Pages

Wednesday, June 14, 2017

Msomi wa Leo - Ibn Arabī

Abū 'Abdullāh Muḥammad ibn 'Alī ibn Muḥammad ibn `Arabī al-Ḥātimī aṭ-Ṭāʾī, alizaliwa Murcia, Spain tarehe 26 Juli 1165. Ibn Arabi alikuwa ni Mwandishi na Msomi mzuri wa dini.

Alianza elimu yake Seville mwaka 1182-1183. Walimu wake walikuwa ma imaam wa karne ya Almohad na wengine walikuwa ma qadi au khatib. Imaam wake wa dini alikuwa
Sheikh Mohammed ibn Qasim Al-Tamimi wa Morocco.Alimaliza masomo yake Morocco mwaka 1200 chini ya mwalimu wake Yusuf Al-Kumi.

Mwaka 1201, Ibn Arab alienda Hija, na akaishi Makkah kwa muda wa miaka mitatu. Hapo ndo alipoanza kuandika kazi yake ya Al-Futuhat al-Makkiyaa.
Baada ya kukaa Makka, alitembelea sehemu nyingi za Syria, Palenstine, Iraq,Anatolia, Baghdad na Madina. Ibn Arabi aliandika vitabu vyake Tanazzulāt al-Mawṣiliyya, Kitāb al-Jalāl wa’l-Jamāl na Kunh mā lā Budda lil-MurīdMinhu, alipoenda kutembelea Mosul na kufunga Ramadhani yake hapo.

Ibn Arabi aliendelea na safari zake na akatembelea Jerusalem, Makka, Misri, Aleppo na Damascus. Mwishoni alirejea Makka ambako aliendelea masomo yake na kudandika kwa muda wa miaka 4 hadi 5, na ni kwenye hii miji ndipo pia alikuwa akifanya ziara ya vitabu vyake. Alifariki dunia tarehe 8 Juli 1240.

Mwenyezi Mungu amsamehe madhambi yake na amlaze mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment