Pages

Sunday, June 5, 2016

Ramadhan 2016 Starts on Monday June 6th

Hurray! We start fasting tomorrow on Monday the 6th, so tighten those belts and let's do it right this time.  The moon sighting committee of UAE and Saudi have announced the moon was sighted in the region on Sunday June 5th. The Fiqh council of North America have also announced Ramadhan to start tomorrow. Let's wipe out our sins on the first 10 days of mercy in'shaa'llah.

Mwezi umeonekana uarabuni na wametangaza Ramadhani unaanza kesho Jumatatu Juni 6. Fiqh council ya Marekani pia wametangaza mwezi wa ramadhani kuanza kesho. Na nimesikiliza Radio Ihsan, Mwenyekiti wa  Baraza la wana Sunna Tanzania akitangaza Ramadhani kuanza Kesho, Kutokana na taarifa za Mwezi kuonekana sehemu mbali mbali ikiwemo handeni Tanga. Kwa hiyo wandugu tunaanza kufunga kesho, tujitahidi tufanye mema ili madhambi yetu yafutwe kati ya siku kumi hizi za mwanzo za msamaha.

Mwenyezi Mungu akubali funga zetu, akubali sala zetu, atusamehe madhambi yetu na atulinde na mabaya ya hii dunio, adhabu ya kaburi na moto wa Jahaman.

May Allah forgive Accept our fast, accept our prayers, forgive our sins and protect us from the bad of this world and the fire of hell .


Update!
Nimepata Habari Sheikh Jongo Kadhi wa Dar Es Salaam katangaza kwenye Radio Kheri kwamba Ramadhani inaanza Jumanne. Haya Ramadhani Njema kwa ndugu zangu watakao anza Jumatatu na wale pia watakao anza Jumanne. In'Shaa'llah Mwenyezi Mungu atufanyie wepesi.

Happy Ramadhan to everyone starting on Monday and also those folks starting on Tuesday.

No comments:

Post a Comment