Pages

Wednesday, May 8, 2019

Msomi wa Leo - Al Būsīrī (1212-1295)

Abu Abdullah Muhammad ibn Sa'īd ul-Būsīrī Ash Shadhili  Almaarufu Al-Busiri, alizaliwa Misri mwaka 1212. Al-Busiri alipata elimu yake ya dini chini ya Sheikh Al-Mursi Abu'l-'Abbas, Alikuwa anajulikana kama Mshairi Maarufu sana Misri.

Al-Busiri japukuwa alikuwa ni Mshairi wa Misri, familia yake ilitokea Moroko. Alianza kuandika Mashairi yake chini ya Ibn Hinna vizier wa Misri. Aliandika mashairi mengi lakini Mashairi yake maarufu ni Qasida al-Burda. Qaswida hizo tunazisikia mpaka leo kwenye maulidi na maharusi, na washairi waliokuja baada yake, bado wanazitumia mashairi yake kama misingi ya mashairi yao. Qaswida zake ziliweza kutafsiriwa kwenye lugha tofauti na zikakuza ukubwa wake. Busiri alifariki mwaka 1295 mjini Alexandria, Misri. 

Sikiliza moja ya Qaswida kwenye kitabu chake cha Qasida Al-Burda.


Mwenyezi Mungu Amuwekee Nuru Kwenye Kaburi lake na Amuinue daraja kwenye Pepo yake. 


No comments:

Post a Comment