Pages

Friday, May 31, 2019

Aya ya Leo - Midnight Sun (Jua la Usiku)

Hata alipo fika matokeo ya jua aliliona linawachomozea watu tusio wawekea pazia la kuwakinga nalo.


Until, when he came to the rising of the sun, he found it rising on a people for whom We had not made against it any shield. (Qur'an 18:90)

Alhamdullillah! Ndo tunamalizia Ramadhani na Ijumaa Yetu ya mwisho.
Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi, apokee dua zetu na atufungulie Milangu yetu ya Kheri hapa Duniani na Akhera.
Ijumaa Njema!

Wednesday, May 29, 2019

Msomi wa Leo - Rajai Ayoub

Msikilize Mwenyewe akielezea Historia yake.
Mashaallah! Mwenyezi Mungu Amzidishie Kipaji chake, na amfungulie milango yake ya Kheri.

Monday, May 27, 2019

Hadithi ya Leo - Ubinadamu (Humanity)


Imehadithiwa na Abu Musa Al-Ash'ari

Mtume alisema, "Toa chakula kwa wenye njaa, watembelee wagonjwa na muachie
aliyefungwa" (kwa kulipia fidia yake)
Narrated Abu Musa Al-Ash'ari:

The Prophet (ﷺ) said, "Give food to the hungry, pay a visit to the sick and release
(set free) the one in captivity" (by paying his ransom). (
Bukhari 5373)
Happy Monday!

LIVE: FAINALI Za Kuhifadhi QURAAN - Diamond Jubilee

Tis the season of Qur'an competitions.
International Qur'an Competition in Tanzania.
I love this, Qur'an competitions everywhere.
Mashaallah! Good luck to all the participants, you are all winners.

Update:
Top 3 winners for the International Qur'an competition, even though it was a tight race are:
1. Zakaria Sheha Ally (16) from Tanzania won $5,000
2. Gaffari Mohammed (14) from England won $4,000
3. Shamsi Mwalimu Said (19) from Tanzania won $3,000

Friday, May 24, 2019

Aya ya Leo - Tafakari (Reflections)

Petra, mji wa zamani Jordan, ambaye nyumba zake zilijengwa ndani ya majabali.

Je! Hawatembei katika ardhi wakaona ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua
ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyo istawisha wao.
Na Mitume wao wakawajia na dalili zilizo wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.

Have they not traveled through the earth and observed how was the end of those before them? They were greater than them in power, and
they plowed the earth and built it up more than they have built it up,
and their messengers came to them with clear evidences. And Allah would not ever have wronged them, but they were wronging themselves. (Qur'an 30:9)
(Jumaa Mubarak!)

Tuesday, May 21, 2019

Hadithi ya Leo - I'tikaf (Kuhamia Msikitini kwa Ajili ya Kumtukuza Allah) - Retiring to a Mosque for the remembrance of Allah



Imehadithiwa na Abu Huraira:

Mtume alikuwaga anafanya I'tikaf(Kuhamia Msikitini kwa Ajili ya Ibada) kila mwaka mwezi wa
Ramadhani kwa siku kumi, na ule mwaka wa kifo chake, alifanya I'tikaf kwa siku ishirini.

Narrated Abu Huraira:

The Prophet (ﷺ) used to perform I`tikaf every year in the month of Ramadan for ten days,
and when it was the year of his death, he stayed in I`tikaf for twenty days.
(Bukhari 2044)

Monday, May 20, 2019

Top 5 winners from the Qur'an competition in Tanzania



5. Sumayyah Juma Abdallah from Tanzania  won 4 million Tshs.
4. Idrissa Ousmane from Niger won 5 Million Tshs.
3. Shamsuddin Hussein Ali from Tanzania won 8.5 million Tshs and a plot in kigamboni.
2. Faruq Karibu Yakubu  from Nigeria won 12 million Tshs.
1. Mouhamed el Moudjtaba Diallo from Senegal won 20 million Tshs and a free ticket to go to Hajj.

