left behind, and all things We have enumerated in a clear register. (Qur'an 36:12)
Jumaa Mubarak!

 

Rostam Aziz Donates COVID-19 Diagnostic Test to Zanzibar

 He also donated 9,000 hand sanitizers and 90,000 masks to the health care workers and the front-liners.
Mashaallah!
Mzee Aziz Katishaaaaa!
Kanunua kifaa cha kuweza kupima coronavirus Zanzibar na kupata majbu ndani ya masaa matatu na nusu. Sasa hivi Zanzibar hamna tena mambo ya kutuma tests Dar alafu usubirie majibu baada ya siku kadhaa.
Jamani haya ni zaidi ya mahaba.
Atasaidia watanzania wengi sana na kuokoa wengi, na kila mtu kwakweli ajitolea jinsi awezavyo kuwasaidia wananchi.
Mwenyezi Mungu amkubalie dua zake zote, amfungulie milango yake yote ya Kheri hapa duniani na Akhera. 
BE INSPIRED!

Tuesday, April 28, 2020

$1.00 COVID-19 Test Kits made in Senegal

Wana sayansi wa Senegal wameweza kutengeneza vipimo vya corona kwa shs 2,300. Na pia wanajitengenezia ventilator zao wenyewe.

Kuna umuhimu wa kuwapigia simu.

Monday, April 27, 2020

Naseeb Abdul Juma Issack AKA Diamond Platnumz Donates his hotel to be used for Covid-19 Patients

He also offered to pay rent for 500 families throughout Tanzania during this time.

Diamond Kweli Babalao!
Yaani, kwakweli inaonyesha vile Diamond ni mtu wa aina gani. Ana roho ya kipekee, na sio kama anapesa za matajiri wakubwa Tanzania. 
Allah amzidishie huu moyo wake wakujitolea, amkubalie dua zake na amfungulie Milango Yake Yote ya Kheri hapa Duniani na Akhera.
Be Inspired!

Hadithi ya Leo - Tiba (Cure)



Imehadithiwa na Abu Huraira:
Mtume (ﷺ) alisema, "Hakuna ugonjwa ulioundwa na Allah, isipokuwa ameunda na tiba yake."

Narrated Abu Huraira:
The Prophet (ﷺ) said, "There is no disease that Allah has created, except that He also has created its treatment." 
(Bukhari 5678)

Aya ya Leo - Wafuateni(Follow)

Wafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka.
Follow those who do not ask of you [any] payment, and they are [rightly] guided. (Qur'an 36:21)

Jumaa Kareem!

Thursday, April 23, 2020

Ramadhan Kareem!

O Allah, let this moon appear on us with security and Iman; with safety and Islam.
(O moon!) Your Rubb and mine is Allah. May this moon be bringing guidance and good. 
(At- Tirmidhi : Book 9, Hadith 1228)
Ramadhan Mubarak everyone!


Ramadhan Mubarak!

It is finally here.... 
Anxiously waiting on those moon sighting reports.
Ramadhan Mubarak everyone. 
May this year be filled with plenty of Allah's blessing.

Monday, April 20, 2020

10 Muslim coronavirus victims buried alongside each other

Dah inasikitisha kijana wa miaka 33

Mwenyezi Mungu awape kauli dhabit, hawa ndugu zetu walio tangulia mbele ya haki.

Friday, April 17, 2020

Monday, April 13, 2020

Hadithi ya Leo - Karantini (Quarantine)



Imehadithiwa na Saud:
Mtume (ﷺ) alisema, "ukisikia kuna mripuko wa ugonjwa unaoambukiza kwenye ardhi, usiingie; lakini kama ugonjwa huo ukitokea sehemu ulipo, usiondoke sehemu hiyo."

Narrated Saud:
The Prophet (ﷺ) said, "If you hear of an outbreak of plague in a land, do not enter it; but if the plague breaks out in a place while you are in it, do not leave that place."  
(Sahih Al-Bukhari 5728)

Stay Safe everyone! 
May Allah protect us all.


Friday, April 3, 2020

Things we take for granted - The Adhan (Call for Prayer)

If you have one of these folks in your neighborhood mosque, remember to seek them out and leave a little tip.
God is truly Great!
 Now hurry up to prayer!
Jumaa Mubarak!

Wednesday, March 18, 2020

Governor wa New York - Cuomo Akitoa maelezo ya virusi vya Corona (Covid-19)

Angalieni wenzetu vile wanaelezea vizuri
Ni hivi, 
Kuna wagonjwa wangapi?
Vitanda vya ICU vingapi?
ICU ventilator ngapi?
Na wafanyakazi (madaktari na ma nesi) wangapi?
Na ni vitu gani wanafanya kuhakikisha wanashughulikia hayo maswali hapo juu.

Mwenyezi Mungu atustiri na hili gonjwa.

Friday, March 6, 2020

Aya za Leo - Amka Uswali


Ewe uliye jifunika!
Amka uswali usiku, isipokuwa kidogo tu!
Nusu yake, au ipunguze kidogo.
Au izidishe - na soma Qur'ani kwa utaratibu na utungo.
Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito.
Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.


O you who wraps himself [in clothing],
Arise [to pray] the night, except for a little -
Half of it - or subtract from it a little
Or add to it, and recite the Qur'an with measured recitation.
Indeed, We will cast upon you a heavy word.
Indeed, the hours of the night are more effective for concurrence [of heart and tongue] and more suitable for words.
(Qur'an 73:1-6)
Jumaa Mubarak!

Monday, March 2, 2020

Hadithi ya Leo - Jinsi ya Kuomba Toba (How to ask for forgiveness)

 Happy Monday!
Abu Huraira alihadithia:
Mtume wa Allah, alikuwa akisema haya wakati amesujudu: " Ewe Mwenyezi Mungu, nisamehe madhambi yangu yote, madogo na makubwa, la kwanza na la mwisho, linalojulikana na lisilojulikana."

Abu Huraira reported:
The Messenger of Allah (ﷺ) used to say while prostrating himself: O Lord, forgive me all my sins, small and great, first and last, open and secret
. (Muslim 483)

Friday, February 28, 2020

Aya ya Leo - Safari ya Usiku (The Night Journey)


SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Exalted is He who took His Servant by night from al-Masjid al-Haram to al-Masjid al- Aqsa, whose surroundings We have blessed, to show him of Our signs. Indeed, He is the Hearing, the Seeing.
(Qur'an 17:1)
Jumaa Mubarak!

Coronavirus COVID-19 Current Data

Kesi zilizothibitishwa: 82,164
Vifo: 2,801
Waliopona: 32,897 
Wagonjwa waliobaki duniani: 46,466
 

Tuesday, February 25, 2020

Ramadhan Countdown - Happy Rajab!

It is official! 
We have begun our Ramadhan Countdown.
So let's start planting those seeds people.
Happy Rajab Everyone!