Pages

Friday, May 29, 2020

Marudio(Repost):::Sura ya Leo - Masaa ya Asubuhi (The Morning Hours)


Naapa kwa mchana!
Na kwa usiku unapo tanda!
Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
Na akakukuta umepotea akakuongoza?
Na Akakukuta fakiri akakutajirisha?
Basi usimwonee yatima!
Wala usimkaripie aulizaye
Na Neema ya Mola wako isimulie (kwa kushukuru na kwa kufanya amali njema)

By the morning brightness
And [by] the night when it covers with darkness,
Your Lord has not taken leave of you, [O Muhammad], nor has He detested [you].
And the Hereafter is better for you than the first [life].
And your Lord is going to give you, and you will be satisfied.
Did He not find you an orphan and give [you] refuge?
And He found you lost and guided [you],
And He found you poor and made [you] self-sufficient.
So as for the orphan, do not oppress [him].
And as for the petitioner, do not repel [him].
But as for the favor of your Lord, report [it].
(Qur'an Chapter 93)


This is one of my favorite Suras in the Quran. Kwasababu inaelezea ubinadamu wa Mtume Mohammed(S.A.W), na unaona vile mwenyezi Mungu alivyokuwa akiwaliwaza mitume wake kwa kazi ngumu waliokuwa wakiifanya. Hii Sura iliteremka Makka, na ni kati ya sura za mwanzoni kushuka. Ulikuwa umepita muda mrefu wa ukimya, Mtume alikuwa na huzuni akifikiri kwamba kuna jambo ametenda lililomuuzi Mwenyezi Mungu. Unacheki vile Mitume wetu walivyo kuwa na heshima na mapenzi ya Mola wao? Akina sisi hapa sijui tuna muudhi mara ngapi na wala mishipa ya damu haituchezi.

Basi Mwenyezi Mungu kumliwaza, akamshushia hii Sura kuvunja ukimya, baada ya hapo, Jibril (Gabriel) akawa anashuka na maneno ya Qur'an mpaka mauti yalipomkuta Mtume Mohammed(S.A.W).  
Isilikize
Natumaini Ijumaa yako leo itaanza vizuri.


No comments:

Post a Comment