All participants received 200 dollars each. 
Mashallaah! Congratulations to the winners and all the participants.
Happy Monday Folks!

Sunday, May 19, 2019

Mashindano ya Qu'ran ya Afrika (Africa Qur'an Competition in Tanzania)


Usipitwe mambo ni moto moto. Lazima Tushinde mwaka huu.
Mashaallah! May Allah bless you all, you are all winners.

Friday, May 17, 2019

Aya ya Leo - Dua ya Nabii Musa (Prophet Moses's Prayer)


(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
Na unifanyie wepesi kazi yangu,
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
Ili wapate kuelewa maneno yangu.
Na nipe waziri kutoka kwenye familia yangu,
Harun, ndugu yangu.
Kwake yeye niongeze nguvu zangu.
Na umshirikishe katika kazi yangu.
Ili tukutakase sana.
Na tukukumbuke sana.
Hakika Wewe unatuona.

[Moses] said, "My Lord, expand for me my breast [with assurance]
And ease for me my task
And untie the knot from my tongue
That they may understand my speech.
And appoint for me a minister from my family -
Aaron, my brother.
Increase through him my strength
And let him share my task
That we may exalt You much
And remember You much.
Indeed, You are of us ever Seeing."
(Qur'an 20:25-35)

Jumaa Mubarak!

Thursday, May 16, 2019

Kutana na muimbaji wa Qaswida kutoka Jumuiya ya Madrassa za Ugweno

Interview ya Suleyman Massanza muimbaji wa Qaswida kutoka Madrassa za Ugweno.

Tuesday, May 14, 2019

Qaswida kutoka Uingereza Leo -Sami Yusuf - Make Me Strong

Njia yako ni ndefu na ina mitihani, sasa unamuombaje Mola wako akufanyie wepesi?


Monday, May 13, 2019

Hadithi ya Leo - Kumlipizia Marehemu Fungo la Ramadhani (Repaying Missed Ramadhan Fasting Days for the deceased)


Imehadithiwa na Aisha:

Mtume wa Allah alisema, "Yeyote aliyefariki na alitakiwa kulipa (Siku ambazo hakufunga mwezi wa Ramadhani) basi ndugu zake wanatakiwa kufunga kwa ajili yake."


Narrated `Aisha:

Allah's Messenger (ﷺ) said, "Whoever died and he ought to have fasted (the missed days of Ramadan) then his guardians must fast on his behalf."
(Bukhari 1952)

Happy Monday and Second Week of Ramadhan!

Sunday, May 12, 2019

Iftar from the Prophet's Mosque (Al Masjid An Anabawi)

Futarii kutoka Msikiti wa Mtume. 
Mashaallah, hakuna mtu kukosa futari hapa.
Don't you just wish you were there right now.
Sema muda ukikaribia tunakuwaga tuna hesabu dakika.

Mwenyezi Mungu Awaongezee wanaojitolea kufuturisha pale walipopungukiwa na azidi kuwashushia baraka zake.
Mnaamka kula daku lakini, maana imejaa baraka tele, usikubali kupitwa nazo.

Saturday, May 11, 2019

Je Unapelelezwa na Simu Yako?

Lets get Educated! 
Jinsi ilivyo rahisi kuhack simu zenu za mkono.
Je! unatabia za ku download apps kwenye simu yako ya mkono mara kwa mara? Basi hii video inakulenga wewe. Facebook wanapelekeshwa kila siku na serizali za wenzetu, kwasababu wanachukua habari nyingi sana kutoka kwenye simu yako zaidi ya wewe unavyodhani.

Hizi app zinaweza ku access camera yako , mic yako ya simu na accounts zako za hela kama Tigo pesa na kadhalika. Hatari kweli, inabidi uwe muangalifu sana ni link gani una fungua kutoka kwenye simu yako, na ni apps gani una download.

Jamani Weekend ya kwanza ya Ramadhani Alhamdullillah tunaimalizia! 
Mwenyezu Mungu atuwezeshe tuweze kumaliza Ramadhani yetu salama. Msisahau kuwechekeni majirani zenu jamani ambao majiko yao hayawakagi mara nyingi.

Friday, May 10, 2019

Aya ya Leo - Mazuri yanatoka kwa Allah (Goodness is From Allah)



Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu [Ewe Binadamau] linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma [Ewe Muhamad] kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha.
 
What comes to you of good is from Allah, but what comes to you of evil, [O man], is from yourself. And We have sent you, [O Muhammad], to the people as a messenger, and sufficient is Allah
as Witness. (Qur'an 4:79)
 
Happy First Friday of Ramadhan!

Thursday, May 9, 2019

Futariii Bureee China na Silent Ocean

Jamani makampuni yakifanya vitu vizuri namna hii, kwakweli tutawapa free promo.

Mashaallah! Mashaallah! Ni Mfano wa kuigwa. Inasaidia sana ukiwa mgeni kwenye nchi za watu.
Mwenyezi Mungu awaongezee pale walipo pungukiwa na azidi kuwafungulia milango yao ya kheri.

Wednesday, May 8, 2019

Msomi wa Leo - Al Būsīrī (1212-1295)

Abu Abdullah Muhammad ibn Sa'īd ul-Būsīrī Ash Shadhili  Almaarufu Al-Busiri, alizaliwa Misri mwaka 1212. Al-Busiri alipata elimu yake ya dini chini ya Sheikh Al-Mursi Abu'l-'Abbas, Alikuwa anajulikana kama Mshairi Maarufu sana Misri.

Al-Busiri japukuwa alikuwa ni Mshairi wa Misri, familia yake ilitokea Moroko. Alianza kuandika Mashairi yake chini ya Ibn Hinna vizier wa Misri. Aliandika mashairi mengi lakini Mashairi yake maarufu ni Qasida al-Burda. Qaswida hizo tunazisikia mpaka leo kwenye maulidi na maharusi, na washairi waliokuja baada yake, bado wanazitumia mashairi yake kama misingi ya mashairi yao. Qaswida zake ziliweza kutafsiriwa kwenye lugha tofauti na zikakuza ukubwa wake. Busiri alifariki mwaka 1295 mjini Alexandria, Misri. 

Sikiliza moja ya Qaswida kwenye kitabu chake cha Qasida Al-Burda.


Mwenyezi Mungu Amuwekee Nuru Kwenye Kaburi lake na Amuinue daraja kwenye Pepo yake. 


Tuesday, May 7, 2019

Qaswida ya Leo kutoka Uingereza- Sami Yusuf

Swali Je Umejitayarishaje ukiitwa na Mola Wako?
Question, How well have you prepared yourself when your called back by your Lord?




Hebu tutafakari kidogo kwenye Mwezi huu Mtukufu.

Monday, May 6, 2019

Hadithi ya Leo - Muda wa Kufunga (When to fast)



Imehadithiwa na Abdullah bin Umar:

Mtume was Allah alisema, " Mwezi unaweza kuwa usiku 29, na msifunge mpaka muuone mwezi, na kama kuna mawingu, basi malizieni siku thalathini ya Sha'ban."

Narrated `Abdullah bin `Umar:

Allah's Messenger (ﷺ) said, "The month (can be) 29 nights (i.e. days), and do not fast
till you see the moon, and if the sky is overcast, then complete Sha'ban as thirty days."
(Bukhari 1907)

Sunday, May 5, 2019

Ramadhan 2019 Kareem!

Ramadhan is here and oh how exciting . 


For those Starting on Monday, may it be a blessing for you and your family and for the rest of us starting on Tuesday, Happy last day of Shabaan and may we all celebrate Eid together.